Waraka wa kwanza wa C.T.U kwenda kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
Habari kiongozi Dr Faustine Ndugulile ndugu pole na majukumu ambayo umekuwa ukiyapitia naona umeanza vizuri katika utendaji kazi wako.

Binafsi natamani nipate wasaa wa kukaa na wewe kukueleza machache ambayo sisi watu wa Startup tunapitia nchini.

Kwanza kabisa napenda kupongeza jitihada za Serikali hii ya awamu ya tano katika kuboresha uchumi na kufanikiwa kuingia katika uchumi wa kati kiukweli Rais Mh Dk John Pombe Magufuli anatakiwa kupongezwa kwenye hili.

Mie binafsi ni mmoja wa wapenda maendeleo katika nchi na katika hilo nimebuni mfumo teknolojia wa mtu kuweza kusikiliza vipindi vya redio duniani uitwao DUNDA.

Sasa katika kubuni mfumo wa DUNDA NIKIWA NI MTANZANIA NA NIKIWA TANZANIA nimegundua mambo mengi ambayo nitakuletea kwako kwa ajili ya uboreshaji kwa mambo kadhaa wa kadhaa.

Kwa kuwa DUNDA ni mfumo ili niweze kufanya kazi ni lazima nisajiri Brela well and good ili kuweza kupata Tin number na maswala ya TRA kwani DUNDA mwisho wa siku ni lazima ilipe kodi ambapo katika ku register kampuni ya technology napenda kuwapongeza kwani Serikali imeboresha brela kwa kiasi kikubwa.

Baada ya ku register STARTUP tunapata ugumu kwenye kuendesha kampuni hiyo ambapo hapa Mh waziri huwa ni machozi, Jasho na damu.

Kwanza kabisa tunapata shida kwenye kupata office Mh Waziri japokuwa yapo makampuni yanayojinasibu kuwa wao wanatoa co working spaces, kwa maana makampuni ambayo makampuni yanayoshindwa kuchukua office hulipa kiwango kidogo kupata office ambapo hupewa meza na dawati kama office Mh Waziri kiwango hicho bado ni kikubwa sana unakuta Mh Waziri unapewa dawati la mtu mmoja kwa Tsh laki tatu (300,000) bado ni shida

Mh waziri nina wazo katika hili Wizara imehamia Dodoma tunaomba Jengo la wizara ya teknolojia na habari Dar Es Salaam tupate hata floor moja ambayo Startups tunaweza kuwa na office zetu hata kwa desks

Mfano unatengeneza Desks 100 pale na gharama inakuwa let's say 100,000 kwa mwezi na ni lazima iwe startups tu yaani uwe na mfumo wako wa teknolojia unapewa pale Desk sehemu kama ile ikiwa na wawekezaji wanakuwa wanakuja pamoja na wadau kuweza kuona ideas mbalimbali, niamini mimi kutakuwa na ideas mbalimbali za vijana ambazo zitakuwa kubwa sana

Kuanzishwa kwa TTIC (Tanzania Tech Investment Center )

Mh waziri pia kuna shida ya uwekezaji, ni dhahiri kuwa hakuna startup ambayo inakopesheka benki sababu kubwa ni kwamba startup uwekezaji wake ni kupitia Equity Financing, convertible note ambapo banks zetu wao they dont accept what they do they provide loans with collateral

So wanachofanya hawa startups ni kutafuta wawekezaji nje ya nchi na kwakuwa bado hakuna Startup Ecosystem nzuri iliyojengwa ni ngumu sana kupata funds, ukiangalia TIC imelenga zaidi kuleta wawekezaji ambao sio wa kuwekeza kwenye startups wao ni Foreign Direct Investment sana sana so ni vyema kukawa na kuanzishwa na TTIC ( Tanzania Tech Investment Center) kwamba ni Taasisi malumu ambayo ina promote Startups za Tanzania kwa Angel and Venture investors Duniani

Startups kama DUNDA nikianzisha na nikifanya MVP naipeleka details TTIC then na wao wana promote kwa wawekezaji duniani kumbuka kuwa itakuwa rahisi kwa startups hizi kupata funds kwani TTIC ambayo ni kama mlezi na since ni Government Entity, TIC yenyewe itabaki na mfumo wao wa uwekezaji

Uchunguzi wa utitiri wa Hubs

Mh Waziri kumekuwa na utitiri wa Hubs mbalimbali ambazo zimekuwapo zikijinasibu kuwa zenyewe zinasaidia Tech Ecosystem kwamba zinasaidia Startups kupata funds na etc

Mh Waziri Zipo baadhi ya Hubs zimetengeneza mfumo wa kuwa wao ndio middleman na investors, Mh Waziri chunguza Founders wa Startups wamekuwa Daraja ya kupiga hela kwa Hubs hizi, founders wanalia kimya kimya hebu fanya uchunguzi utabaini kuwa kuna wajanja wameteneza mchongo wa kupiga hela kupitia startups yaani na nyingi zimejazana kijitonyama na mikocheni pale wanajijua

Mfumo wa malipo

Mh Waziri Mfano DUNDA ni platform ambayo itakuwa ipo Marekani, Ulaya , Australia maanana yake wateja wengi ni Wazungu maana yake wazungu mfumo wa malipo ni kupitia Credit Card na ili alipie kwa Credi Card ni lazima kuwe na mfumo strong wa security so ni lazima DUNDA ifanye integration na mifumo ya malipo kama vile

Stripe na PayPal

Sasa stripe haipo Tanzania lakini kampuni ya Tanzania inaweza kufungua account Stripe kupitia stripe atlas kwa kusajili Marekani kupitia Delaware corporation

Akapewa
• STRIPE ACCOUNT
• ACCOUNT YA BANK YA MAREKANI
• NAMBA YA MLIPAKODI WA MAREKANI
• REGISTRATION IN USA
Sasa basi vijana wengi wanaogopa kwenye utawala huu kufanya hivyo wakiogopa kupigwa money laundering na uhujumu uchumi

Mh waziri tunaomba kama inawezekana Stripe kuwepo Tanzania au Stripe Atlas kuwa integrated na bank za huku kwamba DUNDA nikilipwa Kwa Marekani ni lazima ni transfer hela kwenye account ya Tanzania ambapo Serikali ikaangalia namna ya kuchukua Kodi yake

Ni marakumi equivalent ya kodi jumla ya USA na Tanzania ikawa asilimia hadi 28 lakini mifumo ikawa mizuri

PayPal

Mh Waziri hili limekuwa ni kilio cha muda mrefu hebu kaa na BOT kuona namna ambavyo Startups ndizo ziruhusiwe kutumia PayPal yaani ili niwe na PayPal ni lazima
• Niwe na kampuni ya teknolojia ambapo nature ya malipo ya wateja ni kama DUNDA yaani kupitia credit cards
• Lazima uwe na mfumo ambao unauza nje ya nchi na imehakikiwa na imeoneka ni sahihi
• Lazima kila transaction details nawasilishe BOT

DESIGN AND BUILD A STARTUP ECOSYSTEM

Mh ni vyema tukiamua kama nchi kubuni na kujenga startup Ecosystem kama nchi hii itasaidia vitu vingi mno
• Itasaidia kampuni zetu kupata wawekezaji wa kimataifa
• Itasaidia kuwepo kwa kampuni nyingi za technology
• Itasaidia kuwepo na muingiliano wa wafanyakazi wa technology hivyo kusaidia kubadilishana uzoefu
• Itasaidia kampuni nyingi kuingia fedha hivyo kulipa kodi

Mh waziri najua una kazi nyingi lakini naomba siku uweke kikao uzungumze na startups mbalimbali zilipo nchini utayabaini mengi ambayo ulikuwa huyajui


Nawasilisha
 
Nimesoma kwa uzuri, naona mantiki kubwa ni mazingira bora ya uwekezaji katika teknolojia na mifumo thabiti.
 
Mkuu fikisha ofisini kwa waziri Mtumba Dodoma naamini atalipokea, jamaa yuko smart sana
 
Back
Top Bottom