Black Walker
Senior Member
- Oct 8, 2018
- 107
- 238
Naomba kuwasilisha hii hoja kwa Mheshimiwa Rais, waziri wa ajira na kazi, waziri wa utumishi na waziri wa Tamisemi.
Kuna hili kundi la wanandoa ambao ni wajiriwa wenu na wametanganishwa wako wanakaa mikoa au wilaya mbalimbali kiasi kwamba hawapati muda mzuri wa kuwa pamoja kama wenza muda mwingi wanapitia magumu ya kisaikolojia na matatizo mengine kwa familia zao.
Hali kama hii, na changamoto nyingine nyingi wanazopitia haipaswi kuchukuliwa kwa ukawaida bali izingatiwe kwamba na wao sasa wanastahili kupatiwa posho ya mazingira magumu kila mmoja.
Posho hii itakuwa inatolewa kwa hawa wenza kama kifuta jasho na itakoma pale ambapo mmojawapo atafanikiwa kuhamia kwa mwenzake.
Ikumbukwe kwamba tunaoana kwa lengo moja kubwa la kuwa pamoja na wenza wetu ili tuweze kutatua matatizo yetu tukiwa pamoja kitendo cha kutenganisha ni kama mmoja amerudishwa kwa wazazi wake.
Hali hii imepelekea leo ndoa nyingi kuvunjika na malezi ya watoto kuyumbayumba, mbali na hapo pia imepelekea maendeleo ya familia kusuasua kwani kumekuwepo na mgawanyo wa kipato na tena usiombe kwa wenye mishahara ya kawaida/chini.
Hali ya maumivu makali wanapitia watumishi wa kawaida lakini kwa maboss zetu kwa kutambua umuhimu wa ndoa, akihama anahama na mwenza wake.
Mbaya zaidi unakuta wanaweka vigezo eti ukitaka kuhama utafute mtu wa kubadilishana nae! Huu nao ni uonevu kama uonevu mwingine.
Fikiria maumivu ya ndoa kuvunjika.
Fikiria maumivu ya mzazi mmoja kukaa mbali na watoto wake kwa miaka, hisia za upendo wa watoto hudhihirika bayana pale wanapotuona na pale unapoaga ukienda kuwasalimia kipindi cha likizo. Ukiondoka vilio hutanda kama unaenda kufa na hawatakuona tena, yote haya ni maumivu.
Fikiria pia migogoro ya hapa na pale ambayo chanzo chake chaweza kuwa huo umbali.
Maumivu ya wenza kuleteana magonjwa n.k
HIVYO POSHO YA MAZINGIRA MAGUMU NI MUHIMU na endapo litatekelezwa waajiri wengi hawatakuwa wanakalia mafaili ya watu kwa muda mrefu bila kupitisha maombi yao maana watakuwa wanaogopa hizi gharama.
Karibu ni kwa michango.
Nawasilisha.
NUKIA KIBABE ISHI KIUNGWANA.