Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 1,971
- 4,141
Shalom shalom
Hekoheko marafiki na mashabiki wa klabu ya Union Sportive de la Médina d'Alger maarufu kama USM Alger au USMA. Mara baada ya kuibamiza klabu ya Asec mimosas hapo jana jijini Algers nchini Algeria kwa kichapo kizito cha mabao mawili bila ya majibu ,tunarejea tena kuwawinda underdog (mbwa waliochini) kutoka nchini Tanzania, klabu ya Yanga Afirika katika fainali yq mkondo wa kwanza itakayopigwa jijini Dar-es-salaam kabla ya kwenda kumaliza mauaji yatakayofanyika jijini Algers ndani ya dimba la Stade du 5 juillet katika fainali ya mkondo wa pili na kisha kutawazwa kama mabingwa wapya wa kombe la shirikisho barani Afrika.
Kama kawaida hatoki mtu katika dimba letu hili la olimpic linalobeba watazamaji 95000.Ikumbukwe mara ya mwisho tuliwakanda Yanga Afirika mabao 4-0 hapa jijini Algers tulipokutana katika kundi D kwenye kombe la shirikisho mwaka 2018 ambalo klabu ya yanga ilikamata mkia na tunaimani tutawakanda tenda bao hizo nne zilizotukuka watakapokuja huku jijini Algers.
Ombi langu kwa mashabiki wa USMA tujitokeze kuipa hamasa timu yetu katika mchezo wa kwanza wa fainali utakaopigwa katika uwanja wa mkapa jijini Dar-es-salaam.
Asanteni