mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,855
- 8,253
Nakwera na tabia sugu ya jamaa wanaosha magari pembezoni mwa barabara ya Shekilango Sinza hasa kuanzia eneo la Mori hadi City Food restraurant mbele kidogo kwenye kituo cha mabasi pale kwa Remi,madhara ya uoshwaji huo wa magari ni
1.Bara bara inamong'onyoka na madimbwi ya maji yamefanya mashimo makubwa(kwenye sehemu ya waendayo kwa miguu) kiasi kwamba wapita kwa miguu sasa hupita kwenye barabara kuu yenye magari ambapo ni hatari kwa usalama.
2.Magari yaoshwayo huziba njia ya wapita kwa miguu
3.Kumwagiwa maji machafu pale upitapo karibu kwani jamaa wanapomwagia gari(kusafisha )hawaangalia kama kuna watu wanapita.
Pendekezo langu ni kwa mamlaka zinazohusika kukomesha hili jambo kwanza kwa kuyashika magari yanaoshwa hayo maeneo,na kutoa faini kubwa kwa kufanya hivyo naamini hakuna mtu atakayepeleka gari lake lioshwe hapo na waosha magari watakosa magari ya kuyaosha.
Mwisho tunawaomba wenye magari jamani hayo magari mnaweza kuoshea majumbani kwenu au sehemu maalumu za kuogesha,tutunze barabara zetu na mazingira kwani wenye magari ndio mtakuwa watu wa kwanza kulalamika barabara ikianza kuwa kama mashimo ya Tora bora au Kandahar