Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Zitto, Mbunge hawezi kuwa mtendaji, na hapaswi kuwa mtendaji. Jukumu lake lake kubwa ni kutunga sheria na kuisimamia serikali. Tatizo tulilonalo ni kuwa wabunge wanafanya kazi ya kutunga sheria sawasawa, tatizo kubwa ni kwenye kuisimamia serikali. Kwa maana ya kwamba wao wakiwa ni wawakilishi wa watu wana uwezo wa kuhoji na kutaka maelezo ya kina kuhusu jambo fulani. Endapo jambo fulani katika utendaji haliendi wanavyotaka wanauwezo wa kulitungia sheria na kulibadilisha au wakati wa bajeti kulikatia pesa (the so called power of the purse). Ina maana gani, kama Wabunge wangeona kuwa Rada haitustahili wangegomea kuitengea pesa? Kama wabunge wanaona vijana Ukraine wanastahili ile ahadi ya serikali na mikopo yao waliyonyang'anywa basi wabunge wangeweza kuwatengea fedha.
Nakubaliana na wewe kuwa haiwezekani fedha zinazotakiwa kutumika kwenye majimbo yao zipitishwe kwa wabunge. Wao si watendaji na hawastahili kuwa watendaji. Pesa zozote wanazoomba kwa ajili ya majimbo yao ni lazima zipitishwe kwa watendaji, halmashauri, kata, n.k but never kupitia ofisi zao.
By the way, kwanini kati ya watumishi wote wa jamhuri yetu wabunge peke yao ndio wawe wanajipangia mishahara, posho na marupurupu mengine? Hata Rais hajipangii mshahara!!