wanayakyusa kwa kujidai hadi kwenye lugha, mweeeeeeee!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Tunapodai wamasai, wairaki (wambulu), wandorobo na wahadzabe sio wabantu ni kutokana na miundo na sauti ya maneno ya lugha zao. Lakini kuna hili la Wanyakyusa la kujidai eti baadhi ya vitu kuvitamka kwa kiingereza kama lugha yao ya Kinyakyusa.

Hivi ni kweli hawa jamaa wanapotamka baadhi ya vitu kwa Kiingereza wakidai ni kinyakyusa ni sawa au ndo maringo yao tu pengine waonekane na wao matawi kwa kuwa lugha yao inafanana ya waingereza?

Hebu angalia mifano hii:
Kijiko wanaita -spoon
shule wanaita -skul

Hii imekaaje jamani, kama sio kujidai ni nini hasa? Nyie wanyakyusa hebu tujuzeni!
 
Unataka kuleta bifu hapa jamvini,...anyway kijiko kinaitwa lefani(sio spoon)...shule kidogo imenitoka ngoja ntarudi kukupa jibu mkuu......ila acha mashambulizi
 
Unataka kuleta bifu hapa jamvini,...anyway kijiko kinaitwa lefani(sio spoon)...shule kidogo imenitoka ngoja ntarudi kukupa jibu mkuu......ila acha mashambulizi

nnachoongelea kwa yeyote ambaye ameishi au kusikia wanavyoongea hawa shemeji zangu, takubaliana nami kama sio mbishi
 
Kanisa= tempeli (temple)
sabuni= sopo (soap)
wanyaki nadhani ndio watu wa kwanza kutohoa kutoka kwenye Kiingereza na kuingiza kwenye lugha asilia
 
Hapo red ndugu yangu. What makes us non-Bantu is because were are not....sio tu mundo ya sauti na maneno...it is that our languages are different totally.....in every lingusitc aspect with Bantu...

There are many language families in Africa- Niger Congo of which the Bantu is th elargest group; Nilo Shalaran, Cushitic, Khosaic etc.....this is what identifies people to be who they are....sio sauti kwani sauti watu wanaweza kuiga
 
pipi =sweet shuka=sheet kiukwel kabisa baadhi ya hayo maneno yametohoa kwenye kiingereza hii ni kutokana na muingiliano kati ya wanyakyusa na waingereza (wamissionary) walikuja kueneza dini hasa mbeya sehem za igale ndo wamissionary wa kwanza kuneza thehebu la pentecoste
 
Acha wajidai wanawake wakinyakusa watamu bwana asikwambie mtu na wakipenda wanajua mapenzi siyo wanyakusa wa maji chumvi hao ni wezi!!
 
hama nenda kwingine. Unafikiri wote wanapenda mvu inyeshe pale wanapoishi? waulize mods why wameiweka hapo
Ndyoko, ulikosea kuiweka MMU si unaona sasa imehamishwa sikuwa
na nia mbaya na Thread yako.
 
Lazima turinge na kujidai bwana, nahisi wazungu walikuwa wengi sana huku unyakyusani na ndo maana yakatokea haya!
 
Lugha yoyote hai lazima inakuwa na kukuwa kwa lugha ni kutohoa maneno ambayo awali hayakuwemo kwenye lugha husika na kuyaingiza kwenye lugha ili watumiaji waende sambamba na kukua huko.

Chukulia mfano wai lugha ya kiswahili:

shule........ kijerumani
meza ........kireno
mvinyo ......kireno
chai .........kihindi/kichina/kituruki
hela......... kijerumani

Kwa maana hiyo hatuwezi kusema kuwa wanaongea kiswahili wanaringa, si kweli
 
Back
Top Bottom