Wanawake wengi wamekuwa wahanga wa makanisa, msishangae kuona anagawa mali zote kwa mchungaji wake

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,153
Ninao ushahidi wa ndoa kama nne zimekufa sababu ya hawa called dady my dady ma...

Hawa ni pastors wanatumia udhaifu wa kina mama kuwaibia mali zao na wanapojua una hela basi mume ujipange yaani kilicho chako kifiche kama ni hati ficha mbali kwa ndugu zako

Nimekaa nikawaza hawa wanakuwa wamelogwa ama ni ujinga wa mtu binafsi. Galsha langu nalo siku moja alingia chaka akapata hela zake akaenda kugawa kanisani akaanza na pastor, akafuata waumini gafla naona anaanza kuomba nauli, nauliza anasema amekopesha watu kanisani wanalipa na riba

Ni miaka 5 iliyopita baada ya mwaka lile kanisa likasambaratika mchungaji aliyekuwepo akahama akanzisha kanisa chini ya jina lingine Bunju huko, washarika nao wakasambaratika.

Mwanamke namkuta analia machozi siku tatu ukiuliza hasemi, kha nikauliza mama mkwe ongea na mwanao kama anaumwa twende hospitali wapi. Baadae inafika Jumapili haendi kanisani hapana sitaki kusikia kwa sasa ni shida kubwa alikaa miezi minne hataki kanisa mwisho akahamia kanisa la mbali, sitaki kukumbuka

Nimeona sehemu mume kaenda kudai mahakamani milioni 15 mke alizopeleka sehemu kwa dady. Hawa ma dady wengi ni matapeli.

Kuna mmoja namsikia redioni usiku wa manane yaani anapanga watu usiku wa manane wanampigia wakiomba ndugu yao kafariki

Kama jana nimecheka sana, ati dady dada amefariki.
Pastor; nenda nje naona kuna mwembe chukua maji na chumvi mwagia baada ya dk tano kuna bundi na paka watadondoka toka juu na popobawa.

Dada aliefiwa; dk 2 nyingi unasikia dady dady bundi kadondoka na paka toka kwenye mwembe dady tusaidie

Mdada akaambiwa chukua kitambaa weka usoni mwa marehemu niombe.

Sekunde unasikia dady dady anapiga chafya anachezesha miguu

Uwii nimecheka jamani hii dunia ina wajinga kweli.

Akaambiwa kafufuka kafuka jamani ok mkalishe. Ghafla unasikia dady anaomba maji jamani marehemu amefufuka anaomba maji. Aiseeee Allah atunusuru

Mwisho nahitaji kuwaona leo asubuhi mapema ofisini pls.

Huyuhuyu Jumamosi iliyopita usiku wa manane akasema amefufua mtu

Mbona mnafufua usiku wa manane tu na si mchana ama mchana hawafi?

Wamama mbadilike, madada mbadilike.i
 
😂😂Niliona kanisa moja la mtandaoni jina kapuni.

Kuna wanawake kama 6 hivi wamekuja kubadili dini ,eti walikuwa waislam na wamevaa ninja kabisa na kujitanda ....kama kweli waislamu wanavaa ninja na wewe ushapanga kuwa mkristo kuna haja gani ya kuvaa ninja na hawaonekani hata sura 😂😂..

Nimecheka sana .
 
Pdidy kama kawaida unaendelea kutupia nyuzi, na angalau mwandiko wako unazidi kuboreka.
 
mkuuuuu minasema wale wanaloga pia wangu wakati anafanya umbombo miaka 5 iliopita ana mastersya udsm..elimu sio ukijaa kwenye mfumooo imooo
Kuna elimu ya dasaran na ambayo haikufanyi ujikomboe kifikra.
 
Back
Top Bottom