Wanawake wapigwa na kudhalilishwa, watishiwa kuuwawa na wamiliki wa yard ya kuvuta magari jijini

hapo kwenye bold umekosea sana, unazani anajali????? Kwani nani alikuambia sasa ivi tanzania tuna serikali??? Tuna washehereshaji tu. Kama huyo rahisi wako hakujali vifo vya watu kutokana na mgomo wa madaktari kwa zaidi ya wiki tatu, sembuse huyo mwanamke kunyanyaswa kijinsia? Nothing will happen, kwanza ndo kesho anaruka kwenda ........................!!!!!

[/b]
huyo mkuu wenu wa kaya siku ya mabomu watu wamekufa akawa anaongea huku anacheka cheka
 
watanzania kadhaa leo wakiwemo wanawake na akina mama wamepigwa , kudhalilishwa , kuibiwa pesa na kutishiwa kuuwawa na wamiliki wa yard fulani yenye kazi ya kuvuta magari yanayopaki vibaya jijini
mtiti ulianza pale watu hao walipokuwa wamepaki vibaya magari ndipo wafanyakazi hao wakaja kufunga na kuvuta magari hayo wale kina dada wakaanza kuyafuatilia kwa nyuma mpaka kwenye yadi yao walipofika kwenye yard yao wale watu ambao magari yao yalikuwa yamekokotwa walianza kupokea kipondo kutoka kwa wamiliki na wafanyakazi wa kampuni sababu ni kisa kwa kuwa wale kina dada walilamakika kuwa magari yao yamekwanguliwa katika zoezi hilo la kukokota magari
wale wadada walipigwa, kushikwa matiti, na kutishiwa kuuwawa na mmiliki wa kampuni hiyo kwani alitoa bastola...
Kuna mpiga picha mmoja ambaye alijaribu kupiga picha alipigwa mpaka akavimba mdomo na kamera yake haijui ilipo
wale kina dada walipigwa mpaka wakashikwa matiti kuna mmoja kapoteza dola 30000
vile vile inasemekana kuwa wale wadada walivyofika kwenye yard hiyo walikuta kuna watu wengine wanapokea kipondo kutoka kwa wamiliki na wafanyakazi
hii inamaana kuwa hao wamiliki wa hiyo yard ni kazi yao kupiga watu na kuwaibia na kuwadhalilisha
hivi serikali inajua hili?
Inawezekana ni kampuni ya mtu mkubwa ndio maana jamaa ana jiamini kiasi hiki?
Inawezekana jamaa anajuana na wakubwa ndio maana anajiamini kiasi hiki?
Nashindwa kuelewa hapa tatizo ni nini mimi imeniuma na kunikera sana
hivi watu walio juu ya sheria kumbe bado wapo??
Je na wewe imeshakutokea hali kama hii??
Huu ndio style ya kufanya biashara jamani watanzania??
Naomba tulijadili na tulikemee hili.

Umeogopa nini kutaja jina la hiyo yard ? "jf where people dare to speak" Disclose kila kitu mkuu,
 
mambo mengine yanatia hasira sana
usishangae kukuta kumbe halmashauri wamekula 10%
sasa hiyo yard kuibia watu.

Au wanapopora kuna mahali wanapeleka cha juu....

Kwanza kazi hiyo kwanini wapewe vikampuni uchwara?
Dar wapi kuna parking? Wamezi-identify?
Huu ni ujambazi
 
nimesharekebisha kwa msaada wa wakuu nimepata jina la kampuni na nimelitaja hapo mwanzo kwenye thread
 
Ikipigwa kibao unatoa bastola? Hawa watu ni wababe sana tena hata hawaja weka vibao vya kukataza maegesho ya magari
Jamani taratibu tupunguze hasira,mie ningependa kusikiliza pia kwa upande wa pili wa mwenye yard alete utetezi wake hapa ili haki iweze kutendeka.Inawezekana hao wanawake waliochukuliwa magari wamemkata kibao mwenye yard akaamua atumie resource zake kujitetea kwa hiyo busara ni kusikiliza pande zote mbili ndio tutoe maamuzi yaliyo sahihi.
 
Bongo unaweza kuua mtu kiholela hivi hivi. Serikali iangalie hili jambo kiundani. Nashangaa kuna eneo gani lisiloruhusiwa kupaki gari maeneo ya sinza.
 
Dola 30000 anapanda nazo bodaboda ? tuwe wakweli wajameni labda kaibiwa simu na laki au dola 300 na mwandishi kakosea ?
 
kuna hawa jamaa wa breakdown na wale wa kufunga tairi kufuli wanakera sana ila hawa jamaa wa kufunga tairi kufuli magari siku moja waliingia choo cha kike walienda kufunga gari ya mbaba mmoja pale town yule mzee alivyokuja akakuta gari lake limefungwa kufuli akawaambie wafungue wakaleta jeuri jamaa hakuongea mara mbili alichukua bastola akapiga risasi kikufuli chao akawasha gari lake motoooo jamaa wakabaki mdomo wazi

tunakoenda kila mtu atakuwa na bastola
 
honestly hii thread imeniharibia mood yangu, nimewaza vibaya na nina hasira kali mno......
 
Wrong Parking iko kila nchi na taratibu za kuvuta gari zinafanyika kistaarab sana, ukishamaliza adhabu ya faini unakuta gari lako na vitu vilivyokuwa ndani vikiwa salaMa.

Iweje Iwe tofauti kwetu? Mtu anaburuza tu gari, analilwgeza lidondokee mtaroni, unahoji unapigwa, unaibiwa na sirini unashikwa??

Ushauri wangu kwa wahanga.
Kwa kuwa inaonekana hao jamaa wanajiamini sana, either sababu ya hela au ni mali ya kigogo, inaonekana ni dhahiri kabisa kuwa hata mahakama haitatenda haki. Maamuzi magumu yafanyike, chukua ndugu au marafiki pigeni hiyo yard na hao vijakazi plus boss mawe mpaka yaishe yote ardhini. Au watekeni waonje japo half of what u felt.

Unaleta utani na jasho la mtu, unaharibu gari kisa wrong parkin kwenye barabara ilochakachuliwa ilojengwa kwa kodi yangu?? Ingekuwa mimi hiyo breakdown ingekuwa ni majivu
 
kupark ovyo ni kosa kila mtu anajua na sheria za Tanzania ndio zinaruhusu kupika wapi na kuharibu magari yao kisa wamepark ovyo. jamaa wanashindwaje kufanya kazi kiuzalendo zaidi

Hii sheria ya kupaki Hovyo Haina nafasi hapa Dar es Salaam; Mimi swali langu ni rahisi na Wahusika wakuu ni Mkurugenzi wa jiji, Meya, Wakurugenzi wa halmashauri zote!! Je ni wapi wametenga maeneo ya kupaki magari Watu wakakataa kupaki? Hata maeneo ya kulipia? Sasa tunakomoana kwa Uzembe wa Planners!! Wote naomba tuwabane waonyeshe maeneo Yaliyotengwa kwa parking, Kila Kitongoji, Kata na katikati ya jiji Hata kwa malipo watu wakakataa kulipa?
 
Back
Top Bottom