"Wanawake/wanaume weusi wanajidharau sana"... je nikweli?

uku kwetu wanaume sijaona anayejichubua, labda wadada, wengi wa hivyo ni wanamusic na sijui nini kinawafanya kuamini weupe ndio dili

Mimi nijuavyo (Haijathibitishwa) wanaume wenye light skin (weupe) huwa kidogo hawana confidence kama waliyonayo weusi!.

thank you
kwa jamii zetu weupe ni sifa ya urembo,so ni sifa ya kike..
so mwanaume ukiitwa cheupe,ni tusi...
kuna jamaa mmoja ni mweupe na anafanana mno na will smith..
but akajipachika jina la kabaya....

mbona mimi mweuzi ile titiiiiiiiiii lakini naona niko kawaida tu maana ni matakwa ya Muumba?

Mungu katuumba wanadamu na kutupatia akili kumiliki na kutawala viumbe vyote vilivyopo ardhini. Mwanadamu katika uumbaji alikuwa mwa mwisho na baadae Mungu akapumzika na kuangalia vitu vyake vilivyo vyema machoni pake. Uumbaji huu wa aina yake, wa kufanana na yeye aliye juu umetukuka na yeye Mungu akaona vyema na akasema zaeni mkaongezeke mkaiijaze dunia.

Sasa cha kushangaza tunachokiona hapa duniani sasa hivi, wanadada wengi na wakak pia, wanabadilisha ngozi zao zilizoumbwa na mwenyezii Mungu kwa kemikali za kujipaka kwa hiari,wamezifanya ngozi zao kupauka na kuzifanya nyeupe si nyeupe, nyekundu si nyekundu ilimradi tu ni vichekesho huku mishipa ya damu ikionekena bayana. Loh Mungu wangu tuhurumie.

Kutokana na mikorogo, ngozi zao zimebadilika, ngozi ya kenge si kenge ni mabaka mabaka tu mwili mzima, tazama paji la uso jeupe,macho meusi mithili ya miwani ya jua, vifundo vya mikono na miguu vyeusi, ili mradi ni mikorogo tu ya rangi. Eti kisa ni mwenyezi Mungu kakosea kuwapa hao rangi nyeusi.

Achana na ngozi, nywele nazo kazi ni moja tu, unamwangalia msichana au mvulana inakuwa kama ni kichekesho, nyani si nyani, komba si komba, mbega si mbega, basi ilimradi yupoyupo tu. Watu wanahangaika na maisha, kwao mwenyezi Mungu amekosea.

Na ukiwaambia jamani mikorogo hii ina madhara kubwa kwa afya zao, hapo ndipo utapomjua mwanamke wa kibongo/mwanaume..."mwanga we, unanionea wivu we. Kama umefulia, tulia, na kwanza unikome kabisa" Watu hawa sasa hivi wamevuka mipaka na maadili.

sasa hivi wanatafuta uzuri eti wafanane na malaika wa Mungu, wanatumia vidonge na sindano, na hata kemikali za kukuza matiti na makalio..'toba' walah, hivi tunakwenda wapi jamani?? Yale waliyojaliwa hawaridhiki nayo, Mi naona kama wanamtusi Muumba wao.

Sasa maumbile yao yamewageuka na yanakuwa hayana tofauti na matairi ya nyuma ya trekta, yanakuwa ndembendembe, yanakuwa kama kinyago cha m-makonde uchwara.

Sasa hembu sikiliza hii ya firauni, baadhi ya wanaume wa kibongo licha tu ya mavazi yao ya kuvalia nguo mapajani a.k.a kata K-almaarufu, wao sasa wapo wanataka kujibadili ili wawe kama wasichana kimuonekano na nina uhakika kwamba wakipata fursa watatamani kuwa wanadada kamili.

Kuna wanakaka wengi licha ya nywele tu, wanapaka wanja na lipstick, na wengine kuchonga nyusi achilia mbali kubadili sauti na kutembea mithili ya kinyonga kama watoto wa kike.

Ili kujulisha ukweli huu wamedhihirisha kwa kujiita "MASHAROBARO". Hii ni nomino maana yake halisi ni msichana MREMBO. Anajipenda na kujisikia huku akitafuta kwa hamu KUPENDWA KWA HALI NA MALI. Hawa ni masharobaro wa kiume na si wa kike. Bora wangejiita MABAROBARO, Hali kidogo ingekuwa shwari.

Sasa cha kujiuliza uasi huu unatokana na nini?? Ee wabongo, ni ufinyu wa fahamu juu ya kile wanachokitenda ama?? Huu ni ulimbukeni wa kuiga hata visivyoigika, ni kasumba ya kuthamini vya wenzetu kuliko vyetu, ni ukosefu wa uzalendo, ni lack of confidence, ni utovu wa maadili na ushenzi uliopiliza.

Hii sio kazi ya shetani , ni utashi wa matunda ya wabongo wenyewe kwa jinsi maisha yanavyotubadilikia. Ni ukosefu wa shukrani kwa Mungu dhidi ya uumbaji wake. Ni dhambi na ni kufuru ya wabongo. hatujui tulitendalo.

WABONGO TUBADILIKE. wIKEND NJEMA!!
Kweli kabisa mkuu..

angela-maina.jpg

mbona huyu anatesa sana lakini siyo mchubuo????????????????????labda nywele za bandia ndizo waweza kumto maksi kidogo lakini amejaziliza kivyake hivi......

Mr. LittleX ..hoja yako inategemea na sehemu.. kwani kule kwetu South Sudan hatuna jinsi...

Lakini pia inategemea pia na akili ya mtu ..yaani inategemea kama kichwani kumejaa ubongo au makamasi..yaani kama upstairs "yaani kichwani" kukiwa original basi rangi sio issue ...lakini kama kichwani kumechakachuliwa na kuwekwa ubongo feki wa ki-china ..basi sehemu kubwa itakuwa imejaa makamasi na hivyo kupunguza uwezo wa kufikiri..na hivyo kama ukifanya test ya swali lako hapo juu jibu litakuwa positive..kwani binti kuwa mweusi anaweza kujinyonga..afadhali hata miguu ibaki pepsi na reception iwe Mirinda..

Mr. LittleX ..hoja yako inategemea na sehemu.. kwani kule kwetu South Sudan hatuna jinsi...

Lakini pia inategemea pia na akili ya mtu ..yaani inategemea kama kichwani kumejaa ubongo au makamasi..yaani kama upstairs "yaani kichwani" kukiwa original basi rangi sio issue ...lakini kama kichwani kumechakachuliwa na kuwekwa ubongo feki wa ki-china ..basi sehemu kubwa itakuwa imejaa makamasi na hivyo kupunguza uwezo wa kufikiri..na hivyo kama ukifanya test ya swali lako hapo juu jibu litakuwa positive..kwani binti kuwa mweusi anaweza kujinyonga..afadhali hata miguu ibaki pepsi na reception iwe Mirinda..

Unahoja nzuri!

South sudan kuna nini?(mean tujuze kidogo)

Hizi ni kauli sweeping na hazina facts zozote

Its just another discriminative "colour-thang" which in most cases is brought to disguise or bellitle a person after failure of understanding or expectations

endeleeni

Hata wazungu wenye ngozi nyeupe wanakaa juani au wanatumia tan kubadilisha rangi wasiwe weupe na ikifika masherehe ndio utawaona wengi wamebadilika rangi

Upo hapo ndio maisha hayo wewe kama haufanyi basi endelea na maisha yako achana na nani anafanya nini

Nduguzo waambie juu ya magonjwa ya ngozi though

Hata wazungu wenye ngozi nyeupe wanakaa juani au wanatumia tan kubadilisha rangi wasiwe weupe na ikifika masherehe ndio utawaona wengi wamebadilika rangi

Upo hapo ndio maisha hayo wewe kama haufanyi basi endelea na maisha yako achana na nani anafanya nini

Nduguzo waambie juu ya magonjwa ya ngozi though

Amaizng!

Back
Top Bottom