Wanawake wanaojitokeza misibani kudai walizaa na marehemu siku zote walikuwa wapi

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,198
3,572
Yaani mpka inafika hatua marehemu amefariki ndo unamuona mwanadada anajitokeza msibani akidai amezaa na marehemu wengine wanakuja na watoto msibani kutaka nao watoto kutambulika

Hivi siku zote Hawa wanawake wanakuwa wapi na nyinyi wanawake tabia za kuwaficha watoto baba zao mpka umauti unapata ndo mnajitokeza siku zote mnakuwa wapi ......

Nazungumza kwa sababu yametokea ndani ya ukoo wetu Kuna mwana Dada kajitokeza akidai Kazaa na ndugu yetu lakini upande wa pili mke na watoto wa ndoa umeleta Utata wamegoma kuwatambua huyu mdada yeye kwa Sasa anataka kwenda mahakamani kudai haki yake kwenye sehemu ya urithi upande wa ndugu wa marehemu hawajui wafanye nini maana marehemu hakuacha ujumbe kama alizaa njee

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Ukidate na mume wa mtu ukajiona unataka kuzaa jamani hakikisha unapewa urithi wako na wa mwanao kabla hujazaaaa just incase 😅😅😅
 
Sasa anamletea nani hapo.?unapozaa na mume wa mtu jipange in case of emergency.
Mimi siwezi kupokea mtoto wa mtu.
Amfufue huyo baba wamalizane
Ingawa kumleta sio jambo baya, walau mkae mkijua kuna damu yenu mahali.

Kuhusu alikuwa wapi....kwani huyo ndugu yenu naye alikuwa wapi?. Yeye ndiye alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo na sio Dada akajilazimishe kwa Watu.

Hapo kwa mirathi ni pagumu labda kama Marehemu alifunga naye ndoa...kinyume cha hapo ni kuungana na kuwa wamoja na kuangalia namna ya kusaidiana, haswa kwenye kumsomesha Dogo asiye na hatia.
 
Ukidate na mume wa mtu ukajiona unataka kuzaa jamani hakikisha unapewa urithi wako na wa mwanao kabla hujazaaaa just incase 😅😅😅
Sio rahisi kiasi hicho. Kwanini msiwaache hao waume za watu wawe free for good.
 
Wadada msizae na waume za watu hasa kiboya boya tu.(kama hajakuomba na kukuhakikishia mazingira unayoyataka)

Narudia tena.
Msizae na waume za watu.
 
Tatizo wadada wa siku hizi Akiona Kapata mwanaume kampangia nyumba Nzima anaona kashamaliza

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Mara nyingi hiyo huwa ni ya muda tu,
Baadae anatelekezwa huko,

Haya mambo nimeyachunguza,

Mungu huwa hatoi riziki za kufadhili dhambi za uchepukaji,

Mara nyingi mwanzoni mambo huonekan kwenda vizuri machoni kwao, lakini baadae mambo hugeuka, mara nyingi,

Uchumi huanza kuyumba na hivyo kutelekezana.

Mdada utabaki unataabika na mtoto, huku ukimpa lawama mwanaume kukutelekeza kumbe Naye

kapigwa pigo kwa dhambi zake za uzinzi, asijuwe la kufanya.
 
Mwanamke yeyote anayezaa na Mume wa mtu mwingine, hana akili kabisa.
Na Mwanaume anayezaa nje ya ndoa yake ni "mpumbavu" kabisa.
 
Michepuko inazingua sana na ilivyo jeuri kutwa kutamba una cheti nina bwana
 
Wadada msizae na waume za watu hasa kiboya boya tu.(kama hajakuomba na kukuhakikishia mazingira unayoyataka)

Narudia tena.
Msizae na waume za watu.
Ni wajinga !!Mtu anatembea na mume wa mtu akija jamaa anamtaka anasema eti "am taken".
 
Yaani mpka inafika hatua marehemu amefariki ndo unamuona mwanadada anajitokeza msibani akidai amezaa na marehemu wengine wanakuja na watoto msibani kutaka nao watoto kutambulika

Hivi siku zote Hawa wanawake wanakuwa wapi na nyinyi wanawake tabia za kuwaficha watoto baba zao mpka umauti unapata ndo mnajitokeza siku zote mnakuwa wapi ......

Nazungumza kwa sababu yametokea ndani ya ukoo wetu Kuna mwana Dada kajitokeza akidai Kazaa na ndugu yetu lakini upande wa pili mke na watoto wa ndoa umeleta Utata wamegoma kuwatambua huyu mdada yeye kwa Sasa anataka kwenda mahakamani kudai haki yake kwenye sehemu ya urithi upande wa ndugu wa marehemu hawajui wafanye nini maana marehemu hakuacha ujumbe kama alizaa njee

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Mwanamke hatakiwi kufanya kosa la kuzaa na mwanaume wa mtu huko nikukatili watoto ..ona sasa mtu akifa ndomnaanza kuangaika ..hii kitu nimbaya sana..sishauri kabisa
 
Back
Top Bottom