Wanawake waliofanikiwa sana kiuchumi na career zao, kuliko wote Tanzania pia wamezaa watoto wengi uzazi sio sababu ya mwanamke kufeli

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,881
6,305
Wanawake wengi wa kisasa waoga na wavivu sana kuzaa

Mwanamke umeolewa ila anampangia mume wake idadi ya watoto atakaozaa. Mtoto mmoja ama wawili tu

Wanasema watoto wanaharibu career zao.

Kwa uchunguzi wangu binafsi wanawake tatu bora waliofanikiwa kuliko wote tanzania ni hawa

Namba moja Samia suluhu aliefikia cheo cha juu kabisa Rais wa nchi

Namba mbili Getrude Lwakatare aliefanikiwa sana kibiashara kwenye shule zake za St marys na vyuo

Namba tatu Ruth Zaipuna aliefikia cheo cha CEO wa bank kubwa kuliko zote Tanzania.. NMB

Tukiwatizama hawa wanawake watatu wote wamezaa watoto wa kutosha . mama lwakatare kazaa watoto wa 5, mama samia kazaa wa 4, CEO wa NMB Ruth kazaa wa 4.

ila ndio wanawake waliofanikiwa kwenye career zao kuliko wote Tz.

Sasa hawa wanawake wanaosema uzazi wa watoto wengi unawakwamisha career zao wapo sahihi kweli ?
 
Dunia inaenda Kasi sana, siku hizi kuzaa watoto wanne ni watoto wengi?🤣 Wakati zamani ukizaa watoto wanne au watano ukaishia hapo mume analaumiwa Kwa kuoa mgumba, halafu mawifi wanamshauri aongeze mke mwingine WA kumzalia🤣🤣
 
Dunia inaenda Kasi sana, siku hizi kuzaa watoto wanne ni watoto wengi?🤣 Wakati zamani ukizaa watoto wanne au watano ukaishia hapo mume analaumiwa Kwa kuoa mgumba, halafu mawifi wanamshauri aongeze mke mwingine WA kumzalia🤣🤣

Wanawake wa siku hizi wenye uwezo wa kuzaa watoto wanne kwenye ndoa zao ni wachache sana.

Nikitazama mtaani kwangu majirani na ndugu jamaa na marafiki sioni ndoa ya zama hizi ambayo mke mwenye kazi ama career ya kueleweka amefikisha watoto wanne
 
Wanawake wa kizazi hiki wamezidi ulegelege.

Yaani wengine wamefikia hatua wakibeba ujauzito wanaenda kuomba kwa Daktari wazalishwe kwa Upasuaji kisa kuogopa uchungu..

Imagine Mwanamke wa hivyo ataweza kweli kufikisha hata watoto watatu (3) kwa kuzaa?
 
Back
Top Bottom