Wanawake chukueni hii point

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
WANAWAKE TAFADHALI KUMBUKA...✍🏾 Wanaume ujihusisha na wanawake kwa sababu mbili tu, LOVE, na SEX, lakini mara nyingi wanaume hawaoi kwa ajili ya Love au Sex, mara nyingi huoa kwa ajili ya UTULIVU (Stability).

Hebu nielezee.

Mwanaume anaweza kukupenda na kukuoa, vilevile Mwanaume anaweza kufanya mapenzi na wewe kwa miaka mingi bila kukuoa. Lakini mara moja tu anapopata mtu ambaye humleta utulivu katika maisha yake, aangalii mara mbili mbili, uoa mara moja.

Ninachomaanisha; Utulivu (Stability) ni "amani ya akili." Nimeona baadhi ya wavulana ambao walitoa kauli hii "Nampenda mwanamke huyu lakini sidhani kama ninaweza kukaa naye maisha yangu yote."

Wanaume ni watu wenye maono sana, wakati wanafikiria juu ya ndoa, wanafikiri kama huyu mwanamke anaweza kunijengea nyumba, anaweza kutunza watoto wangu na mimi, anaweza kunipa AMANI ya akili? Wanaume hawapendi wanawake wanaowapa usumbufu, ndio maana mwanaume anaweza kukaa na mwanamke miaka mingi na kukutana na mwingine ndani ya mwezi mmoja, kisha kumuoa.

Faraja ya kuwa na amani ya akili ndio kitu pekee wanataka. Ngono ni raha tu ya muda mfupi, mapenzi ni na mvuto tu, lakini kumbuka HESHIMA ndio ujenga UTULIVU (Stability). Wanaume wengi upenda Heshima, na heshima ni neno pana sana lenye kubeba vitu vingi.

Ndoa za zamani zilidumu sana kwa sababu wanawake walielewa nini maana ya kuwa na mume na Heshima juu ya waume zao. Ila siku hizi kinachofelisha ndoa nyingi ni Heshima
 
Dini ndio muongozo wetu vitabu vyote vinasema
MWANAUME AMPENDE MKE WAKE NA MWANAMKE AMTII MUME WAKE.
Ila watu siku hizi wamekuwa wajuaji sana ndio mambo mengi yanaenda hovyo hovyo
 
Dini ndio muongozo wetu vitabu vyote vinasema
MWANAUME AMPENDE MKE WAKE NA MWANAMKE AMTII MUME WAKE.
Ila watu siku hizi wamekuwa wajuaji sana ndio mambo mengi yanaenda hovyo hovyo
😀😀😀😀kupenda sio kazi yetu
Sio kwa kuwa maandiko yameagiza Mwanaume apende na mwanamke atii basi ndo mtumie hiyo kudhani kwamba mwanamke anapaswa kumchukia mwanaume.... Usisome maandiko kwa mihemko ya ushabiki wa simba na yanga bali jifunze kutafakari pia.

Basi vivyohivyo sio kwa kuwa mwanaume ameambiwa mwanamke ndie amtii yeye basi achukue nafasi hiyo kudharau yote ya mkewe.
 
Back
Top Bottom