Wanaume wanajichubua siku hizi, sura mweupe miguu na mikono mweusi

Kwani uhendisamu wetu watoto wa kiume umeanza miaka hii michache?!!!

Uzuri wa kiume na "kujichubua" ni vitu tofauti....
🤣Sawa we Baki na sura lako jeusi wanawake nao wanataka wanaume weupe Sasa we Baki ukiita mashoga wakati ndo wanakuibia mademu
 
Dunia sijui inaenda wapi? Watoto wakiume kama mabinti, haya mambo ya kupaka madude ya kukufanya uwe mweupe si muwaachie dada zenu, yaani imekuwa to much.

Utandawazi unaharibu zaidi kuliko kujenga, unakutana na mtoto wa kiume kajichubua na kupendeza kama mwanamke, mkifananishwa na wanawake mnakasirika.

Au kuna michezo mingine wanacheza, how come watoto wa kiume kuwa weupe wa hivyo na sio weupe asilia, yaani weupe wa kukutana nao?

Na mashuga mami ndio wanaharibu hivi vitoto vya kiume, yaani wao ndio wanawafanya wasitake kazi, wawe marioo. Ndio maana vinajichubua daily kwa kuwatega washuga mamy, msichana mzuri mdogo mdogo wa miaka 25-30 hawezi kutembea na kitoto kimejichubua hivyo.

Unakuta mtoto wa kiume chumbani kwake kuna lotion ya kila aina, sasa ni mtoto wa kiume huyo? Hatusemi wasiwe nadhifu lakini watoto wa sasa imekuwa to much, yaani wanakera

Ukikatiza K/Koo utakutana navyoo, yaani wamejikoboa sura na kuwa warembo. Baada ya miaka 20 tutapoteza hiki kizazi cha watoto wa kiume wa kweli, naona tunaishia ishia sasa.
Jali maisha yako.
 
Back
Top Bottom