Wanaume wakumbushwa kufuatilia afya zao kama wanavyofuatilia mpira

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

WANAUME WAKUMBUSHWA KUFUATILIA AFYA ZAO KAMA WANAVYOFUATILIA MPIRA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange amewakumbusha wananume kufuatilia afya zao na Afya za Watoto kama wanavyofuatilia mechi za mataifa ya Africa AFCON2023 yanayoendelea nchini Ivory Coast na Tanzania imeshuka dimbani kucheza mechi ya kwanza ya mashindano hayo dhidi ya Morocco iliyoshinda goli 3 kwa sufuri.

Mhe. Dkt. Dugange ameitoa kauli hiyo katika uwanja wa Mbagala Zakhem mkoani Dar Es Salaam wakati akizundua zoezi la uchunguzi wa Afya na Chanjo kwa wananchi wa mkoa huo zoezi lilillowakutanisha wananchi kutazama mechi hiyo kwenye Big Screen iliyofungwa katika uwanja huo kwa ajili ya hamasa kwa timu ya Taifa.

“Tunamwamko mkubwa katika kufuatilia michezo hususani AFCON2023 tunapenda sasa mwamko huo akinababa wenzangu kujali na kulinda afya kinga kwa Watoto maana akinamama wametuzidi mbali juu ya Afya ya Watoto wetu na kuzingatia Afya zao wenyewe” Dkt. Festo Dugange

Zoezi hilo linaloendelea katika viwanja hivyo na maeneo mengine nchini kwa kipindi chote cha mashindano ya AFCON 2023, limeratibiwa na @ortamisemi kwa kushirikiana na @uniceftz na mradi wa Break through Action.

GEEtpGEWcAA3jEx.jpg

GEEtpGEXAAAt87Q.jpg

GEEtpF8XYAABW1u.jpg

GEEtpGAWoAAOUwE.jpg
GEEtpGAWoAAOUwE.jpg
thumb_4623_800_420_0_0_auto.jpg
 
Akumbuke pia hata suala la kuwa shabiki wa mpira halianzi ghafla. Hivyo, hata kupima nako kunahitaji mda.
 
Kufuatilia mpira ni bure, kufuatilia afya inahitaji pesa.
 
Back
Top Bottom