Wanaume oeni yatima, hamtojutia

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Miaka mitatu iliyopita nilioa mwanamke kutoka familia ambayo alikuwa na wazazi wote, kwa kweli ndoa ilikuwa pasua kichwa, mwanamke akajaza vitimbi

Siku moja nikamwambia mjomba wangu kuhusu hali mbaya ya ndoa yangu, akanishauri achana na huyo mwanamke tafuta mwanamke ambaye ni yatima, ambaye maisha yake ya uyatima aliyaishi akiwa kati ya miaka 0 na 23, oa huyo utakuja kunishukuru sana.

Ni kweli kabisa nimetoa shukrani kwa mjomba kwa ushauri aliyonipa ni miaka 2 imepita sasa na hajawahi kuleta mgogoro na mjomba alioa yatima anaishi kwa amani sana na mimi nakushauri tafuta yatima oa, ndoa yako itakuwa salama sana.

Na wanawake wa hivi wananidhamu, upendo, huruma, na wanyenyekevu ila ukimuudhi ni rahisi kububujikwa na machozi na nzuri zaidi mme wake ndiyo humfanya kama baba yake mzazi ambaye alimuacha akiwa mdogo.
 
Miaka mitatu iliyopita nilioa mwanamke kutoka familia ambayo alikuwa na wazazi wote, kwa kweli ndoa ilikuwa pasua kichwa ...
Sio kila yatima anakua hivyo Mimi sitaki kusimulia, kwanza unazungumzia yatima yupi anaeishi na Mama yake au aliefiwa na wazazi wote Mama na Baba?

Maana yatima au binti anaeishi na Mama yake alafu Baba kafari au wanakwambia tu Baba hajulikani jaribu kufuatilia tabia za Mama usije ukaoa bomu la dakika,
 
Back
Top Bottom