Wanaulinzi na maendeleo ya nchi

mwalimu Jr.

Member
Aug 20, 2008
51
4
KAZI ZA Amiri Jeshi wa nchi ni kuhakikisha maslahi ya WOTE yanalindwa na hakuna wanaotumia nafasi au mali zao ili kuwanyonya, kuwanyanyasa au kuwadhulumu wengine.

Pili ni lazima ahakikishe maslahi ya NCHI na sio ya kichama au ya kikundi fulani ndiyo yanayotangulizwa mbele.
Tatu ni kuhakikisha kuwa amani inakuwepo ndani ya nchi na kati ya nchi hii na nchi jirani na za mbali.
Nne, Amiri Jeshi mkuu ndiye anayeweza kuwa mwasisi ya kufanya vyombo vya ulinzi katika nchi kuwa chachu ya maendeleo katika nchi kwa kushajihisha majeshi yawe ni taasisi muhimu katika masuala ya UFUNDI na TEKNOLOJIA na hasa kuzalisha mashine na mitambo muhimu inayohitajika kwa maendeleo ya nchi kama yetu.


JE, JESHI LINAWEZA wakati huu wa amani pamoja na kuendelea na kazi zake za ulinzi kuanza kushughulikia ULINZI WA AINA mpya sasa ambao pengine ni muhimu kuliko Ulinzi wa mipaka:

. Tuanze kujilinda huko huko kwenye matatizo na siyo mipaka yetu. Kupeleka majeshi Kongo ili kuwaondoa wahuni na nchi itawalike. Aidha Burundi, Somalia, Chad na Afrika ya Kati. Kote huku nchi za magharibi zinajihakikishia upatikanaji wa uranium kwa bei rahisi kutokana na kuendelwa kuwepo mitafaruku na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

. Ulinzi muhimu sana ni ule wa kujilinda na chakula kibovu toka nje. Je, jeshi letu linaweza kuwezeshwa kwanza kwa matrekta toka nje na kisha kupewa changamoto ya kutengeneza matrekta yetu wenyewe kama vile Nyumbu ilivyotengenezwa?

. Ulinzi muhimu pia ni kwa nchi kuwa na maji safi ya kutosha ili kuondokana na mabalaa ya kila aina ambayo yanaweza kuua asilimia kubwa ya watu wetu hata kuliko vita vya kawaida. Kwanini jeshi lisipewer ruhusa na kuwezeshwa ili kuhakikisha maji ya maziwa makubwa yanayotuzunguka yanainufaisha Tanzania sawasawa na yanavyowanufaisha watu wengine? Ninadhani jeshi watalielewa hili zaidi kuliko mvua za ndege zinazopiga mabomu mawingu.

. Kwanini jeshi wasiwe na vituo mbalimbali vya utafiti vitakavyoweza kuchangia Tanzania kuwa na vyanzo vinavyoaminika na kutabirika vya mali ghafi kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, viwanda vya msingi,

. Ulinzi sasa hivi haupo kabisa katika masuala ya TEKNOHAMA na tusishangae nyaraka za serikali na fedha kwenye mabenki yatakapoanzwa kuibwa na wataalamu wa nje na ndani tunaowajiri leo. Ni muhimu kwa jeshi letu pia kujikita kwenye eneo hili kwa kuwa na wasomi angalau wachache lakini ambao wamepevuka na kupitukia katika masuala ya TEKNOHAMA.

. Mpaka leo tumeshindwa kuwa na MELI za maana za kivita kwa ajili ya ULINZI wa bahari, maziwa na pengine mito yetu. Je, Jeshi limepewa changamoto gani katika hili. Au tutawaachia watu tu kutoka kilomita elfu kadhaa kuja kuvua kamba na samaki wengine kwenye maeneo yetu huku watu wetu wakiendelea kuwa masikini?

. Sanjari na hilo ni ule ukweli pia kuwa ULINZI mkubwa sana unahitajika katika kulinda madini yetu. Na hili haliwezekani ila kwa kuwa na wasomi wa jiolojia au sayansi ya madini na vilevile nchi kuwa na uwezo wa kuigilizia angalau mashine chache za msingi zinazohitajika katika uchimbaji madini. Kama vile jeshi lilivyoweza kutengeneza madaraja kwa siku kama sio masaa machache ni lazima jeshi letu tukufu liepewe changamoto inayolingana na saizi yake nayo ni kutengeneza mashine na mitambo ya kuchimba madini ili tuondokane na vibaka na wezi wa kimataifa.

. Nina hakika jeshi letu linaweza kutengeneza pia darubini na vifaa vingine vya kufuatilia matukio na majambo au kuziboresha zilizopo ili kulinda pia wanyama wetu kama rasilimali asili.

. Kwa kushirikiana na nchi kama Uchina, Korea, Brazili, Venezuela na kadhalika jeshi letu lina uwezo wa kuanza kutengeneza ndege ndogo na zile za kivita kama kanchi kadogo ka-Israel kilivyoweza. Tatizo ni kuwa tunajirudisha nyuma tu na kutaka kuendelea kuwa watu wa kufadhiliwa wakati ambapo wachimbaji madini wakitulipa fedha nzuri pakawa na ziada ya kutosha hivi vitu wallahi vile tunaweza kuvifanya sie. Sio tunakuwa na marubani wa kijeshi wanaoishia kufa kwa kunywa kupita kiasi eti tu kwa kukosa changamoto. Maana ukishajua kuendesha ndege hakuna jipya tena. Rubani huyo angelihitaji leo awe anatangeneza ndege mpya sio kukarabati iliyopo.


TAFAKARI: Wizi wa mawazo hauna tofauti na wizi au ufisadi wa aina nyingine. Angalau kiri mawazo haya si yako umeyapata toka kwa mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom