Wanasiasa wameshindwa na wamechoka kuiongoza Tanzania,ni zamu ya wengine sasa

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Taifa limepoteza uelekea,limekufa kiuchumi,kitamaduni na kisiasa pia , wanasiasa wanatawala kila sehemu bila ya kujali ni za kitaaluma na si za kisiasa.Siasa imeleta utumwa na kusababisha wizi wa rasilimali za taifa unaofanywa na wageni, siasa imefanya watanzania kuwa watumwa katika taifa lao,


Siasa inadidimiza kila sekta na kutaka yenyewe ndiyo iwe inaamua kila kitu, tumeiachia siasa itawale lakini inaendelea kuua watanzania. Ukosefu wa ajira na kunasababishwa na mipango mibaya ya wanasiasa.

kukosekana kwa huduma mbovu za afya zinasababishwa na wanasiasa kwani wao wataenda kutibiwa India na ulaya,Siasa imefika wakati wa kuchukua maisha ya wanasiasa kwa mauaji ya wao kwa wao kwa kutumia sumu na ujambazi. wakimaliza kuuana wao watakuja kumalizia na kuleta vita kwa wananchi wa kawaida.

Ni wakati wa kutafuta njia mbadala ya kuepuka matatizo yanayotaka kuletwa na siasa na wanasiasa katika taifa letu, na njia hii ya mabadiliko na kuwanyanganya wanasiasa Panga la kutukatia unayo wewe na sisi.


Nini kifanyike kuokoa Taifa kutoka kwa wanasiasa? nani wa Aliongoze Taifa tukiwanyang-anya wanasiasa?
 
Katiba inatambua wananchi ndi wenye nguvu na mamlaka .kama wameona wanasiasa wameshindwa njia ni moja kuwanyanganya madaraka na kuwapa watendaji
 
Back
Top Bottom