Wanasheria Naombeni Msaada Wenu

ashomile

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,625
2,443
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu ,
Kuna kampuni inalipa mshahara wa fixed 150k kwa siku 26 tu .
Wanakwambia masaa yanayozidi unapaswa kulipwa kama Overtime lakini chakushangaa na chakustaajabisha hiyo overtime nashindwa kuielewa.

Maana kuna kampuni nimewahi kufanya nalo kazi basic hours ilikuwa ni masaa (195) na malipo yake yalikuwa laki moja na elfu tano tu 105,000 kwa hayo masaa (195).

Baada yakutimiza hayo masaa (195) masaa mengine yote yalikuwa yanalipwa kama overtime na overtime yao kuipata ilikuwa unatafuta kwanza lisaa la kawaida hulipwa kwa shilingi ngapi ? Namna hii
Unachukua 105,000÷195 =538.46153846

Haya ukishapata lisaa la kawaida unalichukua hilo lisaa la kawaida then unalizidisha namna hii 538×3÷2= 807 hii ndo ilikuwa kama overtime yetu.

Lakini kampuni hili etii overtime yao iko katika lisaa la kawaida je nisahihi ? yaani unachukua hiyo 150,000÷26=5,769.2307692

Na hii 5769 hizo senti huwa wanazitoa kwahiyo kwa hiyo kama umewekewa mshahara hivyo visent hauvikuti .

Kama overtime yako ilikuwa ni siku 9 yaani unachukua 5769×9 =51,921 , lakini wao watakulipa 50,000/=

Kibaya zaidi anayehusika na uhasibu hajasomea na hajui madhara hakufanya hivi. Ni ile tu kapewa mamlaka alafu anaitumia bila kujua madhara yake.

Pia ukiingia siku ya sikukuu sawa na lisaa la kawaida wakati sikukuu najua huwa inalipaa double rate ya lisaa .

Kuna hicho kipengele nimekutana nacho wakati nataka kusaini mkataba ikanibidi nikichukue mara moja labda kiswahili chake mtakielewa kwa undani ili mnisaidie .

Hii Site ina overtime shida ya overtime zake hazina mashiko na hazieleweki .
IMG_20211102_224620.jpg
 
Kila kampuni ina utaratibu wake. Makubaliano yenu yalikuwa vipi kabla ya kuanza kazi?

Mshahara kiasi gani? Overtime kiasi gani?

Kama hayo yanajulikana na ulikubali na kuanza kazi hizi hesabu zingine nadhani ni muhimu kuongea na uongozi ofisini kwenu.

Ila huwezi linganisha mahesabu ya kampuni moja na nyingine ilihali taratibu zinatofautiana.

Fika kwa mhasibu ongea naye na kama haeleweki panda ngazi ya juu yake ongea nao.
 
Back
Top Bottom