Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Kuna baadhi ya watu/Taasisi hazipendezwi na kukosolewa au kuambiwa ukweli.
Naomba mniwie Radhi askari Polisi. Nilisha sema hapa hapa na naomba mniwie Radhi!!

Ha ha ha ha hii nchi hadi miaka 5 iishe labda size ya Magereza iongezwe!!
Ifike sasa viongozi, wakuu wa nchi na mamlaka wajitazame upya na waangalie wapi walipo kosea. Bila hivyo itafikia wakati wananchi watachoshwa na mambo ya matisho, na hii yaweza kua mbaya kuliko matarajio yao
 
badala ya kujiuliza kwa nini watu wanafurahi?wajirekebishe hao polis wanatutisha tena ...
 
Nimejaribu"ku-google"tusi linalofaa kukutukana nimelikosa,ila kwa ujumla unapaswa kupuuzwa zaidi ya upuuzi wenyewe.Acha kiburi cha kiitikadi,kuwaita watanzania wenzako "ng'ombe pori" ni jambo lisilovumilika na ni kielelezo cha dhahiri namna serikali hii ya mwendokasi ilivyofanikiwa kuwagrade raia wake katika matabaka mbalimbali.

Ni ujinga usiomithirika kuliona jeshi letu likitulazimisha tulipigie makofi hata pale tunapolishuhudia dhahiri likitumika kama "kipaza sauti" na mlinzi wa propaganda za serikali.

Jeshi lililozikimbia kambi zake na kuvamia bila kibali maeneo ya wazi na kuanza kuyatumia kama kambi za mafunzo na mazoezi kamwe haliwezi kuvumilika.Ni upumbav wa kiwango cha PhD kuendelea kuliamini jeshi hili lililoacha misingi ya kuanzishwa kwake na sasa limeamua kujisajili rasmi kama tawi la chama cha mapinduzi.

Inasikitisha pale serikali na Taasisi zake kudhani inaongoza misukule isiyoweza kufikiri,serikali haiwezi kupiga marufuku kila kitu alafu akadhani imeweza,kuwazuia watu kujadili mustakabali wao ni hatari zaidi kuliko kuwapa fursa ya kuongea na kutoa hisia zao za ndani.Wako wapi wenye hekima wawezao kuushauri utawala huu uliojiapiza kupambana na kila anaouhoji?

Kabla jeshi la policcm halijaanza kupambana na wale linaowaita wachochezi na wanaolibeza mitandaoni ni vema likajitafakari mwenendo wake kama ni wa haki na unastahili kuheshimika.Linapaswa kwanza kuzivunja kambi zote za mazoezi ya kivita zilizoko mitaani na barabarani na lirudi kambini likafanyie mazoezi yake ya ukakamavu huko.

Kitendo cha jeshi "kutoroka kambini" na kufanyia mazoezi yake barabarani kimeonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuweledi na kiintelijensia,kufanya mazoezi ya kijeshi barabarani huku yakiambatana na maonyesho ya silaha za kivita ni kuwapa fursa maadui kufahamu uimara na udhaifu wa jeshi lako.Huu ni upumbav wa karne na ni kielelezo cha mwisho kabisa cha utawala ulioingia madarakani kwa hila jinsi unavyojaribu kukikimbia kivuli cha hila zake kwa kuzuia kila fursa inayoweza kuhoji uhalali wa serikali yenyewe.

Sasa ninaanza kuamini kuwa PhD ya "malaika mkuu" ni PhD ya kipekee sana,aina hii ya utawala inayoruhusu askari kuandamana katika misururu mirefu barabarani wakiwa wameambatana na zana za kijeshi ni mfumo mpya wa utawala ambao haupatikani popote duniani isipokuwa nchi ya wadanganyika.Kiongozi aliyezuia mikutano na maandamano ya kisiasa kwa kigezo kuwa mikutano na maandamano hayo vitawanyima wananchi muda wa kufanya Kazi,je maandamano ya policcm katikati ya miji na majiji hayaathiri ufanyaji wa Kazi wa watanzania?

Ngoja niishie hapa ila natabiri vituko Na vioja zaidi huko tuendako.
Bro wherever you are big thank to you.

From now i'm ready to give you my daughter and make her your second wife if you wish.
 
Ifike sasa viongozi, wakuu wa nchi na mamlaka wajitazame upya na waangalie wapi walipo kosea. Bila hivyo itafikia wakati wananchi watachoshwa na mambo ya matisho, na hii yaweza kua mbaya kuliko matarajio yao
Mm nadhani Rais akubali kuwa hakuna raia asiye na mapungufu.
Pili, yy hana mamlaka ya kikatiba kuzuia siasa nchini ili hali yy akiambata na wana CCM wenzie wanaendelea kufanya siasa majukwaani na kujijenga kisiasa ambayo pia ni maandalizi ya uchaguzi wa Mwaka 2020. Na yy aweke pembeni Mambo ya CCM na asiandamane na akina NAPE, Ole Sendeka, Kinana, wala UVCCM,. yy abaki IKULU na Ole Sendeka amabaki Lumumba tu.

Ajue baadhi ya watu hapa Tz siasa ndio biashara zao. Mf ZZK, Kigoma nani asiye mjua? Eti huyu mwisho wake ni Kigoma tu!! Duuh!! Atachukueje nchi mwaka 2020 bila ya maandalizi leo? Kamwe mtu hawezi kukubali umunige ingali anakutazama-atang'ang'ana hadi kieleweke!!

Ni bora angezuia Maandamano ila mikutano hasa siku za Jmosi na Jpili iwe ruksa kwa kila mtu.
 
Kusema kweli lazima sote tusikitike pale jambo baya linapotokea, kitendo cha majambazi kutenda uhalifu huo ni cha kulaani kwa nguvu zote.
 
Uwoga waliopandikiza kwa raia pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa umewasaidia sana katika utawala huu wa kiimla, wasifikiri sasa wana uwezo wa kutoa agizo lolote na likafuatwa kama lilivyo hata kama ni la kakipuuzi...!! Yaani unaanzaje kunipangia namna ya kutoa hisia zangu? eti tunawabeza!!? Hivi ni uwaledi upi wanaojivuniaga hawa mapolisi wa tanzania?

Nilishasema na nitaendelea kusema....!! Jeshi la polisi la tanzania ni dhaifu sana na halina uwezo wa kupambana na real criminals

Mara kadhaa tumekuwa tukishuudia uvamizi wa mabenki na waarifu kutokamatwa huku wakifanikiwa kuondoka na fedha na polisi kuishia kukamata suspects tu.

Askari wanapigiwa simu muda ambao tukio la uharifu linafanyika anaanza kuuliza maswali ya kipuuzi... eti wako wangapi!?,wana siraha!?... alafu wanakuja dakika 20 baada ya waarifu kuondoka..bulishiit

Yaani watu wawili wanavamia kituo cha polisi wakiwa na mapanga tu alafu wanaondoka pale wakiwa na siraha nzito tena na magazine na huku wakiacha wameua askari wanne waliokuwa na hizo siraha kwenye kituo hicho.


Sasa kwa jishi la polisi la dizaini hii, si utakuwa ni uchizi nikisema eti na mimi nilisifie kutoka moyoni!!?

Mapolisi wa tanzania kikubwa wanachoweza ni kudeal na vibaka wadogo wadogo kama wezi wa simu, kupambana na raia wema wasiokuwa na siraha huku wenyewe wakiwa wamejizatiti kwa kila namna.....!! Na pia kingine kikubwa wanachooneka kuweza sasa ni kukimbizana na watu mitandaoni waliopo hapa nchini na hii inakuwa rahisi sababu wengi wa hao askari tunashinda nao humu. Majitu yanapenda rushwa kama hayapokei mishahara, yaani mpaka imeshakuwa kawaida bila kurefusha mkono hupati msaada...Nitalieshimuje jeshi la polisi kama hili!?


HAYA NI MAONI YANGU AU HISIA ZANGU....!!

HAKUNA BINADAMU ANAYEWEZA KUNIPANGIA NIWAZE VIPI JUU YA JAMBO FLANI.
 
Kwa siye watu wa martial arts kujipima uko fit you have to fight an opponent of same or higher rank. Sasa hawa polisi wanafanya mazoezi makali kwenye public kujiandaa kupiga watoto, wazee na vijana wasio na training wala siraha yoyote.. Hivi utapambana na jambaz kweli. Acheni siasa rudisheni imani kwa wananchi
 
Uwoga waliopandikiza kwa raia pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa umewasaidia sana katika utawala huu wa kiimla, wasifikiri sasa wana uwezo wa kutoa agizo lolote na likafuatwa kama lilivyo hata kama ni likakipuuzi...!! Yaani unaanzaje kunipangia namna ya kutoa hisia zangu? eti tunawabeza!!? Hivi ni uwaledi upi wanaojivuniaga hawa mapolisi wa tanzania?

Nilishasema na nitaendelea kusema....!! Jeshi la polisi la tanzania ni dhaifu sana na halina uwezo wa kupambana na real criminals

mara kadhaa tumekuwa tukishuudia uvamizi wa mabenki na waarifu kutokamatwa huku wakifanikiwa kuondoka na fedha na kuishia kukamata suspects tu.

Askari wanapigiwa simu muda ambao tukio la uharifu linafanyika anaanza kuuliza maswali ya kipuuzi eti wako wangapi,wana siraha alafu wanakuja dakika 20 baada ya waarifu kuondoka..

Yaani watu wawili wanavamia kituo cha polisi wakiwa na mapanga tu alafu wanaondoka pale wakiwa na siraha nzito tena na magazine na huku wakiua askari wanne waliokuwa na hizo siraha kwenye kituo hicho.


Sasa kwa jishi la polisi kama hili si ni utakuwa uchizi nikisema nilisifie kutoka moyoni!!?

Mapolisi wa tanzania kikubwa wanachoweza ni kudeal na vibaka wadogo wadogo kama wezi wa simu, kupambana na raia wema wasiokuwa na siraha huku wenyewe wakiwa wamejizatiti kwa kila namna.....!! Na kingine kikibwa wanachoweza ni kukimbizani na watu mitandaoni waliopo hapa nchini na hii ni kwa sababu wengi tunshinda nao humu.


HAYA NI MAONI YANGU AU HISIA ZANGU....!!

HAKUNA BINADAMU ANAWEZA KUMPANGIA MWENZAKE AWAZE NINI KUHUSU JAMBO FLANI.
Umesahau tabia mbaya ya kuwabambikia watu kesi za Uongo tena wakati mwingine kesi za mauaji na ujambazi , Jeshi la polis linahitaji mabadiliko makubwa sana ili liweze kuwa na weledi, busara na hekima plus ubinadamu .
 
Kwa siye watu wa martial arts kujipima uko fit you have to fight an opponent of same or higher rank. Sasa hawa polisi wanafanya mazoezi makali kwenye public kujiandaa kupiga watoto, wazee na vijana wasio na training wala siraha yoyote.. Hivi utapambana na jambaz kweli. Acheni siasa rudisheni imani kwa wananchi
Ni kweli kupigana ngumi na mtu ambaye hana mazoezi inashangaza sana.
 
Umesahau tabia mbaya ya kuwabambikia watu kesi za Uongo tena wakati mwingine kesi za mauaji na ujambazi , Jeshi la polis linahitaji mabadiliko makubwa sana ili liweze kuwa na weledi, busara na hekima plus ubinadamu .
Kwanza linanuka rushwa kwanzia juu mpaka chini kwa hawa wanuka jasho tunaoishi nao huku mlimani....!!

Wakubwa zao wanatumikishwa kisiasa na wanafanya maamuzi kwa kutafuta au kulinda vyeo na hawaangalii kama kuna usahihi kwenye maamuzi yao hata kama ni kwa kuvunja sheria... wao wanachoangalia ni kumfurahisha aliyewaweka pale.

Ni tanzania pekee tu askari anafuata chochote anachoamrishwa na boss.... nchi zingine kwanza askari lazima aijue sheria na ana uwezo wa kuhoji kabla ya kufanya kile anachoagizwa hasa pale anapoona sheria zinakinzana na agizo alilopewa.
 
Binadamu siyo ng'ombe wa kuswaga tu unavyotaka ana utashi wake na siku akichoka uhai kwake siyo issue, tuombe Mungu wasitufikishe huko maana ikifika huko hakuna atakaye salimika hata hao wanaotoa matamko ya kimungu mtu hawatakuwa salama na familia zao na ndg zao
 
Polisi wetu wanafanya kazi nzuri sana. Nawashangaa sana wale wanaolibeza

Kazi nzuri sana? Labda. Basi washauri pia wajiimarishe zaidi kupambana kikamilifu na majambazi. Polisi ni chombo kikuu cha udhibiti wa kinguvu (enforcement mechanism). Hatupati faraja kusikia kuna wababe zaidi yao kama tulivyoshuhudia mwaka huu - wakirudia kudhuru polisi zaidi ya mara moja. Tena wenye jeuri ya kuvamia na kuua polisi mara tu baada ya kutoka kututolea "show" la nguvu mitaani juu ya uwezo wao! HII HAIKUBALIKI. Nyenzo za intelijensia, upelelezi na udhibiti zitumike ipasavyo. La sivyo, hiyo sifa ya "kazi nzuri sana" itabakia kuwa porojo ya kisiasa huku polisi wakizidi kuangamia.
 
Hapo ndiyo Nchi ilipofikia, wasipojisahihisha sijui km hii chuki itaisha. Taifa linaelekea siko.

Eeeeeeh Mwenyezi Mungu tupe huruma, akili, hekima, busara na haki.
 
Hawa wanataka watu wasitoe mawazo yao au? Huwezi mlazimisha mtu awe na huzuni kwenye msiba wako, mimi ninawashauri wajitathimini waangalie wapi wamejikwaa kwani miaka ya nyuma watu hawakua hivi.
 
Back
Top Bottom