Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Padre > Father
Kuhani > Priest
Kwenye biblia hakuna neno Padre, na maana ya padre ni Father, kwenye biblia linamaana tofauti kabisa mfano sala ya wakatoliki ya Our Father,Who is in heaven..huwezi sema Padre wetu uliyembinguni....
Bado lugha inakushinda hii.. Unabisha ujinga tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Kipi kigumu zaidi, mtu kuja na kueleza dhambi zake kwa Padri kama Yesu alivyoagiza na kisha Padri mhusika kumwambia Mungu amemsamehe dhambi zake au Ellen White kujigeuza na kuwa Mungu wa kufahamu dhambi za watu na kutaka kuzitaja?

2. Yasome maandiko matakatifu sanjari na Historia.Shirika la Jesuits lilianzishwa kati ya mwaka 1545 na 1563 wakati suala la Kitubio linaonekana katika Kanisa la mwanzo kabisa kabla hata haijajulikana ni lini hao Jesuits walingalianzisha hilo shirika lao.(Rejea Society of Jesus - Wikipedia)
Wasabato ni weupe kabisa hawajui chochote si historia si dini.. Ila wakumbuke hatujasahau uongo wao wa kusema yesu anafanya hukumu ya upelelezi sasa sijui anampeleleza nani wakati yeye anajua tulipotoka na tunapoenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisa la sabato lililoanzishwa kwa misingi ya "kisangoma" (na hadi leo linaendelea na muelekeo huo huo),ndio la kweli?

Ombeni labda nisiwe hai na JF ifungwe. Nina orodha mambo ya mama yenu, Ellen White na wapiga ramli wenzie kama 1000 hivi, tena ya hovyo sana. Nitayachambua moja baada ya jingine tena kwa uweledi unaostahili. Ni lazima mfike mahali muelewe kwamba kupiga kwenu kelele haimaanishi kwamba watu hawakuwa na majibu ya ujinga na upotoshaji wenu.
Hebu anza kuwalipua hawa wapiga ramli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaah sasa mkuu tupo kwenye uhalali wa mapadri kusamehe watu dhambi! Wewe unakimbilia kwa wasabato! Hii maada inawahusu hao wasabato?
Mkuu kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa mijadala ya mleta mada ni kwamba tumeanza kuchambua wapinga Kristo...(Wasabato na Waislam)

Tumeanza na Waislam na Hekaya za Muhamad na uongo wake....mada zinapamba moto huko..

Tulimaliza tutakuja na Kundi la Wapinga Kristo yaani Wasabato(SDA)....Tutazieleza hekaya na uongo wa mama aliyejiita Ellen Gould White..

Ni wewe kuwa karibu na JF

Ahsanta
 
Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"

Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.

Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.

Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani

Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani

Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo

Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo

Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote

Well Said Kiongoz
 
Kapingane na Waraka wa Yakobo 5:14:

“14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.”

Neno “Wazee wa Kanisa” linamaanisha Kasisi.Biblia ya Kiswahili imejipatia neno “Wazee wa Kanisa” kutokana na neno la Kigriki (Lugha ya Agano Jipya) Presbyter lenye kumaanisha Kasisi au Baba au Padri.

Padri maana yake ni baba. Kumbe Yakobo anapowausia watu kuungama dhambi zao, anamaanisha wafanye hivyo mbele ya Mapadri ambao wao ndio wanapatiwa uwezo huo na Kristu.Kumbe, Kristu anauhisha mahusiano kati ya Mungu na mwanadamu kupitia kwa padri.

Huwezi kuwa umedandia maandiko matakatifu kwa mbele na ukafanikiwa kuyaelewa haya mambo.Basi, Imekula kwenu mazima.
Katubu kwa PADRE kwamba umedanya hapa jamii forums kwa kusema uongo! Kwa nini msamiati huu wa Padre msiuingize kwenye biblia wakati wa kufasiri
Bado lugha inakushinda hii.. Unabisha ujinga tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Heri yako wewe usiyemjinga,unayezijua lugha zote za ulimwengu! Japo unashindwa kutoa maana halisi ya Padre kibiblia!
Kwenye biblia kuna mitume ,manabii ,wainjilisti ,wachungaji na waalimu ambapo nyie hayo majina mnayapiga vita!
Mimi nilikua mkatoliki lakini sikuwa na amani na baadhi ya mafundisho yenu duni na dhaifu. Kwa sasa nina amani namtegemea YESU Kristo aliye Bwana na Mwokozi wangu, Siabudu dini wala itikadi za kidini.
Moja ya vitu amabavyo si kubaliani navyo ni:
1.Ibada za wafu et mt....flani utuombee?!
2.Kupewa kofi na askofu eti ndo paji la roho mtakatifu....lol!
3.Kusujudia sanamu au mtu, mfano kubusu na kuinamia pete za maaskofu...
4. Kuungama kwa binadamu eti unamwambia nimezini anakuuliza mara ngapi......duuu!
5.Mganga wa kienyeji kuwa katekista ....daaa!
6. Kufunga ndoa huku mtu ni mjamzito wa miezi kadhaa then anavaa shera/nguo nyeupe kama vile yuko bikra.
7.Kuhiji milimani na kubebeshwa misalaba na masanamu.
8.Kubariki misalaba makanisani inayoenda kupandwa kwenye makaburi ya wafu waliokufa siku nyingi...
9.Kukariri maombi na sala
10.Kuchanganya ushirikina na ukristo kwenu ruksa!
Hayo yote kibiblia ni machukuzo mbele za Mungu,achana na udini,itafute kweli nayo itakuweka huru!.Najua si rahisi kuukubali ukweli maana hata mimi nilikua mbishi na kutetea uongo lakini nashukuru Sana Mungu kwa neema sasa niko huru!
 
Walokole hawajui maandiko inashangaza mtu anakosoa neno kristu au kristo. Hili ni neno moja Tu yani kiebrania na kigiriki. Ni sawa walokole mnavyotamka mesiya na sisi wakatoliki masiha zt ni lugha Tu. Nawashauri sana walokole acheni kujiinua kujifanya nyie malaika wakti matendo yn tunayaona mtaani hamuishi vzr na jamii hata kdg. Mnapenda mungu mnamchukia kiumbe chake binadamu wakti yesu alisema mpende jirani yko km unavyojipenda mwenywe. Walokole ndgu zangu acheni kujikweza bila kanisa katoliki msingeipata biblia wengine mmesomeshwa na wakatoloki Leo mnalipiga mawe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu wakatoliki wanijuze kidogo ktk hali hii tunayoiona sasa ya papa kila anapoenda anashitakiwa mambo machafu yaliyofanywa na mapadri wa kanisa hilo na hasa kwa vijana wa kiume,wanapata wapi ujasiri wa kumweleza MTU mapungufu yao ilihali kuna uwazekano MTU Huyo ana makosa makubwa kuliko wewe unaetaka kusamehewa.Mifano mnayotoa ya wachungaji wa zamani inaweza ikawa sawa lakini hawa wa sasa kwenda kueleza mapungufu yako ni kujisanifu mwenyew tu, Yanayotokea ulaya na marekani hivi sasa ya vjana wa sasa na zamani badala ya kuungama dhambi zao wanaungama kudhalilishwa na mapadri in mambo yanayotokea hata afrika isipokuwa sisi tuna utii kwa viongozi wetu wa dini hadi tunatia kichefuchefu,mwishowe tun abaki kuwalaumu akina delicious nani sijui pasipo kujua huo ushoga walianza anzaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"

Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.

Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.

Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani

Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani

Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo

Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo

Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote
Hapo umenena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubatizo huondoa dhambi na maungamo huondoa dhambi.Kwani hujawahi kujibatiza mwenyewe kwa maana si unajua maji ndiyo yanaondoa dhambi na unafahamu fika yanapatika kwenye mito na maziwa au baharini?
Wenye maneno mengi Mara zote huwa ni waongo. Maji hayaondoi dhambi,kubatizwa kwenye maji ni ishara tu ya kuzikwa utu wa kale na kuzaliwa upya, tangu mwanzo dhambi ilisafishwa kwa damu ya mwana kondoo kupitia kuhani,baadae damu ya Yesu ikamwagika pale msalabani kwa ajili ya Mimi na wewe, hivyo Damu ya Yesu yatosha kwa ondoleo la dhambi na hakuna mbadala
 
Back
Top Bottom