Wanaopanda kutuhubiria na kutuombea katika Mabasi sisi na wao nani wana dhambi zaidi?

Ungekuwa unajua wala usingekuwa unasema ivo usilolijua ni kama usiku wa kiza ..
 
Hao wahubiri wakiwa wanafanya kazi hiyo ya Mungu kwetu hawamaanishi kwamba sisi tunadhambi coz mwenye kujua unadhambi n Mungu tu.
Back to the point
""" mkuu waheshim Sana hao watu hata Mimi nilikuwa Kama wewe ulivyo sasa lakini siku moja niliamua kuwasikiliza wakati nikiwa kwenye basi natokea Kampala kuelekea Nairobi. Wakati jamaa amemaliza kuhubiri akaanza kuomba na kukemea Kama ndani ya gari kuna watu wenye dhamira ovu washindwe katika jina la Mungu, basi akamaliza tukatoa sadaka. Sasa tumefika Nairobi ( maana tuliingia usiku ilibidi tulale kwenye gari). Baada ya muda naona askari Kama kumi hivi wameingia kwenye gari wakiwa na silaha Kali, wakakamatwa abiria wawili waliokuwa na bunduki( wenyeji wanasema huwa wansubiri tukifika maeneo ya porini wanaliteka gari).


Amini kwamba kwa maombi ya yule muhubiri kuwakemea kwa jina la Mungu walishindwa kufanya uhalifu ule wakajikuta wamelala mpaka wanakuja kukamatwa.

HITIMISHO
usimdharau yeyote anayekuja kutoa mahubiri mpe sikio lako kumsikiliza kwa umakini na ukiguswa toa sadaka.
Amen ubarikiwe mkuu mana njia iendeyo upotevuni ni pana na waendao huko ni wengi isishangae humu wengi wakapinga injili isiende Mbele
 
Nadhani huo Utahaira anao Mamaako.
Mamaangu, eti?

Unadhihirisha jinsi ulivyo Mkristo safi au jinsi ulivyo taahira? Hapa tunajadili mimi na wewe, mimi kwa mujibu wa maoni yako na wewe kwa mujibu wa maoni yangu, sasa mamaangu kajaje?

Sikiliza bwana mtukufu uliyetukuka, hajawahi mtu kupewa tuzo ya maneno machafu kwa kuwa si sifa njema.

Aliyehubiri na kuudhi watu anaweza kupata tuzo na si wewe unayetukana na kufurahisha watu.

Dhihirisha Ukristo wako au kaa kimya ufiche utaahira wako.
 
Mamaangu, eti?

Unadhihirisha jinsi ulivyo Mkristo safi au jinsi ulivyo taahira? Hapa tunajadili mimi na wewe, mimi kwa mujibu wa maoni yako na wewe kwa mujibu wa maoni yangu, sasa mamaangu kajaje?

Sikiliza bwana mtukufu uliyetukuka, hajawahi mtu kupewa tuzo ya maneno machafu kwa kuwa si sifa njema.

Aliyehubiri na kuudhi watu anaweza kupata tuzo na si wewe unayetukana na kufurahisha watu.

Dhihirisha Ukristo wako au kaa kimya ufiche utaahira wako.

Kamwambie Mamaako aanze kuuficha wa kwake kwanza kisha nami nitafikiria kuuficha wangu.
 
Nasikitikika ni kwanini huu Utamaduni wa Kijinga kama siyo wa Kipumbavu kabisa unaachwa na sasa umeshika kasi hapa nchini Tanzania kwani kiukweli unatuboa na kama Wahusika wasipoliangalia kwa umakini kuna dhahama inaweza kuja kutokea huko mbeleni.

Ni kweli Binadamu aliye kamili tunatakiwa kumjua Mwenyezi Mungu na hasa kupata mafundisho yake ili aweze kuishi kulingana na yale maandiko na hatimaye kuwa na Jamii njema na yenye Ustawi mzuri.

Lakini tabia hii ya Wahubiri tena hasa wa Kikristo ( ambapo nami pia ni Mkristo niliyetukuka kabisa ) ya kupanda katika kila basi la Mikoani na kuanza kutupigia Makelele kwa kutuhubiria huku wakizunguka basi zima kiukweli Kinakera mno.

Sasa cha ajabu zaidi siku hizi hawa Wahubiri hawapandi tu katika Mabasi ya Mikoani bali tunakumbana nao mno katika Madaladala tena Basi likiwa limejaa kabisa lakini bado tu huyo Mhubiri anang'ang'ana kupishana na Abiria ili azunguke basi zima kutuhubiria na kutuombea tuliomo mule.

Hivi nyie Wahubiri mnaotusumbua kwa mahubiri yenu ndani ya Mabasi ya Mikoani na katika Madaladala nani kawaambieni kuwa sisi hatuombi na hamtumjui Mwenyezi Mungu? Nani aliyewaambieni kuwa kila aliye ndani ya Basi la Mikoani na Daladala ni Mkristo? Hivi nyie Wahubiri kwani mkitafuta tu Uwanja wenu maalum muendeleze hayo Mahubiri yenu kwani hamuwezi kuwapata Watu hadi mje kutusumbua, kutupigia makelela na kutupandisha tu hasira ndani ya Mabasi ya Mikoani na Madaladala?

Mheshimiwa Kamanda Mpinga tafadhali sana lifanyie hili Kazi haraka sana kwani yawezekana Watu wengi wanakereka na hili ila wamekosa tu platform ya kuliongelea ila Mimi kwakuwa nina platform hii na nikiamini kuwa hata Wewe pia ni Member mzuri tu wa JF pamoja na Watendaji wako ni matumaini yangu makubwa kuwa utalitafutia ufumbuzi wa haraka kwani nisikufiche Kamanda LINATUKERA MNO ABIRIA na wengine mikono yetu huwa ni myepesi mno kutoa hukumu au kupiga Vichwa kama vya Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe pindi tupatapo Hasira au Kukereka.

Nimalizie tu kwa kusema nilichokigundua hapa ni kwamba yawezekana hawa Wahubiri wanaopanda kutwa katika Mabasi ya Mikoani na Madaladala kutuhubiria kisha kutuombea wakidhani sisi Abiria ndiyo wenye dhambi nyingi basi pengine wao Wahubiri ndiyo wanatakiwa kujihubiria na kujiombea sana wenyewe kwani wanasababisha dhambi kuwa ya KUTUKERA sisi ABIRIA kitu ambacho kinatupelekea KUCHUKIA hivyo kumkosea Mwenyezi Mungu.

Sipingi NENO la Mungu bali kilio changu hapa ni utaratibu tu mbovu na wa ki hovyo hovyo unatumika kulifikisha hilo neno la Mungu kwa Walengwa ambao kwa kiasi kikubwa sana huwa WANAKEREKA na KUBOREKA nalo.

Binafsi nimewachoka na naomba kuwasilisha.

Jambo hilo si sawa, ni usumbufu usio wa lazma kwa abiria, halafu haiwezekani mtu hujulikani wewe ni nani wala bila ruhusa ya hao wenye gari uanze kutoa mahubiri. Ukiona mtu anafanya hivyo ujue pamoja na nia njema aliyo nayo ila ujue wazi mtu huyo amekosa hekima, maana je ikatokea mtu wa dini nyingine akasimama na kuanza naye kuhubiri juu ya Imani yake huyo mwinjilisti atakakubali kusikiliza na kuheshimu? Halafu mbona kuna maeneo mengi ambayo yanaeleweka kuwa neno la Mungu ni haba? vituoni kumejaa wahuni, mateja n.k kwanini hawataki kwenda sehemu hizo kuokoa vijana wanaoangamia?
 
Ki ukweli hata mbuyu ulianza kama mchicha, hii tabia inatakiwa kukomeshwa
Uko mbeleni hii tabia inaweza kusababisha shida pindi watakapokutana watoa mahubiri wa dini tofauti, au kuna bahadhi ya mabasi yanaweza kubaguliwa na abiria.
mfano:
mfano tu lakini! kwenye mtei kuwe na mahubiri ya kikristo na kwenye saibaba kuwe mahubiri ya kiislam, alafu gari zote zinaenda Babati hapo fikiria wewe mwisho wake inakuwaje?

Tuwache haya mambo kwenye nyumba za ibada, kwani kwenye vyombo vya usafiri tunapanda watu wenye dini tofauti na wasio na dini, na hata kama unayo dini labda muda huu huna mpango wa kuhubiriwa neno.

Nafikiri wenye vyombo vya usafiri, pamoja kikosi cha usalama hili linawahusu.
 
Wanaosomea uchungaji wanakosa kazi hivyo wanaamua wajiajiri taratibu na mwishoni wakishapata pesa huwa wanaanzisha makanisa yao kabsa. Hivyo ni wa kuvumilia tu, na wenyewe wanatafuta riziki
 
Kamwambie Mamaako aanze kuuficha wa kwake kwanza kisha nami nitafikiria kuuficha wangu.
Roho ya Mpinga Kristo iko ndani yako. Umekuja na mada sasa unaifunika na povu kushupalia mama wa mwenzako.

Mungu awarehemu wazazi wako, wameyapata mengi duniani juu yako, sio vyema nikakufuru sbb roho iliyoko ndani yako, sio kosa lako la 100%. Shetani ana nguvu zaidi yetu, bila Yesu unayemkataa, hiyo roho itakusumbua daima.
 
Roho ya Mpinga Kristo iko ndani yako. Umekuja na mada sasa unaifunika na povu kushupalia mama wa mwenzako.

Mungu awarehemu wazazi wako, wameyapata mengi duniani juu yako, sio vyema nikakufuru sbb roho iliyoko ndani yako, sio kosa lako la 100%. Shetani ana nguvu zaidi yetu, bila Yesu unayemkataa, hiyo roho itakusumbua daima.

Utakapomaliza ' kuharisha ' kimaandishi hivi niambie tafadhali kwani naona bado hayajakata.
 
Mosi nimefurahi mno na sana kujua kuwa kumbe na Wewe ni Mfuatiliaji wangu mzuri sana hum JF na nakusihi sana usiache kunifuatilia kwani naamini pia kuna siku unaweza pia ukanitamkia kuwa UNANIPENDA na unataka niwe MUME wako.

Pili kuna tofauti kubwa sana ya Kimantiki kati ya Kulalamika na Kuelezea Kero fulani fulani tena Kiuchambuzi zaidi na nadhani pengine kutokana kwamba huna AKILI hivyo nikifanya humu chambuzi zangu ambazo Wewe huziwezi na huzielewi ndipo unajawa na Jicho la CHUKI na WIVU juu yangu na kunishutumu kuwa najifanya ni Genius.

Tatu kusema kuwa sitakiwi kila mara kutokwa na mapovu ama kukemea au kulizungumzia jambo fulani muhimu na lenye maslahi Kijamii na badala yake niwe tu ninapotezea ndiyo umenipa picha ya jinsi gani ulivyo Mpumbavu na sishangai hata unavyochukizwa na ' Ujiniasi ' wangu uliotukuka na kubarikiwa na Mwenyezi Mungu. Hivi leo hii kwa mfano Vyama vya Upinzani visingekuwa vinaibua ' uozo ' uliopo Serikalini na hadi katika sekta zake zingine na hadi zile za Binafsi nchi leo ingekuwa ina afadhali hivi? Katika Jamii yoyote panahitajika kuwa na Watu ambao wana macho ya ziada ambayo ni myepesi kuibua madhaifu ili Wahusika wayafanyie Kazi na ndiyo maana unaona hata Muanzilishi wa JF aliona mbali na akaona kuwa Watanzania wengi hawana platform ya kufunguka juu ya yale wanayoyaona na ambayo mengine ni Nyeti kabisa hivyo akaja na kitu kama hiki ambacho kimesaidia kuwa dependable Whistle Blowing site na JF kupitia Members wake mbalimbali imeweza kusaidia maeneo mengi sasa Utendaji kuwa wa Kiumakini hasa baada ya Watu kuja na kulalamika humu. Yawezekana Wewe ni Member wa JF lakini umuhimu wako humu huujui zaidi tu ya kila mara kujitokeza kumpinga na kumchukia GENTAMYCINE ambaye pengine hata robo tu ya IQ hujamfikia.

Mwisho GENTAMYCINE siyo tu kwamba ni Genius bali ni ' TALENTED AND CHARISMATIC ' na najivunia mambo mengi sana humu JF kwani yapo mambo mengi niliyowahi kuyaibua humu humu JF na yakafanyiwa Kazi, Impact yangu sehemu mbalimbali ni kubwa mno, Threads zangu za JF huwa zinatapakaa hadi katika Mitandao mingine ( nje ya JF ) na Wahusika huko hunifanyia Acknowledgement kitu ambacho ninawashukuru sana lakini kama haitoshi GENTAMYCINE leo ameweza kufanya hadi Watu wa Taasisi fulani fulani tena muhimu kabisa hapa nchini kuwaweka Watu wao MAALUM kabisa waweze kuangalia kila siku GENTAMYCINE ana post au anaanzisha nini JF kisha wanakifanyia Kazi ( Kwa lugha nyepesi tu Mimi ni both Reliable and Credible source kwa Taasisi nyingi kitu ambacho kinanipa mno moyo na jeuri pia ).

Yapo mengi ila nimeanza na haya machache kwanza lakini na Mimi pia nitafurahi sana kama na Wewe ukiniambia umuhimu wako humu JF ni upi tangia ulipokuwa Member na umeweza kuleta impact gani katika Jamii yako au Taifa letu kwa uwepo wako tu humu.

Naomba ' dozi ' hii ikuingie vizuri sana na kama una chochote kingine tena unachotaka kutoka Kwangu karibu sana na usisite kuniuliza ' Genius ' Mimi.

Na naomba ujumbe huu uwafikie hadi hao wote waliokupa 'Likes ' hapo kwa upuuzi wako ulioupost kwani ni imani yangu kubwa sana kuwa unafanana nao hata kwa kuwa na IQ fupi kama zao.
Kuna watu wa ajabu sana humu, GENTAMYCINE ameongea ukweli wa kero ambayo imekuwa haifurahishi watu wengi, kero lazma izungumzwe halafu mitizamo ibaki. haiwezekani tusipaze sauti kwa kile cha kusema ''potezea tu'' hapana!!!!
 
Kuna watu wa ajabu sana humu, GENTAMYCINE ameongea ukweli wa kero ambayo imekuwa haifurahishi watu wengi, kero lazma izungumzwe halafu mitizamo ibaki. haiwezekani tusipaze sauti kwa kile cha kusema ''potezea tu'' hapana!!!!

Mkuu humu ndani napambana na Wapumbavu kadhaa waliotukuka kabisa halafu nikiwadharau wanakasirika. Huwezi amini kwa ' upuuzi ' huo alioundika huyo Binadamu Mwanaharamu kapata ' Likes ' nyingi tu za Wafuasi wenzake wasiojua kufikiri. Yaani nimemdharau kunakotukuka huyo Members nikimjumuisha na hao ' Wafuasi ' wake wote wanaoonekana hapo kumpa ' likes ' kwa fujo.
 
Mwisho wa siku watu wataanzisha makanisa katika mabasi ya abiria,
mie napenda kuwaza nawaza tu
mfano tabia hii ikijengeka, alafu kukawa na uchaguzi watu fulani wakaja kufanya kampeni kwenye mabasi,
mtawazuia au,?
jibu litakuwa "humu sio kwenye majukwaa ya kisiasa?" na je kwenye mabasi ni majukwaa ya dini au mihadhara?
kumbukeni hata jangwani/bonde la mkwajuni wanaoambiwa wahame sasa, alianza mtu mmoja kujenga.
 
Back
Top Bottom