Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,648
- 698,191
Nadhani kuna laana kwenye hizi teuzi za kisiasa kwa wateuliwa wengi.. Nasema ni laana kwakuwa wanakuwa kama wamerukwa na akili kutokana na matendo, matamshi na maamuzi yao hasa wanapokuwa mbele ya makamera ya waandishi wa habari:
. Huchanganyikiwa.
. Utu huwatoka.
. Hujisahau walikotoka, na kushindwa kutafakari yajayo.
. Hukosa adabu na heshima.
. Huwa na ukatili wa ajabu n.k
Akili zao huwabadilika hata kama ni wasomi kwa maana ya kufaulu mitihani na kupata vyeti. Wakishapigwa chini akili huwarudi na kuanza kuwa wanyenyekevu na watu wa kujuta mno.
Msikilize Kigwangala anavyojutia kuwacharaza viboko askari wa wanyamapori mbele ya kadamnasi. Watu wazima na familia zao kuwadhalilisha namna ile. Leo hayupo pale alipokuwa kuna mzimu wenye kumtia hofu mno unamuandama na anajutia matendo yake yale.
Msikilize Gambo anavyolalama! Anahisi kuonewa, anahisi kuchukiwa, anahisi kufanyiwa vitendo viovu! Huyu ndio Gambo RC mwenye nguvu nyakati zake wa kuitwa ofisi ya DC akajieleze.. Ni Gumbo huyu leo hii wa kubebewa condom na lotion nyumbani kwake ili vitumikeje?
Makonda mla bata namba moja duniani kijana mjivuni katili aliyejawa dharau leo anaishi kama digidigi, hana misafara tena! Hana wasaidizi hana walinzi, hana uwezo tena wa kumpigia simu rais na kuweka loud speaker.. Ama kweli maisha hayana formula.
Sabaya.. Kukamatwa kwake watu walifanya sherehe wiki nzima wakila na kunywa! Huyu ndio yule alikuwa anaingia popote na kufanya lolote na asifanywe kitu na yeyote yule... Sasa hivi ni hata rufaa zake zinawekewa mapingamizi na aliokuwa nao pamoja.
Hawa ni mifano michache kama key figures! Lakini list ni ndefu sana.. Kuna wale wasaliti na waliounga juhudi, kuna kina Dr. Mihogo, bro wangu Kakurwa nknk.. Leo hii wanaishi kwa wasiwasi kutojiamini na majuto makubwa
Waliopo kwenye chart kwasasa kuna baadhi wamegutuka! Kwamba kuna kesho, baadhi wanarudia makosa yale yale ya wenzao! Kauli na matendo yao bi kama vile watabaki hapo walipo milele. OLE WAO!
Hawa ni masikio ya kufa hayasikii dawa ama wameyatia nta wasisikie. Baadhi watamaliza mwaka nasisi mtaani! Tutawakaribisha bila kinyongo! Baadhi mwakani. Wengine kabla ya 2025 na wengine baada ya hapo! Tuwaombee wote.
Kuna yule DC kamchapa binti kofi la uso! Kuna huyu diwani kawacharaza vikongwe bakora! Watu ambao ni sawa ama zaidi ya wazazi wake! Laana inayomjia atakuja kuweweseka mitandaoni!