Wanaofanya Biashara ya Manukato (Perfumes) za Kupima...

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,989
Naamini humu sitokosa mtu anaefanya hii biashara kama si mfanya hii biashara ila ana idea na elimu au taarifa kuhusu hii biashara.

Ni moja ya biashara ambayo nimechagua kuifanya kwa ukubwa sana huu mwaka Ndani ya biashara yangu Flani hivi.

Naombeni muongozo wa namna naweza ianzisha sijui bajeti kabisa kwahyo hapa nyie ndio mtaniambia bajeti yangu ianzie ngapi hadi ngapi.

Msione uvivu kufunguka Pesa kwani sitoianza kwa udogo nitaianza kwa ukubwa kwahiyo Fungukeni kadri moyo unavyoweza kufunguka kuhusu hii biashara. Hii ni kwa Perfume za Kupima TU.

1.Mtaji kiasi gani?
2.Zinapatikana wapi?
3.Bei zake zikoje?
4.Vifaa vyake zile mashine za kufungia vifuniko.
5.Chupa za kupimia za style tofaut zinapatikana wapi?
6.Faida yake ipo vipi?
7.Na mengine mengi ambayo sijaweza yaandika hapa nitaomba Mnisaidie ndugu zangu.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom