Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Kuna baadhi ya watu wanao ibeza CDM kwa uamuzi wake wa juzi, wa kususia hatua za mwisho za mjadala wa kufanyia marekebisho kanuni inayotoa ufafanuzi wa ni nini maana ya kambi rasmi ya upinzani. Kwangu mimi kitendo hicho cha CDM ni ushahidi mwingine unao dhihilisha namna chama hicho kilivyokomaa kisiasa; maana kama kingeliendelea kukaa ndani ya bunge mpaka suala hilo likafikia hatma yake, kusingelikuwapo uhalali wowote wa chama hicho kuendelea kulipinga suala hilo, kwa vile nacho kingelihesabiwa kuwa sehemu ya uamuzi huo. Maadam wakati uamuzi huo unachukuliwa chenyewe hakikuwepo kina kila sababu ya kuendelea kupinga hatua hiyo.