Wananchi wanalia, Rais analia

SOKON 1

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,134
331
Baada ya siku 100 na ushee madarakani, Kikwete amesalimu amri, analalama ni kweli maisha magumu na haonyeshi ufumbuzi wa kuyatatua isipokuwa kuegemeza utetezi kwa waliomtangulia.
Wananchi wanalalamika kwa kuongezeka gharama za maisha.

My take;
Ajabu nani atayatatua?
Wananchi wanahitaji mwelekeo mpya wenye matumaini mapya. CCM wameshindwa je tufanyaje?

Nawasilisha
 
Ni wakati umefika sasa JK akili kuwa kuna group la viongozi walioteuliwa na Mungu yaani (Philosopher King) na kuna watu wa kuongozwa yaani (Populace). Sasa inapofikia mtu anayetakiwa kuongozwa anakuwa kiongozi mambo haya lazima yatokee. Yaani nchi inageuzwa kuwa kichwa cha mwenda wazimu. Ni wakati umefika wananchi wajitabue wenyewe na wachukue maamuzi wenyewe ili kuliokoa taifa kutoka katika mikono hafifu ya muuongozwa anayeongoza.
 
...JK alidhani Urais wa Nchi ni sawa na kula wali kwa kachumbali kwenye sahani ya fedha! Urais ni kazi-dume; inahitaji wanaume wa shoka wenye mboni za kuona mbele zaidi ya wanavyoona wananchi wa kawaida. Urais si chetezo na ubani pekee kilichojazwa uvumba, manemane, ambari, mvuje na kashkash baruani...ni kazi ya kuonyesha njia yenye saada kiuchumi, kijamii na kisiasa.

JK amefeli tena amefeli mtihani uliyotungwa na Dr. Ndalichako (Mkurugenzi wa NECTA); kwa mshangao, mtihani uliyotungwa na Dr. Slaa (Operesheni Sangara) na Prof. Lipumba (Operesheni Zinduka) atatoka kweli? Sidhani! Mwacheni alie...kama walivyoimba MSONDO NGOMA, "ukimuona mtu-mzima analia ujue ana jambo". Amefilisika kisiasa, hana jipya...tusubiri maumivu makali ya msoto wa maisha ya kubangaiza kiuchumi, kisiasa na kijamii.
 
Bravo Mr!Huwa napenda sana kusoma makala zako.Huwa unaongea ukweli mtupu bila kutafuna maneno.Hongera kwa hilo
 
Tz ina miaka sita,haijawai kuwa na rais,Mkwere alikuwana nia ya kuchuma pesa za watz tu,sio siri tutamkumbuka
 
Back
Top Bottom