Wananchi wanakula mizizi Kisarawe

Juzi nimeenda Wilaya ya kisarawe nikashangazwa kuona dhiki ilkiyokubuhu kule. Lakini lililonitisha ni kuambiwa kuwa wananchi wako maeneo ya kibuta wana dhiki kiasi cha kuwa hawana hata chakula wameishia kula mizizi

Hivi kweli miaka 50 baada ya uhuru imekuwaje wilaya ile inaonekana kama vile bado wako enzi za mkoloni mjerumani?

Hivi jimbo la kisarawe lina mbunge kweli?

wabunge waliopita ni:

KIGOMA ALI MALIMA (marehem)

MZEE JANGUO (alikuwa mkurugenzi THA)


Jamani kuna siri gani ambayo inafanya viongozi wa serikali na chama na NGO's kulikimbia hili jimbo la kisarawe?

Nashauri Rais atangaze hali ya dharura ili ijulikane imekuwaje wananchi ambao ni watanzania wanakula mizizi wakati kuna programu za maendeleo, wna wanatengewa fedha za maendeleo na wanakatwa kodi za kila namna

Hayo ndio "maendeleo" yaliyoletwa na magamba bwana! Ndio "maisha bora kwa kila Mtanzania" yaliyoletwa "Kwa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya". Na Kisarawe (kama ilivyo kwa sehemu zingine zenye umaskini mbaya kabisa) ni ngome ya ccm.
 
Back
Top Bottom