Wananchi Hai waunganisha nguvu zao na kutengeneza Barabara ya kambi ya nyuki na Lerai na kupunguza kero kubwa inayowakabili

davimsu

Member
Mar 28, 2019
13
4
Katika Kile Kinachoonekana Kuwa ni Kuchoshwa na Ubovu wa Barabara Zinazounganisha Maeneo Mbalimbali ya Mtaa wa Kambi ya Nyuki iliyopo katika mamlaka ya mji mdogo wa bomang’ombe Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ,Madereva wa Wameamua Kuunganisha Nguvu Zao na Kujaza Kifusi Barabara ya kambi ya nyuki na Lerai na Kupunguza Kero Kubwa inayowakabili

Wakizungumza na waandishi wa habari walifika katika eneo hilo uku zoezi la kufukia mashimo kwenye barabara hiyo likiendelea madereva hao walisema kuwa magari yao yamekuwa yakiharibika kutokana na ubovu wa barabara hiyo

Jonh Masawe mmoja wa madereva hao ,alisema wameamua kujitolea kujaza vifusi katika barabara hiyo ili waweze kufanya shughuli zao bila usumbufu wowote

Aleni Mollel, Elisant Swai, wa wakazi wa maeneo hayo Anasema Uamuzi wa Kuweka Kifusi Kwenye Barabara Hiyo,Unatokana na Kutopitika kipindi cha mvua za masika hivyo kusababisha gharama za usafiri kuongezeka hasa kwa wagongwa na wajawazito

Mollel alisema Barabara km 5 hii ni muhimu ni kiunganishi kati inasafirisha mchanga kwa ajili ya ujenzi katika maeneo mengi ya Wilaya hii na nje ya Wilaya hii hivyo ni muhimu kukarabatiwa kwa kufukia mashimo yaliyopo katika barabara hii

Unakuta kipindi cha kawaida kusafiri kwenda Bomang’mbe ni sh,2000 lakini kipindi cha mvua gharama zinapanda hadi sh,7000 kwa pikipiki kutokana na barabara kuwa mbovu’’alisema Mollel

Nao Baadhi ya Madereva wa malori ya machanga Wamewaomba Madereva Wengine Kujitokeza kushiriki Zoezi Hilo,Lililolenga Kuboresha Sekta ya Usafiri wa Umma na Kuifanya Yenye Uhakika Zaidi katika eneo hilo

Kwa uapande wake mwenyekiti wa Mtaa huo Marko Dioli ,alisema zoezi hilo litakuwa ni endelevu kwa kujaza kifusi cha katika maeneo yote ambayo hayapitiki kwa pikipiki na malorin ili kupunguza gharama za usafiri kipindi chote ikiwamo cha mvua

Kwa upande wake Afisa Tarafa Masama Nsajigwa Ndagile,aliwasifu madereva hao kwa kutoa magari yao kwa ajili ya kubeba kifusi kwa ajili ya kufukia mashimo hayo na pia amewaongeza wananchi wa mtaa huo kujitolea kuzambaza vifusi hivyo





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora ya hao wana akili ya kujiongeza, huko pwani watu wanajua kucheza mdundiko tu
 
Back
Top Bottom