Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuondoka Congo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Baraza la usalama la umoja wa mataifa, linatarajiwa kutuma ujumbe katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo siku ya jumamosi, kujadili muda mwafaka wa kuondolewa kwa wanajeshi elfu ishirini wa kimataifa nchini humo.
Hiki ndio kikosi kikubwa zaidi cha wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani.
Rais wa nchi hiyo,Joseph Kabila, amesema anataka wanajeshi wote hao kuodnoka ifikapo katikati ya mwaka ujao.
Ingawa katibu mkuu wa umoja wa mataifa , Ban Ki Moon amependendekea waondoke kwa awamu katika kipindi cha miaka mitatu, ikiwa ni sehemu ya mpango wake kurejesha amani katika nchi hiyo ambapo raia wangali wanashambuliwa na makundi ya waasi.
Baraza la usalama lina hadi mwishoni mwa mwezi ujao kufanya uamuzi ni lini jukumu lake la kulinda amani litatizamwa upya.



http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2010/04/100414_un_congo.shtml
 
Back
Top Bottom