Wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kufanya mtihani mwingine

Hayo ndo madhara ya kuweka wanasiasa katika kusimamia Elimu yetu, serikali itatoa wapi pesa za kuridia mitihani?? Serikali inatumia vibaya pesa za walipa kodi,

Wanatengeneza ufisadi hapo hamna lolote yaana nachukia sana hawa viongozi Wa Elimu.

Kuna watoto walifauru ila wazazi wao wakaamua kuwapeleka shule binafsi je na hao watarudi kufanya mitihani??

Na wale walioko masomoni nnje ya nchi je? Yaani hii nchi imeoza!!!

Nani atafidia garama za wazazi kama Mtoto atafeli jamanii???
 
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema kuwa
wanafunzi ambao walichaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza katika shule za serikali nchini wanahitajika
kufanya mtihani wa udahili tarehe 28 mwezi huu na
wale watakaofaulu wataruhusiwa kujiunga na kidato
hicho.
Taarifa hii ilitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu
Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt.
Charles Msonde lakini kwa mujibu wa barua kutoka
NECTA iliyosainiwa na Edgar Kasuga kwa niaba ya
Katibu Mkuu kwenda kwa Makatibu Tawala wote wa
Tanzania Bara siku ya Jumatatu, wale ambao
hawatafaulu hawataruhusiwa kuendelea na masomo
hayo ya sekondari.
NECTA inakusudia kutumia mtihani huo kuhakiki
uwezo wa wanafunzi waliounesha katika kiwango chao
cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu
ya Msingi uliofanyika mwaka jana. “Watakaofeli
hawataruhusiwa kuendelea na masomo,” inasomeka
sehemu ya barua hiyo. Makatibu Tawala wote, maafisa
elimu na walimu wakuu wote wa shule za sekondari za
serikali waliombwa kufikia leo wawe wamewasilisha
orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na shule zao ili maandalizi yafanyike.
Afisa mmoja wa NECTA amesema maandalizi kwa ajili
ya mtihani huo yanaendelea na kwamba wanafunzi
wajiandae. “Maandalizi yanaendelea vizuri na tutatoa
taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko yoyote
yatakayojitokeza,” alisema.
Katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi
uliofanyika mwaka jana, watoto 789,479 waliofanya
mtihani huo ambapo wanafunzi 555,291 walifaulu. Idadi
hii ya waliofaulu ni sawa na asilimia 70 ya wanafunzi
wote waliofanya mtihani huo.
Elimu bure inatugharimu
 
Kuna kitu hakiko sawa NECTA kama wanafikiri mtihani wa taifa wa darasa la saba una mapungufu warekebishe kuliko kufanya mitihani 2 ni gharama zisizo na msingi.

Vinginevyo kuwe na chombo kingine kitakachosimamia mtihani huu wa pili kuliko NECTA kusimamia mitihani yote miwili kwa candidates wale wale. Kwa maoni yangu ni uamuzi ambao unahitaji mjadala wa kitaifa kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Stay blessed!
 
Kwa hiyo mtihani wa Taifa hauaminiki tena?
Gharama zote zilizotumika katika kufanya ule Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba leo wanasema warudie? Bado sijamuelewa Ndalichako. Ina maana:
-Aidha wasahihishaji wa ule mtihani hawaaminiki?
-Watungaji wa ule mtihani hawana sifa?
-Vigezo vya ufaulu havina ukweli?
-Mtihani ulivuja?
-...,...
 
Hapa sipati mantiki yake, ni kama vile baraza haliwaamini waliosimamia mitihani ya drs la saba au wasahishaji. Mi nadhani, wangeongeza tu ufanisi ktk usimamizi wa mitihani.
Ufanisi utapatikanaje wakati msimamizi kazi ya wiki nzima analipwa laki moja tu? Kwanini mwenyeji akiongeza laki nyngne nisimpe mzigo? Haya, shule INA walimu wanne toka darasa la kwanza had Ia saba. Uchawi gani utatumika kukamilisha masomo hapo? Mwalimu mkuu wa shule isiyofaulisha atawajibishwa na kudhalilishwa, nani atakubali kudhalilishwa? Pana mengi ya kutatua,lakini yamefumbiwa macho. Matokeo yake ni kupeleka vihiyo sekondari.
 
mikurupuko bado tu inaendelea! sijui wamejipanga kurudisha na gharama za wazazi tulizo zitoa kama za nauli,sare madaftari, sijui huwa wanafanyiwa vigezo gani kuwekwa kwenye baraza hilo
mlishafanya makosa tokea huko kwenye mtihani wa taifa basi kausheni mjipange kwa hawa watakao maliza mwaka huu
hayo ni matumizi mabaya ya kodi zetu na pia ni kuaribu mipango tuliyoiweka
 
mikurupuko bado tu inaendelea! sijui wamejipanga kurudisha na gharama za wazazi tulizo zitoa kama za nauli,sare madaftari, sijui huwa wanafanyiwa vigezo gani kuwekwa kwenye baraza hilo
Watumishi wa umma wamekosa ubunifu kabisa zaidi ya kufanya kazi kwa mihemuko.
 
Kama mtihani wa necta hauaminiki ni bora wakarudia wote(pamoja na wale walofeli) kwasabab hauez kusema wamefel wakat mtihan waliuofanya siyo wenyew
 
Watumishi wa umma wamekosa ubunifu kabisa zaidi ya kufanya kazi kwa mihemuko.
kazi kweli kweli kwa vichwa kama hivyo kusimamia suala la elimu ni hatari sana naona tunazidi kujichimbia shimo kwenye suala la elimu
kila siku matamko tu
 
National Exam maana yke ni nn?au ni pre- National in otherway paper yenywe ndio hyo tarehe 28....kaz ipo kwa mpango huu
 
Hii na sawa na screening ambayo serikali haitaki shule za private zifanye.
 
Back
Top Bottom