Wanafunzi waacha shule na kwenda kufanya kazi za ndani kutokana na michango kuwa mingi mashuleni

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shule za Serikali za Kata wameshindwa kuendelea na masomo na kuacha shule kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni utitiri wa michango mashuleni.

Moja ya shule kati ya nyingi zilizopo Jijini Arusha ni Sekondari ya Lemara iliyopo katika Kata ya Lemara kwenye Halmashauri ya Jiji la Arusha ambazo wanafunzi wameacha masomo Na kukimbilia miji mingine kama Dar es Salaam kwenda kufanya kazi za ndani na baadhi ya vijana kukimbilia kwenye machimbo ya Madini na kwenye vibarua vya ujenzi.

Michango inayodaiwa katika shule hizo ni pamoja na pesa ya Taaluma (20,000) kwa kila mwanafunzi,
Pesa ya chakula (15,000) kila mwezi Rim paper mbili kwa mwaka kila. Muhula rim paper moja.
Hela ya Ulinzi.

Hela ya Remidial classes kiasi cha shilingi (500) kila siku jioni na ni lazima kwa kila mwanafunzi baada ya masomo kusoma Masomo ya jioni.

Pesa ya mtihani kila jumamosi kiasi cha shilingi (1000) na (1500) nk.

Kutokana na utitiri wa michango na uwezo Mdogo wa wazazi wengi hushindwa Kumudu gharama hizo.

Huko wilayani Babati katika Mkoa wa Manyara baadhi ya Shule za Kata zimekuwa zikiwaweka wazazi ndani kwa kile kinachodaiwa kushindwa kulipia watoto wao michango mashuleni.

Baadhi ya shule zinazotuhumiwa Kuwaweka ndani wazazi ni shule ya sekondari Burunge na shule ya sekondari kaiti iliyopo katika Kata ya Kaiti.

UFAFANUZI AFISA ELIMU BABATI DC
Akizungumzia taarifa hizo, Afisa Elimu Sekondari wa Babati DC, Alice Mwallo amesema "Nimezungumza na wahusika katika shule hizo maelezo ni kuwa mchango ambao unatolewa ni wa chakula, tunahakikisha Wanafunzi wote wanapata chakula ili kuwa na afya bora kwa ajili ya uelewa wao.

"Kama ni masuala ya hatua inawezekana hatua zinachukuliwa katika Ofisi za Kata, hizo ni Sheria ndogondogo ambazo zinatengenezwa ngazi ya Kata.

"Utaratibu huo sio kwa shule hizo tu bali shule zote za kutwa, kwa kuwa wanafunzi wanasoma hadi saa kumi na moja na wengine hadi saa kumi na mbili."

UFAFANUZI AFISA ELIMU ARUSHA JIJI
Jitihada zinaendelea kumtafuta
 
Halafu utasikia kuna ngedere pori moja iliyoshiba pesa za ruzuku inakuja kufungua domo lake kuwa elimu bure. Kipindi hicho watoto wake wanasoma Feza.

Hapo hapo kuna mipumbavu mingine ambayo dada zao wanaosha vyombo majumbani mwa watu kwa kushindwa kuendelea na masomo inakuja kusifia humu kuwa mama anaupiga mwingi.

CCM ni LAANA kubwa mno katika hili taifa.
 
Halafu utasikia kuna ngedere pori moja iliyoshiba pesa za ruzuku inakuja kufungua domo lake kuwa elimu bure. Kipindi hicho watoto wao wanasoma Feza.
Hapo hapo kuna mipumbavu mingine ambayo dada zao wanaosha vyombo majumbani mwa watu kwa kushindwa kuendelea na masomo inakuja kusifia humu kuwa mama anaupiga mwingi.

CCM ni LAANA kubwa mno katika hili taifa.
Kuna mtu mmoja humu, kaanzishaga uzi, watu wakiweka maoni akiwajibu mwishoni anajibu mama anaupiga mwingi, nilitamani kumuliza maana yake Nini? Ila sijazoea mabishana au kumpinga mtu kwenye maoni yake.
 
Hata usithubutu kuuliza ndugu yangu maana hakuna kitu kilicho hatari duniani kama mtu mpumbavu na imani yake. Mpumbavu akiamini lake hata umwambie nini hawezi kubadilika na cha zaidi huwa wanaishia kutukana.
 
Hela ya Chakula ibaki Kama ilivyo. Wafute hizo tuition sijui remedial, pia rimu iwe moja tu kwa mwaka na watoe hela badala ya rimu ili mzazi alipe Mara mbili kwa mwaka (,nusu nusu), Mambo yatasonga tu.
 
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shule za serikali za kata wameshindwa kuendelea na masomo na kuacha shule kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni utitiri wa michango mashuleni,.

Moja ya shule kati ya nyingi zilizopo jijini Arusha ni sekondari ya Lemara iliyopo katika Kata ya Lemara kwenye halmashauri ya jiji la Arusha ambazo wanafunzi wameacha masomo Na kukimbilia miji mingine kama Dar es Salaam kwenda kufanya kazi za ndani na baadhi ya vijana kukimbilia kwenye machimbo ya Madini na kwenye vibarua vya ujenzi.

Michango inayodaiwa katika shule hizo ni pamoja na pesa ya Taaluma (20,000) kwa kila mwanafunzi,
Pesa ya chakula (15,000)kila mwezi
Rim paper mbili kwa mwaka kila. Muhula rim paper moja.
Hela ya Ulinzi.

Hela ya Remidial classes kiasi cha shilingi (500)kila siku jioni na ni lazima kwa kila mwanafunzi baada ya masomo kusoma Masomo ya jioni.
Pesa ya mtihani kila jumamosi. Nk

Kutokana na utitiri wa michango na uwezo Mdogo wa wazazi wengi hushindwa Kumudu gharama hizo.

Huko wilayani Babati katika mkoa wa Manyara baadhi ya shule za kata zimekuwa zikiwaweka wazazi ndani kwa kile kinachodaiwa kushindwa kulipia watoto wao michango mashuleni.
Baadhi ya shule zinazotuhumiwa Kuwaweka ndani wazazi ni shule ya sekondari Burunge na shule ya sekondari kaiti iliyopo katika Kata ya kaiti.
Kwani wazazi hawajakubaliana kwenye kikao?
 
... hapo ni Lemara CBD ya Jiji la Arusha, the Geneva of Africa. Kule Nakapanya au kijiji cha Mpigamiti - Lindi hali ikoje?
 
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shule za serikali za kata wameshindwa kuendelea na masomo na kuacha shule kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni utitiri wa michango mashuleni,.

Moja ya shule kati ya nyingi zilizopo jijini Arusha ni sekondari ya Lemara iliyopo katika Kata ya Lemara kwenye halmashauri ya jiji la Arusha ambazo wanafunzi wameacha masomo Na kukimbilia miji mingine kama Dar es Salaam kwenda kufanya kazi za ndani na baadhi ya vijana kukimbilia kwenye machimbo ya Madini na kwenye vibarua vya ujenzi.

Michango inayodaiwa katika shule hizo ni pamoja na pesa ya Taaluma (20,000) kwa kila mwanafunzi,
Pesa ya chakula (15,000)kila mwezi
Rim paper mbili kwa mwaka kila. Muhula rim paper moja.
Hela ya Ulinzi.

Hela ya Remidial classes kiasi cha shilingi (500)kila siku jioni na ni lazima kwa kila mwanafunzi baada ya masomo kusoma Masomo ya jioni.
Pesa ya mtihani kila jumamosi kiasi cha shilingi( 1000)na (1500) nk.

Kutokana na utitiri wa michango na uwezo Mdogo wa wazazi wengi hushindwa Kumudu gharama hizo.

Huko wilayani Babati katika mkoa wa Manyara baadhi ya shule za kata zimekuwa zikiwaweka wazazi ndani kwa kile kinachodaiwa kushindwa kulipia watoto wao michango mashuleni.
Baadhi ya shule zinazotuhumiwa Kuwaweka ndani wazazi ni shule ya sekondari Burunge na shule ya sekondari kaiti iliyopo katika Kata ya kaiti.

Michango jumla ni kama 40,000 tshs bado nauli kwa mwezi.

Unakuta familia ina watoto wanne. Kama laki mbili kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom