Wanafunzi wa kike wakutwa wakivuta bangi na viroba, walimu wapeleka kwenye mitandao

we unadhani ni kwanini mwl aliamua kusema tunaweka kwenye mitandao?

huoni kama ni sababu ya direct attack ya serikali kwa waalimu baada ya tukio la mbeya!!

Binadamu ni asili yetu kusawazisha mambo !!! let it happen mkuu!!
That's even worse.

Ualimu una miiko yake. Kwenye nchi zenye kuelewa faragha ya mtoto ni nini unaweza kushtakiwa kwa kutoa picha kama hizi. Hao watoto ni underage, hawajafikisha age of majority, wanatakiwa kupewa adhabu katika framework ya shule, si kuwadhalilisha mitandaoni.

Kama walimu wana matatizo na serikali waandamane, wa deal na serikali, si kuwafanya wanafunzi kama pawns katika matatizo yao na serikali.
 
Tukienda kwa style hii,watakaoumia zaidi ni Wanafunzi
Maana wengi ndio majanga.
Maana kuna moja wanakata mauno,kuna moja hapo Dar wanalana Denda
Hahaha,aisee wanafunzi sasa wanaingia pabaya zaidi
 
Kuweka picha hizi za watoto kwenye mitandao ni udhalilishaji wa faragha yao.

Ukisikia mwalimu anahimiza ataweka picha hizi kwenye mitandao ndio unajua kwamba matatizo yetu ni makubwa sana, hata walimu hawana elimu.
MUNGU ATUSAIDIE.... SISI WENYEWE HATUTAWEZA. BIFU HILI SASA HALITAISHA.
 
Naanza kuona mtifuano wa serikali na walimu...bila shaka hapa polisi watawashughulikia wavutaji na wanywaji hao(wanafunzi)kisha hao walimu Mungu wangu sijui kifuatacho...
 
Hakuna wito hapo kila mtu atimize wajibu wake ipasavyo.

tusiwanyanyase waalimu eti kwa sababu ya wito whats the hell,mwanao alete upumbavu eti kisa wito achekewe tu hakuna kitu kama hcho
Hakuna mtu aliesema asiadhibiwe...elewa hilo kwanza.
Kuna adhabu maalum kwa ajili ya wanafunzi..
The point was kulikuwa kuna haja gani ya hao walimu kuwarecord na kusema ngoja tuwarushie mitandaoni..huoni huo ni ukosefu wa hekima??.what if wanafunzi nao wangeruhusiwa kumiliki sim shuleni..jiongeze ni mangap maovu ya waalim dhidi ya wanafunz yangefichuka..
 
Kuweka picha hizi za watoto kwenye mitandao ni udhalilishaji wa faragha yao.

Ukisikia mwalimu anahimiza ataweka picha hizi kwenye mitandao ndio unajua kwamba matatizo yetu ni makubwa sana, hata walimu hawana elimu.
Hii ni kujihami kwa walimu maana huenda hao wanafunzi tena wa kike wangechana sketi zao na kupiga kelele kusema mwalimu alitaka kuwabaka..

Mwalimu kujihami akasema nitarusha kwenye mitandao....
 
Tukio la walimu kufukuzwa chuo kwa kuonewa na mihemko isiyo na maana kwa viongozi wetu hakika tumejenga kitu kibaya sana mbeleni kwa wanafunzi.....Sasa kutakuwa hakuna mipaka ya mwalimu na mwanafunzi.. Nani anatakiwa kumheshishu mwingine..

Natabiri majambazi na wavuta bangi watatoka mashuleni maana ni kama Serikali imehalalisha. .
Kweli mkuu!!
Kitakachofuata ni pale mwanafunzi anapokosea,mwalim hatomrekebisha bali atachukua smartphone yake anamrekodi video anatupia mtandaoni,habari imeishia hapo.
Kuna msemo nakumbuka mwalimu wangu wa primary alikuwa anautumia "uelewe au usielewe,mimi ikifika mwisho wa mwezi navuta changu,wewe utajijua mwenyewe"
 
Haya sasa tuone tamko la Mwigulu nchemba na Ndalichako
Kosa la hao wanafunzi haliwezi kuwafikisha polisi,
Kwa sababu
Kwanza wako chini ya 18 wangekuwa 18+ walitakiwa washitakiwe kwa kutumia madawa ya kulevya kinyume cha sheria

Pili utovu wa nidhamu wa mwanafunzi hauwezi kuwa kesi ya kufika kwa waziri wa elimu.

Kwa hiyo hapo iko hivi;
Walimu wapeleke taarifa kwa mkuu,
Mkuu amwite mzazi,
Wajadiliane, wakielewana na mtoto akaomba kusamehewa aendelee na shule, hata kama ni kwa mashart sawa

Akija kurudia afukuzwe shule,
Hizo ndizo tunazoweza kuita busara juu ya jambo kama hilo;
Wala hatupaswi kulilinganisha na lile la Mbeya,
lile la mbeya ni shambulio la kudhuru mwili, kwa upande wa sheria maana wale walimu ni18+ na nikukosa maadili ya kazi kwa upande wa wizara.
 
That's even worse.

Ualimu una miiko yake. Kwenye nchi zenye kuelewa faragha ya mtoto ni nini unaweza kushtakiwa kwa kutoa picha kama hizi. Hao watoto ni underage, hawajafikisha age of majority, wanatakiwa kupewa adhabu katika framework ya shule, si kuwadhalilisha mitandaoni.

Kama walimu wana matatizo na serikali waandamane, wa deal na serikali, si kuwafanya wanafunzi kama pawns katika matatizo yao na serikali.
Walim hao ni kweli wamekosea.. Ila ni ujumbe kwa Wanasiasa..waache maamuzi ya kukurupuka/mizuka.
 
nani awaadhibu tushanyimwa kila m moja ataadhibu mwanae nyumbani kwake
Hivi nyinyi ndio walimu? Mbona mna akili fupi hivi?!! Kilichopingwa ni ule ukatili wa wale vijana wanne kumpiga mtoto mmoja kama mwizi.
 
Wadau kunavideo inasambaa huko Instagram ikionesha wanafunzi secondar wamekamatwa wakinywa viroba na kuvuta bang kibaya zaid ni watoto wakike
Hii inapaswa kuangaliwa kwa makini maana iletulio ionambeya inaweza kuwa ndio tabia za wanafunzi wengi zinaanzia hapa ndio maana hawana nidhamu darasani



waacheni watoto wavute bangi,hamtakiwi kuwagusa; mnatakiwa mtumie saikologia mliofundishwa chuoni kuwafundisha watoto kuacha bangi..nyie walimu vipi?
 
sidhani kitendo hicho ni cha maadili ya ualimu, Ndelichako atawpiga chini hao walimu muda si mrefu ngoja aione hiyo clip

Daah...Mi nashangaa enzi hizo mpaka uingizwe ofisini maana yake umeshindikana na ukisikia mwenzenu kaingizwa ofisini mnajua anaenda kuchakaa....

Kipindi hicho ukiingizwa ofisini ile unaambiwa lala chini, wakati unaelekea kulala chini tayari mzigo wa fimbo umekuishia mwili wote...Yani mpaka ufike chini umeshachakazwa....

Huyo dogo mvuta bangi kaguswa na tubao viwili tuu imekuwa nongwa ...

Acha kabisa niko fom 2 kuna jamaa alipigwa hadi akatenguliwa kiuno, dunia imebadilika eti mwanafunzi anakunjana na mwalimu, enzi hizo sisi viongoz wa shule walikuwa wananyoosha ukijichanganya.
 
kwani ukivuta bangi ni kuchapwa ? bangi ni crime kwa hiyo sharia ichukue mkondo wake
Bangi ni madawa ya kulevya; Nafikiri Kukutwa na Bangi ni kosa la jinai. Tunategemea Polisi wachukue hatua dhidi ya watumiaji wa madawa ya kulevya.
Huenda sheria ya under age itawalinda hao wanafunzi;hata hivyo kuna magereza ya watoto watukutu sijajua huwa wanakuwa na makosa yapi au hufungwa kwa sheria ipi.
 
Nani anaweza mfukuza mwanafunzi? Mimi nakuunga mkono kwenye kuachana nao,hata kuwahoji na kuulizauliza nikupoteza muda tu hao walimu wangefanya mambo ya manufaa zaidi ya hayo.
Shule/kamati ya nidhamu, whatever it is.
 
Back
Top Bottom