Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 228
- 551
Kama kuna jambo linatishia uhai wa Taifa basi ni swala la vijana hasa wa kike kuchukulia swala la ngono jambo la kawaida sana
Zamani mvulana kugusa mwili wa msichana (hata mkono tu) ilikuwa mvulana anaweza kuota mwezi mzima na atawasimulia washikaji zake kijiweni. Hiyo ilikuwa kugusana tu na mtoto wa kike kwasababu walikuwa na staha na adabu na waliheshimu miili yao
Mambo yamebadilika sana siku hizi! Watoto wadogo hasa wanafunzi wa sekondari na vyuo kwao swala sio kuguswa tena, ngono kwao imekuwa kama jambo la kawaida sana! Yaani sio swala la aibu wala kujitafakari, wanaona fahari kutembea na wanaume
Watoto wa kike kuanzia miaka 16+ kutembea na wanaume wenye miaka 30+ sio aibu kwao ni fahari
Wasichana wadogo miaka 20+ kutembea na wanaume miaka 40+ kwao sio aibu tena ni jambo la kawaida sana
Ukiangalia umri huo ni wa uanafunzi bado.
Walimu mashuleni kazi wanayo hasa kwa hawa watoto wa uswahilini maana wamekua wakiona dada zao, shangazi zao, mama zao wadogo wakifanya hivyo. Hawana wa kuwashauri kitu kinachofanya walimu nao waonekane wanatwanga maji kwenye kinu wanapokemea maswala hayo
Nimeshuhudia mtoto wa kidato cha kwanza (miaka 13) amejenga mahusiano "sugu" na jamaa ana familia yake (mke na watoto wawili) kiasi cha kupata ujasiri wa kutoroka kwao kila ifikapo usiku wa manane kwenda kwa jamaa huyo na anavizia alfajiri ndio anarudi kwao. Binti haoni hata aibu anakiri kabisa kuwa anampenda!!
Ukiona shule ya sheria pale mawasiliano wanafaulu wanafunzi 17 kati ya maelufu sio swala la kuwalaumu watunga mitihani, tuangalie chanzo
Ukiona wanafunzi wa udaktari Muhimbili wanagomea baadhi ya mitihani tutafute chanzo sio kulaumu utaratibu
Watoto siku hizi hawasomi, "standardization" inayofanywa na NECTA huku madarasa ya chini kwa malengo ya kisiasa inaharibu sana elimu yetu
Zamani kuvuka kidato cha pili kwenda cha tatu ilikuwa "avarage" ya alama 30, yaani mwanafunzi afaulu masomo saba si chini ya alama 30. Lakini siku hizi akifaulu masomo mawili tu kwa alama 30 anavuka (yaani D mbili) na bado wanafeli wengi sana tu
Mmomonyoko wa maadili kwenye Taifa letu unaua vipaji vya watoto na sasa kipaji kinachoibukia kwa kasi kubwa sana ni kipaji cha Ngono! Hiki watoto wanajua kukitumikia vizuri sana
Kumbi za starehe na hizi night clubs siku hizi kuwakuta watoto wadogo wa kike kwa wa kiume ni kawaida sana kana kwamba hakuna serikali wala sheria zinazoongoza maeneo hayo
Mtoto wa sekondari anakesha club akichezewa chezewa maungo yake na kulewa kila aina ya kilevi halafu utegemee aheshimu Wazazi na Walimu na kuelewa darasani?