Wanafunzi na uchaguzi

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
31,275
31,404
Nionavyo ni kuwa wanafunzi wengi wamejiandikisha kupiga kura katika vituo vilivyo karibu na vyuoni kwao. Kitendo cha kufungua vyuo vya elimu ya juu baada ya uchaguzi hakutawanyima wanafunzi haki ya kupiga kura..........??? Nahisi kama vile kuna mpango fulani wa kumkosesha Dr. Slaa kura za wanafunzi.......
 
Wanafunzi hasa wa elimu ya juu hawaiungi mkono CCM ndio maana kwa kugundua hilo wamefunga vyuo ili wasipige kura. ila wanaweza kumpigia debe jemedari wao Dr. Slaa huko aliko na kuelezea vema uozo wa CCM kisha kumzolea Dr. Slaa kura za kutosha
 
Serikali imepagawa tu, wanadhani kuwa wanafunzi watarudia ule mgomo wa 2000 - ambao ulishirikisha wanafunzi wa vyuo vyingi vya elimu ya juu (sio mlimani pekee). Sidhani kama kwa sasa vyuo vina watu kama kina Mkili (RIP), Zitto, yule mkurya wa kibiti, Mkangara, yule dada VP wa mlimani sijui alikuwa anaitwa nani ...nk
 
Wanafunzi hasa wa elimu ya juu hawaiungi mkono CCM ndio maana kwa kugundua hilo wamefunga vyuo ili wasipige kura. ila wanaweza kumpigia debe jemedari wao Dr. Slaa huko aliko na kuelezea vema uozo wa CCM kisha kumzolea Dr. Slaa kura za kutosha
Sidhani kama kumpigia debe bila kupiga kura kutasaidia. Kwa upande wangu naona cha kufanya ni kuishinikiza selikari kuwarudisha vyuoni ili watimize haki yao ya kupiga kura
 
Nionavyo ni kuwa wanafunzi wengi wamejiandikisha kupiga kura katika vituo vilivyo karibu na vyuoni kwao. Kitendo cha kufungua vyuo vya elimu ya juu baada ya uchaguzi hakutawanyima wanafunzi haki ya kupiga kura..........??? Nahisi kama vile kuna mpango fulani wa kumkosesha Dr. Slaa kura za wanafunzi.......

Wanafunzi wenye uchungu na nchi yetu na ambao ni wazalendo halisi watasafiri tu kwenda kwenye vituo vyao vya kupigia kura.
 
serikali iache uhuni, ila watavuna wanachokipanda naamini wanafunzi watainfluence jamaa zao wote kupigia kamanda slaa
 
Burundi walikataa kupiga kura Jumapili kwa sababu watu wengi wanakuwa makanisano. Vyuo vikuu anzeni mkakati vyuo viwe wazi muwae kupiga kura
 
Nadhani hata ningekuwa serikalini nami ningefanya hivyo. We unadhani nani haopgopi kupoteza madaraka...
 
.....kimsingi CCM imefanya kitu mbaya sana vyuoni hivi sasa.....wanafunzi wamekuwa waoga sana.....wakujipendekeza kwa chama kwa sana! naamini kwa dhati kabisa kama wataamua kwa umoja wao ama kuishinikiza serikali vyuo vifunguliwe kabla ya siku ya uchaguzi au kishinikiza tume ya uchaguzi kwa mamlaka iliyonayo itafute modality itakayowaruhusu wanafunzi wa vyuo wapige japo kura ya urais, basi umma tutakuwa nyuma yao. Jamii imechoka kusikia wanafunzi wakigoma kwa kudai posho ila wakiinua sauti yao kwa jambo kama hili, hakika tutawaunga mkono!
 
Huuu hauna tofauti na ubakaji.. Na kunyima watu uhuru wao...

Ila tukiamua tunaweza.. Wakt ni sasa wa kuamua.. Piga kura Tar 31.10.2010
 
Back
Top Bottom