Wanafunzi 90 Wapata Mimba Katika Shule Moja Marekani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Wasichana 90 wa shule moja ya sekondari nchini Marekani walipata mimba ndani ya mwaka mmoja na kuonyesha wazi jinsi tatizo la mimba za wanafunzi linavyozidi kuiumiza kichwa Marekani.
Idadi ya mimba za wasichana wenye umri chini miaka 18 katika shule za Marekani imeongezeka kwa kasi na kufikia asilimia 26 na kupelekea kuwepo kwa mjadala wa kuitilia mkazo elimu ya ngono mashuleni.

Katika shule moja ya sekondari katika kitongoji cha Frayser, North Memphis, Tennessee, kulikuwa na jumla ya wasichana 90 waliopata mimba katika mwaka wa masomo uliopita.

Maafisa wa shule hiyo wanatafuta njia za kupambana na tatizo la ujauzito mashuleni lakini lawama zao wameitupia televisheni ya MTV kwa kipindi chao cha mama wenye umri mdogo kinachoitwa "MTV's Teen Mom".

Maafisa hao wamesema kuwa kutokana na umri wao mdogo, wasichana wamekuwa wakiiga wanayoyaona kwenye kipindi hicho wakidhani ndio staili ya maisha.

Maafisa wa kitongoji cha Frayser wamepanga kuanzisha kampeni inayoitwa "No Baby" ili kuwashinikiza wasichana wajizuie kupata mimba mapema.

Idadi ya wasichana waliopata mimba katika kitongoji cha Frayser ni asilimia 10 zaidi ya idadi ya mji mzima wa Memphis.

Afisa mmoja wa shule hiyo aliwatupilia lawama wanaume kuwa nao wanachangia kuongezeka kwa idadi ya wasichana wajawazito kwenye kitongoji hicho.

"Kuna wanaume wengi watu wazima wamekuwa wakiwalaghai kimapenzi wasichana wenye umri mdogo", alisema afisa huyo.
 
Ngono zembe katika umri mdogo na ni hawa blacks. Hawasahau asili like Bongo vile
 
Hivi condoms siku hizi haziko effective au watu wanagonga ngozi kwa ngozi tu?
 
The message sent to Obama and all americans, and am sure that the problem gonna get solutions as soon as possible,
But we've to remember that there is the same problem in our country and never forget to remind our lovely sisters there at schools avoid early pregnancies!
 
Tatizo hilo liko sana Africa na si huku huyu jamaa kapata wapi habari hiyo kama kweli lete SOURCE.
 
Kuna wanaume wengi watu wazima wamekuwa wakiwalaghai kimapenzi wasichana wenye umri mdogo",
hawa ndio mafataki, hat tz ni wengi sana.....
 
Back
Top Bottom