Wanachadema hamjachoshwa na hii too much expectation with zero strategy?

Nini kifanyike ili ccm iwe imeshinda kihalali!

Sheria na kanuni zifuatwe mshindi halali atangazwe. Hatumaanishi kwamba ccm huwa haishindi kihalali sehemu nyingine, bali kuna sehemu nyingi dola hulazimisha ccm kutangazwa washindi. Pitia post nyingi za wanaccm hata hapa jukwaani, wengi hawaamini kwamba ccm inaweza kushinda kihalali kulingana na hali halisi. Wangalau wanategemea 50% ya ushindi wake iupate kwa nguvu ya mwenyekiti wake kama amiri jeshi mkuu.

Kipara kipya bila kujali utaukubali ukweli huu ama la, ccm ni chama kilichochokwa tena kwa sababu za kibinadamu kabisa kwamba kitu kikaa muda mrefu huchosa/kuchokwa. Sababu hizo na ukichanganya kwamba sasa ccm haifanyi siasa za ushawishi bali kulazimisha hapo ndio inakuwa mbaya zaidi. Leo hii rais akitoka nje ya ccm, basi ccm ndio itakuwa mwisho wake. Kinachoifanya ccm iendelee kuwepo kwa hiyo nguvu ya mwenyekiti wake ambaye ni rais ni udhaifu wa wapinzani. Wapinzani hasa cdm wenye wafuasi wengi ni kama wamenasa kwenye mtego wa ccm, wao wamejikita kuhubiri zaidi siasa za madaraka zaidi na sio maendeleo. Hili linawasaidia sana ccm kuwamudu kwani kwenye siasa za madaraka ccm wanambeleko ya dola, lakini cdm wangewachonganisha ccm kwa kuhubiri maendeleo wangewaangusha kirahisi sana. Laiti kama viongozi wa cdm kutokana ushawishi wao wangefanya kama Zitto Kabwe na chama chake, leo hii tungekuwa tunaihesabia ccm dakika za kukata roho. Ccm waendelee kuiombea cdm izidi kulala kwenye siasa za madaraka kwa kubaki na watu kama kina Lowassa, Mashinji nk, lakini wasiombe mtu kama Zitto kuunganisha nguvu na cdm.
 
Back
Top Bottom