Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,410
- 119,115
Ni ukweli ulio wazi kuwa Dr. John Pombe Magufuli ndo raisi wa JMT...ni raisi wa watanzania na sio raisi wa CCM...whether tunampenda au hatumpendi yeye ndo rais...whether tulimchagua au hatukumchagua ila ndo ameshakuwa.
Hatuna budi kusahau maumivu na maisha yaendelee tujenge nchi yetu. Kinachonishangaza hawa wenzetu wa ccm ni kama wamejimilikisha rais,wanaona kama ni wa kwao wao ndio maana hawaishiwi mipasho,full kuzodoana hata kwenye mambo ya kawaida yanayohitaji majadiliano ya kawaida.... Wanamabadiliko tumekuwa kama wakimbizi nchi hii.
Huku mtaani hawaachi kuimba zile nyimbo zao za 'tumejipanga,mwaka huu wataisoma' Mmejipanga kwa lipi tena au mmepanga kutusomesha kwa lipi? Acheni hizo wadau.
Rais ili afanikishe mipango yake na ili atimize ilani ya chama chake anahitaji ushirikiano wa kila Mtanzania kwa nafasi yake...sasa mambo ya kuimbiana mipasho wakati uchaguzi umepita mnataka kutengeneza Tanzania ya namna gani? Mnataka tuendelee kugawanyika kwa misingi ya kisiasa wakati Tanzania yetu moja ili iweje? Msidharau 40% ni kubwa sana kama kundi hili la watu likiamua kuwanyima ushirikiano.
Majadiliano ya kwamba Magufuli anafaa au hafai kwa kipindi hiki mimi naona hayana tija maana kampeni zilishaisha na mtu ameshaapishwa....binafsi watu wanaonitumia vimeseji vya kumsifia au kumponda Magufuli nimewapiga stop... Huu sio muda wa kusifiana au kudongoana,mtu hajamaliza hata wiki tangu aapishwe,utendaji wake hatujauona hebu tuweni na subira then tuone utekelezaji wa yale aliyoyasema.
Ushauri wangu kwa wana-UKAWA naomba tuwe watulivu japo najua tuna maumivu ila tujitahidi kurudisha moyo nyuma na tuwape ushirikiano viongozi wetu waliochaguliwa.
Tuijenge Tanzania yetu, mabadiliko tunayotaka yanaweza kutokea hata chini ya viongozi hawahawa japo mfumo wao umeoza ila hatuwezi kusubiria miaka mingine mitano tukingoja mabadiliko. Mabadiliko yanaweza yasitokee kwa kiwango kile tunachotaka sisi ila ni lazima tuhakikishe walau tunasogea hatua kadhaa.
Mimi yangu ni hayo tu na huo ni ushauri wangu kwa watanzania wenzangu. Ukiona nimeandika pumba au post hii haijafikia kiwango chako pita kimyakimya.