Wamiliki wa lodge kuweni serious

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,906
Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi, au ukumbi wa mikutano na kadhalika. Sometimes kwa sababu ya lodge zingine kuwa zimejaa n.k..

Lakini sasa unaona lodge nzuri Kwa nje na hata ndani Kwa macho unaona iko Sawa, unalipia ulale unashangaa na unayo kutana nayo.

1. Feni inapiga kelele.
2. Bomba bovu maji yanatiririka bafuni.
3. Vitasa vibovu.
4. Mlango wa bafuni haufungi.
5. Taa bafuni haiwaki
6. Kitanda kinatoa milio
7. Mto ngumu Sana au mlaini Sana..
8. Feni haipungui wala kuongezeka Ama uwashe au uzime.
9. AC inapiga kelele
10. Tiles bafuni zina kutu.
11. Wahudumu Wana makelele.

Mradi matatizo ni mengi ambayo mtu anaejali biashara yake ni rahisi kabisa kutatua.

Nashauri kama mtu unamiliki lodge au kuendesha uweke utaratibu wa kulala wewe mwenyewe kila chumba Kwa mda Fulani ukague ujirishishe na huduma unazotoa.

Kuna lodge chumba kimoja kina joto kuliko chumba kingine Nakadhalika.

Kuweni serious, lodge ni sehemu ya mteja kulala comfortable sio kuwaza wateja wote wanaenda kwa ngono tu na kuondoka.
 
Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali..ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi .au ukumbi wa mikutano na kadhalika...
12. Bed sheet jeupee, godoro limechakaa na limevunda
13. Makahaba wanaruhusiwa kiholela kuja kusumbua wateja(shetani ashindwe), Jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa mteja na Mali zake.
14. Kibao Cha Lodge kimeandikwa kuna breakfast na TV lakini hakuna kitu.
15. Kiti Ni kibovu, unakikalia unajikuta umeanguka kwa kisogo, unazirai ukija kuzinduka umeibiwa kila kitu
 
Kuna tule tusabuni tudogo kama kiberiti, sijui wanavinunua Tsh100.. unapewa wakati umelipa 50k+ wanashindwa kutoa sabuni zinazoeleweka, sijawahi kuvitumia kuoga!
Mbaya unamkuta mwamba anaweka kwenye bag, sometime hata wateja tuwe serious!
 
Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi, au ukumbi wa mikutano na kadhalika. Sometimes kwa anaenda kwa ngono tu na kuondoka.
Lala gest ya kuanzia elf40 hutaona huo ujinga, yaan kila siku unalipwa 150k wewe unalala gest ya elf10
 
Siku moja nilisafiri nikakutana na hii lodge.
Sikugusa chochote humo ndani.
Screenshot_20230611-051222_WhatsApp.jpg
Screenshot_20230611-051232_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom