Wameshindwa kuongoza, sasa wanashikana mashati!

Seti kubwa ya UTANZANIA iko katika hali mbaya sana baada ya kiongozi mkuu wa Nchi na wasaidizi wake kutoisimamia vilivyo KATIBA yetu. Sasa hivi kila mtu anajaribu kujihalalisha kwa namna anayoona inafaa. Kama sio KABILA, DINI. Kama sio hayo UZANZIBARI na UBARA.
Mimi naamini mambo haya yamekuwa yakilelewa na kuenziwa na CCM ya sasa na serikali yake. Wanayafanya kwenye TEUZI mbalimbali hasa za ngazi ya TAIFA. Hawaangalii SIFA na UWEZO wa MTEULIWA kwanza, badala yake wanaangalia DINI au MKOA anakotoka.
 
Back
Top Bottom