Wamaasai wa Loliondo: Waziri Lazaro Nyalandu analiongopea Taifa & Rais

HNIC

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
1,898
2,195
Taarifa ya Haraka kwa Vyombo vya Habari Kuhusu Mgogoro wa Ardhi Loliondo

Sisi Viongozi wa Mila, Kisiasa, Wawakilishi wa Wanawake tumesikitishwa sana na Taarifa ya uongo aliyoitoa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu juu ya ukweli wa Mgogoro wa Loliondo. Ifuatayo ni ufafanuzi wa hali halisi kinyume na Waziri alivyodanganya Dunia kupitia BBC tarehe 19/11/2014 na Gazeti la leo la Mwananchi
  1. Kwamba eneo la Loliondo halina Wamaasai 40,000 watakaoadhirika endapo Serikali itatoa tamko Wakati wowote sasa:
Jibu: Idadi ya wakazi katika eneo la km za mraba 1,500 ambavyo ni vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu, Oloipiri, Arash, Maaloni, Olorien/Magaiduru, Piyaya na Malambo ambavyo vina jumla ya wakaazi 57,532. Kwa mujibu wa sensa ya Taifa ya watu na Makazi ya 2012 kama ilivyo kwenye jedwali hapa chini.

SNKataIdadi ya watu
1Arash7,841
2Olosoito/Maaloni4,353
3Oloipiri4,114
4Soitsambu10,956
5Ololosokwan6,557
6Piyaya5,303
7Malambo8,923
8Olorien- Magaiduru9,485
9Orgosorok1,521
10Engusero Sambu12, 268
Jumla71, 321

Vijiji viwili (Engusero sambu na Orgosorok) venye idadi ya watu 13,789 hawana makazi katika eneo la mgogoro lakini ni watumiaji wa eneo hilo la malisho.Hivyo tunathibitisha kuwa watu watakaoathirika eneo hili likichukuliwa ni 71,321.Hivyo Waziri kusema eneo hilo halina watu 40,000 ni uongo mtupu.
  1. Kwamba Serikali ya Tanzania haijawahi kuwa na mpango wa kuwaondoa Wamaasai katika eneo la Loliondo:
1992: Serikali ilitoa ardhi ya vijiji vya Tarafa za Loliondo na Sale kwa Mfalme wa UAE bila RIDHAA ya wananchi na kusababisha mgogoro unaoendelea mpaka sasa. Kumweka mwekezaji katika ardhi ya jamii bila ridhaa ilikua ni mpango wa muda mrefu wa kupora ardhi.

2008: Mgogoro huu umechukua sura tofauti baada ya kampuni kuweka mikakati ya kuchukua ardhi yetu kwa ajili ya uwindaji na kutengeneza mikataba iliyoridhiwa na viongozi na sio wananchi.

2009: Serikali ilitumia mikataba iliyoridhiwa na baadhi ya viongozi wa vijiji kufanya opersheni ya kijeshi ambayo iliharibu rasilimali, ilichoma makazi na kusababisha mtoto moja katika kijiji cha Arash kupotea mpaka leo. Kijana Ngodidio Rotiken alijeruhiwa kwa bomu na kupoteza jicho na madhara mengine mengi.

2010: Serikali ilitengeneza RASIMU ya mpango wa Matumizi wa Ardhi ya Wilaya kwa ufadhili wa OBC wa shilingi 157,000,000. Mpango huo ulitengeneza rasimu ya ramani ya kutenga eneo la Kilomita za Mraba 1,500 kutoka kwenye ardhi ya vijiji. Mpango ulipingwa vikali na kukataliwa na baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro na jamii kwa ujumla kwa sababu ya dhana nzima ya kutenga ardhi ya vijiji bila ushiriki wa wananchi.

2011/12: Serikali kupitia kamishina wa ardhi iliagiza vijiji vya Ololosokwan na Engaresero kurudisha vyeti vya ardhi ya vijiji kwa madai kuwa vina migogoro. Madai hayo yalithibitishwa kuwa ya uongo na yenye hila ya kupora ardhi ya vijiji.

2013: Serikali kupitia Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii (Mhe. Khamis Kaghasheki) ilitangaza RASMI kutenga eneo la Kilomita za mraba 1,500 ya ardhi ya vijiji kuwa Pori Tengefu la Loliondo. Jambo hili lilizua taharuki kubwa ndani na nje ya Nchi na kutishia usalama kwenye jamii ya Wafugaji na hatimaye kumlazimu Waziri Mkuu kuingilia kati.

2014: Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) alizuru Loliondo mara mbili kwa nia ya kuhamasisha na kushawishi madiwani na wenyeviti wa vijiji kukubali pendekezo la Serikali/OBC kutoa FIDIA ya shilingi Bilioni moja kwa vijiji endapo watakubali kuachia eneo la kilomita za mraba 1,500. Pendekezo lake halijakubaliwa hata na viongozi wachache aliyokutana nao.

Tarehe 19/11/2014 wakati wa mahojiano na mtangazaji wa BBC, Mhe. Lazaro Nyalandu alisema alikwenda Loliondo Kuhamashisha Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi:

Jibu: Waziri kisheria, hana mamlaka juu ya kupanga matumizi ya Ardhi ya vijiji na wala haijawahi kuzungumziwa katika mikutano ya Waziri na Baadhi ya Madiwani na wenyeviti alipokuja Loliondo. Mipango ya Matumizi bora ya ardhi za vijiji inaratibiwa na Wizara ya Ardhi na Makazi na sio Wizara ya Maliasili na Utalii…….. Ni Wizara hiyo hiyo inayoongozwa na Nyalandu iliyopinga upimaji wa vijiji uliokuwa unatekelezwa na Wizara ya Ardhi na Makazi mwaka 2013 kwa kuwarudisha ndani ya masaa 24 timu ya wataalamu wakiongozwa na mpima wa Wizara ya Ardhi Ndg. Isaa Marwa waliokuwa wameanza zoezi la upimaji.

Katika Mahojiano na BBC tarehe 19/11/2014, Waziri Nyalandu alisema sio Wamaasai tu wanaishi katika eneo la kilomita za mraba 1500:

Jibu: Wakazi wa eneo hili ni wafugaji wa jamii ya Wamaasai ambao ni zaidi ya 40,000

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 21/11/2014 Mhe Nyalandu alisema "yaani tunapanga kutumia askari kuwaondoa wananchi kwenye maboma yao na kuyachoma moto…..Huu ni uongo, hakuna mpango kama huo"

Jibu: Kwa kuwa Mhe Waziri Lazaro Nyalandu yaelekea hana kumbukumbu ya matukio ya Loliondo tunamrejesha kwenye tukio la mwaka 2009 lililoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia jeshi la Polisi (FFU) kuteketeza kwa moto maboma ya wafugaji ya jamii ya Kimaasai zaidi ya 300 katika eneo la Loliondo.
  1. Baada ya mkanganyiko huu wa Mhe Nyalandu, sisi viongozi wa Kisiasa, Kimila na Wawakilishi wa wanawake tumedhamiria kumwona tena Mhe. Waziri Mkuu ili kupata uhakika wa mpango huu wa Nyalandu, kwani hatuna imani tena na Wizara ya Maliasili na Utalii. Tumeumizwa na kusikitishwa sana na kitendo cha kushindwa kumwona japo tulipata uhakika wa muda wake wa kutuona (appointment) tarehe 19/11/14.
  2. Katika sakata hili tunatoa tena kwa mara nyingine ushauri ufuatao kwa Serikali ili kufikia suluhu ya kudumu kwa mgogoro huu:

I. Waziri Mkuu kutoa agizo lenye masharti ya muda kwa Wazira ya Maliasili na Utalii kufuta kwa Maandishi Tamko lake kwa vyombo vya habari la tarehe 21, Machi 2013 kama ulivyotuahidi Sept mwaka jana.

II. Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kutengua/kufuta hadhi ya Pori Tengefu katika vijiji vya Loliondo kwa mujibu wa sheria mpya ya Wanyamapori ya mwaka 2009 na kuheshimu miliki halali za kisheria kwa ardhi yetu na mfumo wa maisha yetu usioharibu mazingira.

III. Waziri Mkuu kutoa TAMKO kwa umma wa Watanzania na Dunia nzima kwa maandishi kuhusu Ahadi yake ya tarehe 23/9/13 kwetu kwamba Serikali imeachana na mpango wa kupora ardhi ya Vijiji vyetu. Aidha tunamwomba Waziri Mkuu kukemea kwa uzito usumbufu huu tuanoupata watu wa Loliondo toka kwa Wizara ya Maliasili na Utalii unaojirudia kila Wakati.

IV. Tunaishauri Serikali kufuta uwindaji katika Ardhi yetu, kwani hauhifadhi Wanyamapori wala sio rafiki na mazingira, ufugaji na utalii wa picha. Uwindaji katika eneo la Loliondo ni mpango wa kuwamaliza wanyama katika ikolojia ya Serenegeti, Ngorongoro na Maasai Mara. Kuendelea kuruhusu uwindaji katika eneo hili, mgogoro utaendelea na kusababisha madhara endelevu kwa uhifadhi wa wanayamapori, maisha yetu na ustawi wetu.

V. Tunamwomba Mhe. Waziri Mkuu kutoa maelekezo ya haraka kwa Wizara ya Ardhi na Makazi iendelea na zoezi la upimaji wa vijiji lililohairishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii mwezi August, 2013 ili kuharakisha zoezi la kuandaa mipango ya Matumizi ya bora za Ardhi.

VI. Tunamwomba Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza haya kwa muda mfupi uwezekanavyo kwani tumekuheshimu kwa kuvuta subira kwa mwaka mzima kama ulivyotuelekeza kwenye Barua yako ya Mwezi Mei mwaka jana "tuwe watulivu na wavumilivu wakati ukishughulikia kilio chetu". Kama utashindwa kutoa maelekezo hayo ya kutimiza ahadi yako kwetu, basi hatuna budi kuhamasisha dunia kupitia vyombo vya habari na kufika Dodoma ofisini kwako kwa maelfu ili utueleze hatma ya Ardhi yetu na maisha yetu. Japo tunaamini katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani, hata hivyo uvumilivu umetuishia na kamwe ardhi yetu haitaporwa kwa maslahi ya kampuni ya OBC.

Imeandaliwa na:

1.Elias Ngorisa – Mwenyekiti Wa Halmashauri
2. Ibraham Sakai- Mwenyekiti wa CCM Wilaya.
3. Daniel Ngoitiko- Diwani
4. Mathew Siloma- Diwani
5. Tina Timan- Diwani
6. John Kulinja- Kiongozi wa Mila.
7. Mathew Timan- Kiongozi wa Mila
8. Loserian Minis- Mwakilishi wa Wenyeviti wa Vijiji.
9. Kooya Timan – Mwakilishi wa Wanawake
10. Manyara Karia- Mwakilishi wa Wanawake

Imetolewa leo tarehe 21/11/2014, Arusha na Wawakilishi wa Jamii toka Tarafa za Loliondo na Sale.

NATIONAL
By Patty Magubira ,The Citizen Reporter

Posted Sunday, November 23 2014 at 12:35

IN SUMMARY
He stressed that the plan dated back to 1992 when the government offered Lolilondo and Sale ward villages to the United Arab Emirates (UAE) without the consent of the residents.

Arusha. Residents of Ngorongoro District have threatened to ditch Chama Cha Mapinduzi (CCM) if its government implements what they called its long-standing ‘conspiracy' to evict them from their ancestral land.

Their delegation comprising Maasai elders, politicians and women told a press conference here that a series of events dating back to 16 years ago indicated the government was intending to lease their 1,500 square-kilometre land to an investor.

Their claims come just a few days after Natural Resources and Tourism minister Lazaro Nyalandu vehemently dismissed a report by the UK-based Guardian newspaper on Tanzania government's intention to evict them and turn their land into a reserve for the royal family of Dubai to hunt.

An attempt by a 10-man delegation of Loliondo District residents led by the district council chairman Elias Ngolisa to meet Prime Minister Mizengo Pinda in his Dodoma office on their quandaries proved futile on Wednesday despite getting an appointment beforehand.

Addressing journalists on their way back from Dodoma, the CCM chairman for the district, Mr Ibrahim Sakay, asked the ruling party's secretary general to consider intervening in the government's plan to grab the pastoralists land in a bid to meet interests of investors.

He said Mr Nyalandu had visited Ngorongoro thrice lately in his attempt to convince nine councillors on the CCM ticket, including the district chairman and four CCM village chairpersons to buy the government's plan.

The minister's frequent visits had nothing to do with village land use plans as he claimed, for the assignment did not fall in his docket, the CCM district cadre insisted.

He stressed that the plan dated back to 1992 when the government offered Lolilondo and Sale ward villages to the United Arab Emirates (UAE) without the consent of the residents.

In 2008, a fresh row erupted when Ortelo Business Corporation (OBC) -- a luxury safari company set up by an official close to the UAE royal family -- conspired with local leaders to take over their land.

The following year the government enforced the contracts which lacked legitimacy by carrying out a military operation which saw the residents' property destroyed and a mysterious loss of a boy -- Ngodidio Rotiken.

The government drafted Sh157 million worth of a land use plan financed by OBC in 2010 without engaging residents of the district. The commissioner of land ordered Ololosokwan and Engaresero villages to return their village land certificates on grounds that they were mired in conflict.

Last year, the Natural Resources and Tourism ministry announced that he had earmarked 1,500 square kilometres of the Loliondo Wildlife Management Area for tourism, triggering protests from in and outside the country against the decision.
source: THE CITIZEN
 
huu udhalimu na uonevu dhidi ya familia nyingine utawarudia hawa mawaziri wanaofikiria tumbo .... wao na familia zao hata kama sio leo ..... machozi ya mnyonge hayaendi hivi hivi!
 
ina maana Lazaro hana hata wafanyakazi wa kumpa facts?
 
Taarifa ya muda huu toka Loliondo ni kwamba ng'ombe wengi wa wamaasai wa Loliondo wamekamatwa, ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa 'serikali' wa kuwahamisha wamaasai toka katika eneo lao lenye 1,500 sq kms na kumkabidhi mwarabu toka UAE. Waziri Nyalandu na 'serikali' ni waongo. Richmond, EPA, Escrow havijawatosha hata mnapanga njama za kuiba makazi ya asili ya wanadamu wenzenu? Oneni aibu.
 
NATIONAL
[h=1][/h]By Patty Magubira ,The Citizen Reporter

Posted Sunday, November 23 2014 at 12:35

IN SUMMARY

He stressed that the plan dated back to 1992 when the government offered Lolilondo and Sale ward villages to the United Arab Emirates (UAE) without the consent of the residents.

Arusha. Residents of Ngorongoro District have threatened to ditch Chama Cha Mapinduzi (CCM) if its government implements what they called its long-standing conspiracy to evict them from their ancestral land.

Their delegation comprising Maasai elders, politicians and women told a press conference here that a series of events dating back to 16 years ago indicated the government was intending to lease their 1,500 square-kilometre land to an investor.

Their claims come just a few days after Natural Resources and Tourism minister Lazaro Nyalandu vehemently dismissed a report by the UK-based Guardian newspaper on Tanzania governments intention to evict them and turn their land into a reserve for the royal family of Dubai to hunt.

An attempt by a 10-man delegation of Loliondo District residents led by the district council chairman Elias Ngolisa to meet Prime Minister Mizengo Pinda in his Dodoma office on their quandaries proved futile on Wednesday despite getting an appointment beforehand.

Addressing journalists on their way back from Dodoma, the CCM chairman for the district, Mr Ibrahim Sakay, asked the ruling partys secretary general to consider intervening in the governments plan to grab the pastoralists land in a bid to meet interests of investors.

He said Mr Nyalandu had visited Ngorongoro thrice lately in his attempt to convince nine councillors on the CCM ticket, including the district chairman and four CCM village chairpersons to buy the governments plan.

The ministers frequent visits had nothing to do with village land use plans as he claimed, for the assignment did not fall in his docket, the CCM district cadre insisted.

He stressed that the plan dated back to 1992 when the government offered Lolilondo and Sale ward villages to the United Arab Emirates (UAE) without the consent of the residents.

In 2008, a fresh row erupted when Ortelo Business Corporation (OBC) -- a luxury safari company set up by an official close to the UAE royal family -- conspired with local leaders to take over their land.

The following year the government enforced the contracts which lacked legitimacy by carrying out a military operation which saw the residents property destroyed and a mysterious loss of a boy -- Ngodidio Rotiken.

The government drafted Sh157 million worth of a land use plan financed by OBC in 2010 without engaging residents of the district. The commissioner of land ordered Ololosokwan and Engaresero villages to return their village land certificates on grounds that they were mired in conflict.

Last year, the Natural Resources and Tourism ministry announced that he had earmarked 1,500 square kilometres of the Loliondo Wildlife Management Area for tourism, triggering protests from in and outside the country against the decision.

Source: THE CITIZEN
 
Wamasai ni wagumu sana kubadilika wanangatwa na nnge lakini wanaendelea kumkumbatia, watu wa ajabu sana hawapendi badiliko.mi nasema wanyanganywe hata ngombe wao ili wapate akili.
 
Taarifa ya Haraka kwa Vyombo vya Habari Kuhusu Mgogoro wa Ardhi Loliondo

Sisi Viongozi wa Mila, Kisiasa, Wawakilishi wa Wanawake tumesikitishwa sana na Taarifa ya uongo aliyoitoa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu juu ya ukweli wa Mgogoro wa Loliondo. Ifuatayo ni ufafanuzi wa hali halisi kinyume na Waziri alivyodanganya Dunia kupitia BBC tarehe 19/11/2014 na Gazeti la leo la Mwananchi

  1. Kwamba eneo la Loliondo halina Wamaasai 40,000 watakaoadhirika endapo Serikali itatoa tamko Wakati wowote sasa:

Jibu: Idadi ya wakazi katika eneo la km za mraba 1,500 ambavyo ni vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu, Oloipiri, Arash, Maaloni, Olorien/Magaiduru, Piyaya na Malambo ambavyo vina jumla ya wakaazi 57,532. Kwa mujibu wa sensa ya Taifa ya watu na Makazi ya 2012 kama ilivyo kwenye jedwali hapa chini.

SNKataIdadi ya watu
1Arash7,841
2Olosoito/Maaloni4,353
3Oloipiri4,114
4Soitsambu10,956
5Ololosokwan6,557
6Piyaya5,303
7Malambo8,923
8Olorien- Magaiduru9,485
9Orgosorok1,521
10Engusero Sambu12, 268
Jumla71, 321

Vijiji viwili (Engusero sambu na Orgosorok) venye idadi ya watu 13,789 hawana makazi katika eneo la mgogoro lakini ni watumiaji wa eneo hilo la malisho.Hivyo tunathibitisha kuwa watu watakaoathirika eneo hili likichukuliwa ni 71,321.Hivyo Waziri kusema eneo hilo halina watu 40,000 ni uongo mtupu.

  1. Kwamba Serikali ya Tanzania haijawahi kuwa na mpango wa kuwaondoa Wamaasai katika eneo la Loliondo:
1992: Serikali ilitoa ardhi ya vijiji vya Tarafa za Loliondo na Sale kwa Mfalme wa UAE bila RIDHAA ya wananchi na kusababisha mgogoro unaoendelea mpaka sasa. Kumweka mwekezaji katika ardhi ya jamii bila ridhaa ilikua ni mpango wa muda mrefu wa kupora ardhi.

2008: Mgogoro huu umechukua sura tofauti baada ya kampuni kuweka mikakati ya kuchukua ardhi yetu kwa ajili ya uwindaji na kutengeneza mikataba iliyoridhiwa na viongozi na sio wananchi.

2009: Serikali ilitumia mikataba iliyoridhiwa na baadhi ya viongozi wa vijiji kufanya opersheni ya kijeshi ambayo iliharibu rasilimali, ilichoma makazi na kusababisha mtoto moja katika kijiji cha Arash kupotea mpaka leo. Kijana Ngodidio Rotiken alijeruhiwa kwa bomu na kupoteza jicho na madhara mengine mengi.

2010: Serikali ilitengeneza RASIMU ya mpango wa Matumizi wa Ardhi ya Wilaya kwa ufadhili wa OBC wa shilingi 157,000,000. Mpango huo ulitengeneza rasimu ya ramani ya kutenga eneo la Kilomita za Mraba 1,500 kutoka kwenye ardhi ya vijiji. Mpango ulipingwa vikali na kukataliwa na baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro na jamii kwa ujumla kwa sababu ya dhana nzima ya kutenga ardhi ya vijiji bila ushiriki wa wananchi.

2011/12: Serikali kupitia kamishina wa ardhi iliagiza vijiji vya Ololosokwan na Engaresero kurudisha vyeti vya ardhi ya vijiji kwa madai kuwa vina migogoro. Madai hayo yalithibitishwa kuwa ya uongo na yenye hila ya kupora ardhi ya vijiji.

2013: Serikali kupitia Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii (Mhe. Khamis Kaghasheki) ilitangaza RASMI kutenga eneo la Kilomita za mraba 1,500 ya ardhi ya vijiji kuwa Pori Tengefu la Loliondo. Jambo hili lilizua taharuki kubwa ndani na nje ya Nchi na kutishia usalama kwenye jamii ya Wafugaji na hatimaye kumlazimu Waziri Mkuu kuingilia kati.

2014: Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) alizuru Loliondo mara mbili kwa nia ya kuhamasisha na kushawishi madiwani na wenyeviti wa vijiji kukubali pendekezo la Serikali/OBC kutoa FIDIA ya shilingi Bilioni moja kwa vijiji endapo watakubali kuachia eneo la kilomita za mraba 1,500. Pendekezo lake halijakubaliwa hata na viongozi wachache aliyokutana nao.

Tarehe 19/11/2014 wakati wa mahojiano na mtangazaji wa BBC, Mhe. Lazaro Nyalandu alisema alikwenda Loliondo Kuhamashisha Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi:

Jibu:
Waziri kisheria, hana mamlaka juu ya kupanga matumizi ya Ardhi ya vijiji na wala haijawahi kuzungumziwa katika mikutano ya Waziri na Baadhi ya Madiwani na wenyeviti alipokuja Loliondo. Mipango ya Matumizi bora ya ardhi za vijiji inaratibiwa na Wizara ya Ardhi na Makazi na sio Wizara ya Maliasili na Utalii…….. Ni Wizara hiyo hiyo inayoongozwa na Nyalandu iliyopinga upimaji wa vijiji uliokuwa unatekelezwa na Wizara ya Ardhi na Makazi mwaka 2013 kwa kuwarudisha ndani ya masaa 24 timu ya wataalamu wakiongozwa na mpima wa Wizara ya Ardhi Ndg. Isaa Marwa waliokuwa wameanza zoezi la upimaji.

Katika Mahojiano na BBC tarehe 19/11/2014, Waziri Nyalandu alisema sio Wamaasai tu wanaishi katika eneo la kilomita za mraba 1500:

Jibu
: Wakazi wa eneo hili ni wafugaji wa jamii ya wamaasai ambao ni zaidi ya 40,000

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 21/11/2014 Mhe Nyalandu alisema "yaani tunapanga kutumia askari kuwaondoa wananchi kwenye maboma yao na kuyachoma moto…..Huu ni uongo, hakuna mpango kama huo"

Jibu: Kwa kuwa Mhe Waziri Lazaro Nyalandu yaelekea hana kumbukumbu ya matukio ya Loliondo tunamrejesha kwenye tukio la mwaka 2009 lililoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia jeshi la Polisi (FFU) kuteketeza kwa moto maboma ya wafugaji ya jamii ya Kimaasai zaidi ya 300 katika eneo la Loliondo.

  1. Baada ya mkanganyiko huu wa Mhe Nyalandu, sisi viongozi wa Kisiasa, Kimila na Wawakilishi wa wanawake tumedhamiria kumwona tena Mhe. Waziri Mkuu ili kupata uhakika wa mpango huu wa Nyalandu, kwani hatuna imani tena na Wizara ya Maliasili na Utalii. Tumeumizwa na kusikitishwa sana na kitendo cha kushindwa kumwona japo tulipata uhakika wa muda wake wa kutuona (appointment) tarehe 19/11/14.
  2. Katika sakata hili tunatoa tena kwa mara nyingine ushauri ufuatao kwa Serikali ili kufikia suluhu ya kudumu kwa mgogoro huu:

I. Waziri Mkuu kutoa agizo lenye masharti ya muda kwa Wazira ya Maliasili na Utalii kufuta kwa Maandishi Tamko lake kwa vyombo vya habari la tarehe 21, Machi 2013 kama ulivyotuahidi Sept mwaka jana.

II. Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kutengua/kufuta hadhi ya Pori Tengefu katika vijiji vya Loliondo kwa mujibu wa sheria mpya ya Wanyamapori ya mwaka 2009 na kuheshimu miliki halali za kisheria kwa ardhi yetu na mfumo wa maisha yetu usioharibu mazingira.

III. Waziri Mkuu kutoa TAMKO kwa umma wa Watanzania na Dunia nzima kwa maandishi kuhusu Ahadi yake ya tarehe 23/9/13 kwetu kwamba Serikali imeachana na mpango wa kupora ardhi ya Vijiji vyetu. Aidha tunamwomba Waziri Mkuu kukemea kwa uzito usumbufu huu tuanoupata watu wa Loliondo toka kwa Wizara ya Maliasili na Utalii unaojirudia kila Wakati.

IV. Tunaishauri Serikali kufuta uwindaji katika Ardhi yetu, kwani hauhifadhi Wanyamapori wala sio rafiki na mazingira, ufugaji na utalii wa picha. Uwindaji katika eneo la Loliondo ni mpango wa kuwamaliza wanyama katika ikolojia ya Serenegeti, Ngorongoro na Maasai Mara. Kuendelea kuruhusu uwindaji katika eneo hili, mgogoro utaendelea na kusababisha madhara endelevu kwa uhifadhi wa wanayamapori, maisha yetu na ustawi wetu.

V. Tunamwomba Mhe. Waziri Mkuu kutoa maelekezo ya haraka kwa Wizara ya Ardhi na Makazi iendelea na zoezi la upimaji wa vijiji lililohairishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii mwezi August, 2013 ili kuharakisha zoezi la kuandaa mipango ya Matumizi ya bora za Ardhi.

VI. Tunamwomba Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza haya kwa muda mfupi uwezekanavyo kwani tumekuheshimu kwa kuvuta subira kwa mwaka mzima kama ulivyotuelekeza kwenye Barua yako ya Mwezi Mei mwaka jana "tuwe watulivu na wavumilivu wakati ukishughulikia kilio chetu". Kama utashindwa kutoa maelekezo hayo ya kutimiza ahadi yako kwetu, basi hatuna budi kuhamasisha dunia kupitia vyombo vya habari na kufika Dodoma ofisini kwako kwa maelfu ili utueleze hatma ya Ardhi yetu na maisha yetu. Japo tunaamini katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani, hata hivyo uvumilivu umetuishia na kamwe ardhi yetu haitaporwa kwa maslahi ya kampuni ya OBC.

Imeandaliwa na:

1.Elias Ngorisa – Mwenyekiti Wa Halmashauri
2. Ibraham Sakai- Mwenyekiti wa CCM Wilaya.
3. Daniel Ngoitiko- Diwani
4. Mathew Siloma- Diwani
5. Tina Timan- Diwani
6. John Kulinja- Kiongozi wa Mila.
7. Mathew Timan- Kiongozi wa Mila
8. Loserian Minis- Mwakilishi wa Wenyeviti wa Vijiji.
9. Kooya Timan – Mwakilishi wa Wanawake
10. Manyara Karia- Mwakilishi wa Wanawake

Imetolewa leo tarehe 21/11/2014, Arusha na Wawakilishi wa Jamii toka Tarafa za Loliondo na Sale.

Timan alikuwa mbunge wa maeneo hayo miaka ya nyuma,amekuwa kiongozi wa mila? Am a little bit confused, anyway that is not an issue, nadhani yaliyoandikwa humu ni kweli kabisa na mimi naunga mkono hoja Nyalandu ni mgumu sana wa kuelewa na ni mwepesi wa kusahau, au ni hizi hela la escrow ndo zinamsumbua pia? Usikute alipata mgao pia
 
Waziri Nyalandu atamdanganyaje rais Kikwete wakati Kikwete ndiye anayemtuma Nyalandu kusema anayoyasema?

Watanzania mbona mnampa rais kinga asiyostahili?
 
Nyalandu ni kiongozi mbovu lakini kwa hili namtetea. Nilipata kuandika 'bila kudhibiti NGOs loliondo haitawaliki'. Hii ni taarifa ya ngos za wakenya. Wanasumbua sana. Kinara wabkupost haya ni raia wa kenya aliyeajiriwa wizara ya maliasili na utalii. Tunamjua na anayetaka jina na namba yake ani-pm. Nasema, nyalandu ni waziri mbovu lakini kwa uzushi huu nitamtetea.
 
KUWAPA MAENEO HAYA WATU WAKAYAANGALLIA NI BORA ZAIDI NA SALAMA KATIKA KULINDA UJANGIRI.

UWINDAJI UNAOFANYIKA NI KWA VIBALI NA HATA MIMI NA WEWE VIBALI HIVYO UKITAKA UNAVIPATA.

TATIZO TUNAWATUMIA WAMASAI VIBAYA.UKWELI WAMASAI NJIA ZAO ZA UFUGAJI ZIMEPITWA NA WAKATI. WAMEKUA WAKITEMBEA NA KUSABABISHA MAPIGANO SEHEMU NYINGI NCHINI.

inachotakiwa ni kuwapa elimu sahihi ya kuandaa mashamba yao kwa ajili ya malishisho ya ngombe na sio kuhama hama dunia nzima..lazima wabadilike..hakuna njia nyengine.

Ardhi Tanzania ni mali ya Tanzania hakuna ardhi ya wamasai, ndio maana kule Mtwara pia waliambiwa Gas ni ya tanzania na walipo fanya fujo walipelekewa jeshi kutiwa adabu...labda kule kwa sababu ni waislam ..na wamasai wanatumiwa na kuchoma sehemu za wawekezaji na hakuna hatua za kijeshi zinazo chukuliwa.

Hawa manasai wanapoona ardhi mwekezaji ameindeleza wanakuja wanasiasa uchwara wanawatia maneno machafu ili wafanye uhalifu kusingizia ardhi ya wamasai.

tanzania hakuna ardhi ya wasukuma au wazaramo au wamakonde umuliki huu haupo.Majuzi waliharibu eneo la hifadhi huko Ndarakwai kwa kulichoma moto..huu ni uhuni na uhalifu mkubwa sana mimi nasema Tanzania tuko double standard sana kwenye kushurutisha sheria. Laiti ingekua uchomaji ule umefanywa Mtwara au Lindi kwenye waislam wengi basi serikali hii hii ingetumia nguvu kubwa sana kuwashikisha adabu wahalifu hao wa mtwara, lakini wamasai wabunge wao na viongozi wana wasapoti ni dini nyengine hakuna hata nzi aliye guswa!

Someni hapa kisa cha mwenye mali yake ambaye wamasai hao wanao tumiwa walivi haribu mali zake

Hi Everyone,
I am sure that everyone knows by know about what happened at Ndarakwai last friday. What hurts me the most is the negative comments i keep hearing and reading. This is one that annoys me a lot and i want to share his comments and my response with everyone. It would be great it people could read it all they way through to get the full story.

"You were not supposed to give these lands to foreigners and denying rights to Masai People. It has been their land for years. What Tanzania failed to do is to grant these prime lands to outsiders for investment without discussing with the locals. No one in Europe or USA give their prime investment lands to someone not native or citizens. They know damn well how much a stake that is. The Masai could have given the rights to build and operate those safaris for their benefit. I dont blame these Masai People I blame the government officials to fail to recognize the injusticeness to the Masai people. They should also stop using Masai for advitisement for free.

They came in the name of invironment, paid nothing and making a hell of money which does not benefit the Masai or Tanzanians. Our leaders have been manipulated knowingly they cant think out of the box. Tanzania and many other African Countries have become resources for money for developed countries. These contracts and land leasing must be reviewed. Colonies coming back where they left and exploiting people using Government lazzy thinkers and lazzy planners."

Hi Bodi,

I am actually a director of the lodge that got burnt down in West Kili. There are a few things you need to know first, before being able to comment on such a sensitive topic. I will go through your post…

"It has been their land for years"
This is untrue, there are over 120 different tribes in Tanzania, (you seem to only know about one, the Maasai) and this was never maasai land, I really don't know how you can make that comment….

"What Tanzania failed to do is to grant these prime lands to outsiders for investment without discussing with the locals"
Again, i don't see how you can say this because before even thinking about getting the land in 1995 we did exactly that - go to every single village and community around us and explained to them our intentions. Also… this is not "prime land". West Kilimanjaro has a rain shadow effect from its position around Mount Kilimanjaro. Out of any other area around the mountain, it gets the least amount of rainfall. This is an area that was unfit for agriculture or cattle, which made us think that the land could be conserved to sustainably maintain wildlife populations.

"They came in the name of invironment, paid nothing and making a hell of money"

This is a biggie.. please read all…. Our intention at Ndarakwai was to create "self sustaining conservation". This, is in its most basic terms, is conservation that does not rely on donations. If you were to walk on Ndarakwai in 1995, you would not see one single animal. In 18 years of conservation we have completely restored the habitat and brought back over 65 mammal species and over 300 bird species. We built the lodge as a way for us to maintain this conservation (I believe this is crucial because the lodge can then finance the conservation, while promoting Tanzania and helping communities). With everyone working in the lodge coming from all of the direct communities around us, we were able to start helping a wider group of people.

As things grew, we realised that we were able to continue our community work. In 2006 we started supporting the O-Vet Primary school. We started supplying meals every day for 150 children. By 2014, the school has over 400 children (which are all being fed from the proceeds of the lodge we built, a lot of which are Maasai children) and the school has gone from unranked in the district to #1 , and to #4 in the entire Kilimanjaro region. We have also re built parts of the school, and built a complete kitchen. We have also started building a dormitory for Tinga Tinga secondary school so children didn't have to walk kilometres a day to get to and from school. (A project that is now stopped due to the lodge being burnt down). These are a number of things that we do, among a whole list. Others include creating local business like fish farming and supplying bee hives for honey harvesting. When one project is on its feet and running well, we start another.

"Which does not benefit the Maasai or Tanzanians"

We employ people from over 15 different tribes at Ndarakwai, and we have many employees who have been with us for over 15 years. Your comment is strange because we protect the Tanzanian land…. protect the Tanzanian wildlife, employ the Tanzanian people (including maasai), pay taxes to the government, work on community projects, so i don't know how you can say it doesn't benefit Maasai or Tanzanians…

Now…. finally back to the "Maasai mob who torched our camp". There are rumours going around that they burnt it down because we were adding to our conservation area. This is simply not true. Not only is the border of our land also the border of our district, but it is also the border between Kilimanjaro and Arusha Region. We have never ever tried to expand our property. The truth of the mater is this……

Maasai entered our conservation area in force so they are able to graze their cattle. Why? because we have done such a good job in land conservation that the grass has completely returned and they want it all.

On the other side of things, why are their no other areas for the Maasai to graze other then our property??? It is because all of the land around us, for over 50 kms in every direction of us has been completely overgrazed. Our property is 11,000, but the land around us is over 300,000 acres. If all of the grass is gone in the 300,000 acres around us, how long will it take to completely finish the grass we spent so long trying to conserve for wildlife populations? And after they do finish our grass… where will they go? another property? a village? where does it end? To add on, why are they completely over grazing hundreds of thousands of acres? why are they not growing trees, what are they doing to help the environment or Tanzania?

I employ over 75 people which directly benefits the community around us. We buy all our local produce from farmers around us, eggs, pork, milk as well. We support over 400 children in a school (for over 8 years), and more and more businesses have opened in Siha District because of us. You say i come in and make a lot of money…. i invite you to come to my house and see what "luxury" i live in, i really do. I am so sick of the truth not getting out, and people forgetting that there are over 120 other tribes who need help in this country, not just Maasai. I was born and raised in Tanzania, I do apologise for being born white, otherwise I might actually have been taken seriously in this country of mine.

I am sorry if this post is controversial, but i can't stand that Maasai keep turning their land into deserts and feel it is ok to ruin something that someone else has worked so hard to build. I do not know why the world holds them on such high pedestals, while criticising people who are actively working on helping this country.
 
bado ana ndoto za kuwa rais huyu jamaaa
 
"Nyalandu ni kiongozi mbovu lakini kwa hili namtetea. Nilipata kuandika 'bila kudhibiti NGOs loliondo haitawaliki'. Hii ni taarifa ya ngos za wakenya. Wanasumbua sana. Kinara wabkupost haya ni raia wa kenya aliyeajiriwa wizara ya maliasili na utalii. Tunamjua na anayetaka jina na namba yake ani-pm. Nasema, nyalandu ni waziri mbovu lakini kwa uzushi huu nitamtetea."

Asilimia 95%ya madiwani wote wilayani Ngorongoro ni wakenya.asilimia 90% ya wenyeviti wa vijiji ni wakenya wanaoingizwa kwa mbinu ya rushwa na zaidi ya NGO 30 zilizotapakaa eneo dogo la Loliondo.

Hata hawa walioorodhesha majina yao ni wakenya.

Ushauri wangu wa bure huu ujumbe mlioweka hapa ni wa kibaguzi.acheni kuwaingiza wenzenu bila kufuata utaratibu.
Uhamiaji wilaya ya Ngorongoro haitimizi majukumu yake zaidi ya kuwalinda wahamiaji haramu wa koo za Loita na Purko zilizojimilikisha ardhi ya Tanzania kinyume cha sheria miaka ya 1990
 
Kwenye rangi nyekundu ni mtu na mke wake.

sasa muulizeni M.Timan mke wake sio Mkenya tena ukoo wa Loita toka Ndyamanangi?

Tunaofahamu siasa za wilaya ya Ngorongoro hawa hawatupi shida, hizi ni siasa za maji taka na ni za kikakila zaidi.
na hao wote ni wasaka tonge kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwakani.

Timan alikuwa mbunge wa maeneo hayo miaka ya nyuma,amekuwa kiongozi wa mila???am a little bit confused,anyway that is not an issue,nadhani yaliyoandikwa humu ni kweli kabisa na mimi naunga mkono hoja Nyalandu ni mgumu sana wa kuelewa na ni mwepesi wa kusahau,au ni hizi hela la escrow ndo zinamsumbua pia?usikute alipata mgao pia
 
Back
Top Bottom