Waliovunjiwa Madale Nakasangwe "B"Kuna harufu ya rushwa!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,584
8,611
Inasemekana watu waliovunjiwa Nyumba nakufukuzwa maeneo ya Madale Nakasanga"B" Wameonewa na wafanyabiashara waliodai wamevamiwa maeneo yao, kumbe waliowengi maeneo siyo yakwao na wengi wao ni waarabu walichangishana sh,3milioni! ili wauonge uongozi wamkoa wa Dar es salaam usimamie zoezi hilo!!Na zoezi hilo lilisimamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.Kwakiwango kikubwa ambapo walivunja nyumba za wakazi wa hapo na kukiuka haki zabinadamu kwakuwachomea nyumba zao na kuwabambikia kesi kuwa wao ni waamiaji haramu!!
 
Nenda mahakamani uone,walishashitakiwa since last year na hukumu ilitolewa this year wenyewe ktk kesi pamoja na kuitwa hata hawakutokea,leo unakuja kusema wameonewa,nani ambaye anaweza kuhonga mkuu wa mkoa pesa ili watu wahamishwe tu sehemu for his benefit pasipo yeye kumiliki?kama hali ingekuwa hivyo kwa nini mwananyamala ama gongo la mboto wasihonge halafu waende kubomolewa?tusipende kulalamika ovyo tu,na wamiliki ambao walikuwa na maeneo yao hapo baadhi washayauza ,yaweza kuwa umeona muarabu huyo kauziwa na mtu ama hata yeye akiwa anamiliki kwani ni kinyume cha sheria kumiliki ardhi?ok hawana hati je ni watanzania wangapi mpaka sasa wanaomiliki ardhi bila hati?kwa hiyo unashauri watu wakiona ardhi haina hati wavamie tu na kuweka makazi holela pasipo mpangilio?asante
 
Mhm!!Ila hapo mkuu naona kama umeshambulia kwani swala la huko Madale ni swala mtambuka ukiangalia zoezi zima lilivyoendeshwa kuna uwalakini japo mimi sina uhakika kwa hilo kwa tetesi zinasema wafanya biashara walijichangisha shilingi milioni tatu kwakila kichwa wakapeleka kwauongozi wamkoa either ni mkuu wamko sijui lakini kunakitu kama hicho!!
 
Back
Top Bottom