ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,115
- 49,836
Nssf imesema imewalipa Watumishi Feki zaidi ya 13,000 takribani Bilioni 35 kama Rais Samia alivyoagiza.
Ikumbukwe hao walioitwa Watumishi Feki walifukuzwa utumishi na Marehemu Magufuli Kwa visingizio vya kukosa vyeti bila ya kulipwa hata senti Moja.
My Take
Mpaka hapa Rais Samia ana mtaji wa kura 13*000 kutoka Kwa Watumishi Feki.
---
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Hosea Kashimba amesema, wametumia zaidi ya Sh35 bilioni mpaka sasa kuwalipa waliokuwa watumishi wa umma 13,000 waliobainika kuwa na vyeti feki.
Kishimba amesema hayo leo Alhamisi, Agosti 31, 2023 jijini Dar es Salaam katika kikao kazi baina ya mfuko huo na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
"Hatuna madai ya watumishi wa vyeti feki, pengine ambao bado labda hawajui au walirudi kijijini, lakini wakija wanalipwa haraka kwani tumeweka dawati maalum," amesema Kishimba na kuongeza:
"Tunataka huruma ya mheshimiwa Rais aliyoitoa wanaipata kwa wakati na tumejipanga vyema."
Kishimba amesema baada ya tangazo,"kutoka kuwa una cheti feki wengine walikimbia, sasa baada ya tangazo la kuanza kutoa mafao wanakuja na wakija tunafuatilia utumishi, tukiona michango yao tunawapa mafao."
Mwaka 2022, Rais Samia Suluhu Hassan alitaka watumishi hao waliobainika kuwa na vyeti feki na kuondolewa katika utumishi wa umma walipwe mafao yao.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma

Bilioni 47 zilizotengwa Vyeti Feki walipwe hawa
SUALA la kulipwa watumishi wa umma waliotumbuliwa vyeti feki kiasi cha shilingi Bilioni 47 linaonekana kuwa na kizungumkuti wa kisheria ndio maana hadi sasa hakuna Waziri Jenista Mhagama anawalalamikia maafisa utumishi kwamba wamekaidi agizo la Rais. Nilikuwa nashauri hizo bilioni 47 zitumika...
www.jamiiforums.com