Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,495
- 37,787
Ulianza vizuri mbio zako baada ya kupokea kijiti Kwa bahati ya Mungu. Watu wa Pwani tunasema ulianza na mguu mzuri baada ya kuchagua uelekeo tofauti na mtangulizi wako kuhusu demokrasia na mahusiano ya ndani na nje.
Uliwafanya wengi wakuamini na kukupenda ghafla Kwa vile siasa za mtangulizi wako ziliumiza wengi nje na ndani ya Chama chako.
Ulikuwa na nafasi nzuri ya kuchukua mema ya watangulizi wako na kuacha mabaya yao maana ulikuwa mchezaji wa akiba uliyeingia uwanjani kutokana na mabadiliko ya lazima.
Baada ya Wahafidhina kuona unaelekea kuzuri na utafunika ndoto zao na maslahi yao, wakakufuata na ngonjera zao za siku zote nawe ukawakubalia na kutoka kwenye reli.
Ghafla, ukachukua Tabia ya udikteta toka kwa mtangulizi uliyemrithi, ukawa Mbabe wakike na kuunguruma hata mahali palipohitaji mazungumzo, ukaacha kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake kama ilivyokuwa wakati wa Mtangulizi wa mtangulizi wako yaani Mzee Tabasamu. Ukaacha uchumi uende unavyojiendea kama ilivyokuwa kabla ya 2015.
Ukaacha kundi la wenye kejeli ya kipato lianze kuwakejeli wasio nacho Kwa kuwaelekeza wahame nchi aidha waende Burundi kwa Bibi yao au Kenya kwa mjomba.
Wakakutengenezea utamaduni wa sifa na mapambio na kudanganya ndizo zitakazokuongezea mvuto. Wakasema mtangulizi wako alipendwa kwa sababu alisifiwa bila sababu na nchi nzima ikajaa mabango yake. Nawe ukaamuru fungu litolewe picha zako zisambazwe bara na Pwani na njia zote zienee kama mgombea mmoja aa 2015 alivyojitandaza kwenye mawe.
Nadhani Sasa umeona mwenyewe upotoshaji wa Wachumia tumbo. Kila unachoshika kinakosa mvuto. Umebadili Waenezi wanne Kwa miaka 3 lakini bado ha2kusaidia jina lako kuenea. Ukateua vyeo visivyotambulika kikatiba ili kuvutia kabila lile kubwa lakini Hakuna aliyevutika. Ukasema ujaribu kambi ya Mzee Mamvi labda utaambulia mvuto wake wa M4C lakini wapi.
Hizi makeup zote zimebuma Mamangu Kipenzi. Dawa ilikuwa ni kubaki kwenye misingi ya maridhiano na kulileta Taifa pamoja kama ulivyoanza. Bado hujachuelewa, fanya Sasa na utaona matokeo yake. Wasaidie Watanzania kupata walichokikosa Tangu 1992 (katiba Bora).
Warudishie Watanzania maamuzi Yao wanapopanga mistari toka alfajiri kupiga Kura. Wasaidie kile walichoamua kisimame kama kilivyo badala ya Wakurugenzi kutangaza wateule badala ya wachaguliwa. Umeona Mbunge wako wa Same alivyopopolewa maneno mbele ya MC wa Chama chenu huko Kilimanjaro, na hiyo ni trailer, bado Action yenyewe mwakani.
Bado hujachelewa anza sasa.
Wasalaam,
Mjukuu wa Kizimkazi.