Waliojiuzulu udiwani Meru wabwagwa kura za maoni CCM, wamwangukia Magufuli

kumbe hawakupewa ajira nyingine? ma****! sitamani hata kuwasikia hao mafisi tamaa zao wanaingiza taifa kwenye garama za kijinga
 
Ccm watu wa ajab kabisa..wanapitisha mazimio kuwa mwanachama alie toka chama ch upinzani asigombee nafasi mpaka ipote miaka 2 ..lakini kwa kudhani hawa madiwani bado wata shinda uchaguzi wamesahau maazimio yao
 
Si Mnyeti aliwamwagia AJIRA ambazo tunawapa wadogo zetu nauli wakafanye interview?
 
Arusha. Madiwani watatu wa Chadema waliojiuzulu katika Halmashauri ya Meru mkoani Arusha na kujiunga na CCM, wameangushwa katika kura ya maoni ndani ya chama hicho.

Madiwani hao waliojiuzulu hivi karibuni kwa kile walichoeleza ni kutokana na kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli waliomba kutetea nafasi zao.

Waliogombea na kuangushwa ni Solomon Laizer, aliyekuwa diwani wa Ngabobo, Japhet Jackson (Embuleni) na Anderson Sikawa (Leguruki).

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meru, Andrew Mungure amesema leo Jumatano Oktoba 18 kuwa, matokeo ya kura ya maoni si mwisho wa uteuzi. Uchaguzi huo ulifanyika jana Jumanne.

Mungure amesema wagombea katika kata hizo watajulikana baada ya vikao ambavyo vimeanza leo.

"Leo wanajadiliwa wagombea wote ngazi ya kata, baadaye tutajadili kamati ya siasa na halmashauri kuu ya mkoa ndipo watapitishwa wagombea," amesema.

Amesema kutokana na mchakato huo, matokeo ya kura ya maoni si mwisho.

Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Aloyce Hayuma amekiri madiwani hao kugombea na kushindwa. Hata hivyo, amesema mchakato unaendelea.

- ITV
 
Piga makofi Piga makofi.. Piga makofi tafadhali..

CCM ni kiini cha Rushwa mlidhani unapita kwa uwezo na hoja mtasubiri sana..Milion 2 zimeisha..
 
Waliokuwa madiwani wa CHADEMA mkoani Arusha,waliohamia ccm kwa kile walichodai ni kumuunga Rais Magufuli Mkono ,wameangukia pua kwenye kura za maoni ndani ya Ccm,
Chanzo;Gazeti la Mwananchi
 
Aibu yao, hakika malipo ni hapa hapa duniani. Ahsante sana mkuu wa wilaya, umesaidia sana sana kuwafanya watu wajitambue zaidi
 
Yani Tanzania ili iendelee lazima CCM iondoke madarakani..
So CCM kwa akili zao waliona wamepata kweli wale madiwani..!?
CCM ni kusanyiko la binadamu WAPUMBAVU.
 
Katika kata zote ni Emmanuel Mollel peke yake wa kata ya MAKIBA aliyeibuka kidedea, wengine wote katika kata zao wameangukia pua maskini!

Kituko kikubwa ni kata ya Ambureni Japhet Jackson ambaye NAYE alijiuzulu udiwani kupitia CHADEMA kwa ahadi ya kupewa nafasi ya kugombea ndani ya CCM, yeye alipata kura 4 (kati ya hizo 2 alizawadiwa na mwenyekiti wa kikao ili kuficha aibu).

Ndugu huyu sasa anahaha kufanya mazungumzo na viongozi wa wilaya akiwakumbusha ahadi aliyotoa Mwenyekiti wa CCM John Magufuli, stadium kuwa "tutawarudisha hawa hawa" Kura zilipigwa jana lakini leo ameamkia wilayani na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa apate tiketi ya kugombea udiwani aliouachia.

Wajumbe wa kamati ya siasa wana mkejeli kuwa atajiju, lakini wengine wapo bega kwa bega na yeye.

Pia PCCB walifika katika shule yake kuulizia kama kuna nafasi ya kuleta watoto (walijifanya wazazi wahamiaji), jamaa akawaambia shule ilifungwa. Itakumbukwa kuwa moja ya ahadi alizopewa ili kuachia udiwani ni kufunguliwa kwa shule yake ambayo ameijenga kwenye tindiga ambayo serikali waliifungu.

Lakini baada issue ya Nassary kubumburuka, wakaifunga haraka, hivyo PCCB walipokuja kwake aligundua mtego akategua. Balaa hii!!! udiwani hana, shule bado imefungwa.

Nitaendela kuwajuza.
 
Back
Top Bottom