Waliochelewa kuripoti JKT wakataliwa kupokelewa

Mlendamboga

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
664
334
Wahitimu wa kidato cha sita waliochelewa kuripoti kambini tarehe 11/6/2023 wamezuiwa kuripoti na kuungana na wenzao. Zaidi ya vijana 150 katika kambi ya JKT Mafinga wamerejeshwa wakati wakiripoti jana 12/6/2023 siku moja baada ya tarehe ya mwisho.

Kwa wale waliofika jana jioni walipewa hifadhi mpaka asubuhi kwaajili ya usalama wao na leo asubuhi wametakiwa kurejea kwao. Nidhamu ya jeshi ni msingi wa jeshi imara! walidhani ni kule sekondari mtu anavuta wiki mbili mbele baada ya shule kufunguliwa.

Wazazi kama mwanao alienda JKT tarehe 12/6 wasiliana naye ama mtumie nauli yupo nje anapunga upepo!
 
Hahahaaaaaa peleka siasa zako huko, jeshi sio kikundi cha upatu mzee na ndio maana likaitwa jeshi sasa kama unataka kujua kwa sheria ipi nenda pale kawaulize
Pale ni jeshini au mgambo. Jwtz haiwezi kufanya upuuzi kama huo .
 
Pale ni jeshini au mgambo. Jwtz haiwezi kufanya upuuzi kama huo .
Wewe ambaye huelewi chochote kuhusu jeshi ni haki yako kudhani JKT ni mgambo, na sidhan kama hata JWTZ unaijua vizuri wewe,kwa taatifa yako kwa JWTZ kuchelewa kambini kwa muda ulio pangwa na hasa kama ni mafunzo kunaweza kukufanya ukafukuzwa kabisa ukisindikizwa na adhabu kali kabisa.
 
Wahitimu wa kidato cha sita waliochelewa kuripoti kambini tarehe 11/6/2023 wamezuiwa kuripoti na kuungana na wenzao. Zaidi ya vijana 150 katika kambi ya JKT Mafinga wamerejeshwa wakati wakiripoti jana 12/6/2023 siku moja baada ya tarehe ya mwisho.

Kwa wale waliofika jana jioni walipewa hifadhi mpaka asubuhi kwaajili ya usalama wao na leo asubuhi wametakiwa kurejea kwao. Nidhamu ya jeshi ni msingi wa jeshi imara! walidhani ni kule sekondari mtu anavuta wiki mbili mbele baada ya shule kufunguliwa.

Wazazi kama mwanao alienda JKT tarehe 12/6 wasiliana naye ama mtumie nauli yupo nje anapunga upepo!
Nadhani Uongozi wa Jeshi katika kila Kambi unapaswa kumhoji kila mtu mmoja mmoja juu ya sababu zilizofanya Mwanafunzi kuchelewa kuripoti kambini katika muda uliopangwa kuliko kuwarudisha nyumbani wote pamoja kwa ujumla.

Yawezekana kabisa wapo baadhi ya Wanafunzi wenye sababu za msingi kabisa (reasonable and genuine reasons) zilizowakwamisha wasiripoti kambini kwa wakati muafaka.

Huu ni mtazamo wangu, I stand to be corrected or to be criticised.
 
Back
Top Bottom