walevi nao wanataka kuanzisha mgomo wao

Midavudavu

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
287
59
Nimewasikia mwenyewe jana kijiweni walevi wakipanga mgomo wao. "Ati haiwezekani tunanyanyaswa sana kila wakitaka kupanuo wigo wa kutoza kodi wanaanza kwanza kwa walevi halafu wavuta sigara, wengine hawaguswi. Jamani mimi nashauri tugome kunywa pombe mwezi mzima tuwakomeshe tuone kama hawatashusha bei. Na wakishusha tu tunarudi ulingoni kwa fujo" mmoja wao akasikikia akisema. Mwingine akasema "hiyo inawekana kweli na bei ikashuka tatizo bei itakapokuwa imeshushwa wengine hatutafaidi maana tutakuwa tumeshakufa kwa kiu". Nimewaacha na mada yao wanaendelea ila jioni nitapita tena kujua je, mgomo upo au la na unaanza lini?
 
Back
Top Bottom