Wale walocheza fainali za 1980 wapewe heshima kuihamasisha Taifa Stars icheze kwa hari na kujituma ili iende kwenye fainali za AFCON

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Hali ya barabara ya kuelekea Cameroon kwenye fainali za AFCON au CON 2019 ikionekana kuwa safi na siyo na matuta mengi.

Tanzania inacheza na Lesotho jumapili hii ikiwa na pointi 4 nyuma ya Uganda yenye pointi 10 na ikishinda mechi hiyo itafuzu kucheza fainali hizo baada ya miaka 38.

Hivyo umuhimu wa mechi hiyo ni wa pekee kwa kuzingatia muda mrefu amapo tangu mwaka 1980 Tanzania imekuwa ikishindwa kufuzu kucheza fainali hizo kwa kukutana na timu zingine mahiri za barani Afrika.

Huu ni wakati wa serikali kupitia wizara ya michezo kufanya kampeni ya kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali ili hata kama ikienda huko Cameroon basi inashinda angalau mechi zote za awali.

Cameroon ilishinda nafasi ya kuandaa mashindano hayo ambayo mara ya mwisho kuyaandaa ilikuwa ni mwaka 1972.

Cameroon ndio wanaoshilikia kombe la AFCON ambalo mashindano yake hayo hufanyika kila baada ya miaka miwili. Nchi ya Ivory Coast itaanda mashindano hayo kwa mwaka 2021 na Guinea mwaka 2023.

Miji mitano ya Cameroon inajianda kuzipokea timu zitakazshiriki mashindano hayo ukiwemo mji mkuu wa Younde ambapo uwanja wake maarufu wa Paul Biya ambao huchukua watu 60,000 utakuwa unaongoza kwa shughuli hiyo.

Miji mingine ni ya Bafoussam ambao ni mji wa kibiashara uliopo katikati ya nchi hiyo, mji wa Limbe ambao upo pembezoni mwa bahari ya Atlantic, mji wa Douala na mji wa Garoua uliopo kaskazini mwa nchi hiyo na ulio pembezoni mwa mto Benue.

Mji wa Douala ndo mji wenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Douala ambao ndipo timu zote zitaweza kuwasili kabla ya kuelekea makambini kwa njia ya mabasi kwenye miji mingine.

Ni wakati sasa wa kuwashirikisha wachezaji wa zamani kama Sunday Manara aka computer na Juma Pondamali ambae vituko vyake vya huko Lagos vyaelezewa vilileta hamasa kubwa kwa wachezaji wenzie.

Hivyo basi watu kama Leodgar Tenga ambae ni mwenyekiti wa zamani wa TFF, Juma Pondamali aka Mensah na Sunday Manara, huu ni wakti wa kujitokeza na kufanya kampeni kupitia runinga, radio na majukwaani.

Taifa Stars ya mwaka 1980 iliundwa na akina Juma Pondamali, Mohammed Kajole, Salim Amir, Jella Mtagwa, Omary Hussen, Thueni Ally, Adolf Rishard, Peter Tino, Mohammed Salum na Ahmed Amasha.

Wengine ni, Hussein Ngulungu, Omary Mahadhi na Maulidi Dilunga, Juma Mkambi, Mtemi Ramadhani, Leopard Tasso Mukebezi na Mohamedy Bakari Tall,

Makocha wa timu hiyo ambao wote kwa sasa ni marehemu walikuwa ni Joel Bendera na kocha kutoka Poland alieitwa Slowmir Worke..

Timu hiyo ya Taifa Stars ilipangwa kundi moja na timu kali kabisa za Misri, Ivory Coast na Nigeria.

Lakini kabla ya kwenda Lagos, Taifa Stars ilipaswa kuiondoa timu ya taifa ya Zambia ya wana KK 11 ambayo iliundwa na wachezaji kama Godfrey Chitalu, Obby Kapita, Pele Kaimana, Hakimu Mwasenge, Mosses Musoreko, Dickson Makwaza, Dick Chama ambae alikuwa ndo mkoba wao na wengine.

Ilikuwa kwenye dakika ya 80 Taifa Stars ikapata kona ilopigwa na Tasso na kumkuta Peter Tino akiwa amebanwa na mabeki wawili ambao aliwazidi kwa kuruka juu na kugonga mpira kwa kichwa na kumuacha kipa Kapambwe Mabenga akiwa anashangaa.

Baada ya goli hilo pekee raisi Keneth Kaunda alilia sana kwa uchungu mkuu wa kutoamini kilichotokea kwani Zambia walikuwa wakishambulia sana goli la Stars.

Fedha zipo na wizara inayoongozwa na Dr Mwakyembe huu ni wakati wa kujinafasi na kuisaidia timu hii itutoe watanzania kimasomaso.
 
Wapewe mara ngapi mkuu Peter tino alikuwepo hadi kwenye mechi ya cape Verde tukapigwa tatu.
.
Tatizo ni ubishororo mwingi halafu wanasahau majukumu yao.
.
Kina CR7, neymar wao ni ubishororo lakini uwanjani wanapambana haswaaa
 
Je! wakipewa hzo tunzo alafu tukaenda lizwa..tuzo zitakua zimetusaidiaje?

Siyo tuzo bali ile nafasi ya wao kushiriki kikamilifu kuihamasisha Taifa Stars.

Miaka ni mingi sana imepita na huu ndo wakti wa kufanya kweli.
 
naunga hoja 100%/

hamasa huanzia nje ya uwanja na baada ya dk 90 huwa ni matokeo tu
 
Inaweza kuwa ni 100%

Richard nakuheshimu, pitia rekodi yako uone kama taifa stars ya wakati huo ilienda kwa ushindi kutoka kwenye kundi au ilipitia kapuni baada ya timu/nchi halisi iliyopaswa kwenda kukutwa na jambo fulani. Nakusubiri hapahapa nikupe taarifa sahihi, hapa ndio nitajua unajua mambo au ni mbabaishaji tu.
 
Richard nakuheshimu, pitia rekodi yako uone kama taifa stars ya wakati huo ilienda kwa ushindi kutoka kwenye kundi au ilipitia kapuni baada ya timu/nchi halisi iliyopaswa kwenda kukutwa na jambo fulani. Nakusubiri hapahapa nikupe taarifa sahihi, hapa ndio nitajua unajua mambo au ni mbabaishaji tu.

Kwani "dark arts" haziruhusiwi?
 
Kwani "dark arts" haziruhusiwi?

We Richard ni mbabaishaji mwenye uwezo wa kujenga hoja. Hilo nimeligundua muda mrefu kwako. Nilisubiri uje na taarifa za kumezeshwa nikupe ukweli wako naona umeruka kihunzi. Amini hayohayo uliyomezeshwa kwamba Tanzania ilishiriki hiyo mwaka 80 kwa ushindi na sio hisani.
 
We Richard ni mbabaishaji mwenye uwezo wa kujenga hoja. Hilo nimeligundua muda mrefu kwako. Nilisubiri uje na taarifa za kumezeshwa nikupe ukweli wako naona umeruka kihunzi. Amini hayohayo uliyomezeshwa kwamba Tanzania ilishiriki hiyo mwaka 80 kwa ushindi na sio hisani.

Hayo ni mawazo yako na endelea kuamini hivyo.

Nimeona umebishana sana na mtu mmoja humu kuhusu masuala ya timu yetu, hivyo sikutaka kuingia huko.

Mimi nipo Maseru hapa naangalia timu yetu iingie tena kwenye fainali za 2019.

Miaka 38 ya kungoja ni mingi sana.
 
Hayo ni mawazo yako na endelea kuamini hivyo.

Nimeona umebishana sana na mtu mmoja humu hivyo sikutaka kuingia huko.

Mimi nipo maseru hapa naangalia timu yetu iingie tena kwenye fainali za 2019.

Richard narudia ww ni mbabaishaji, hii mechi ya leo umehamasika baada ya hizi promo ila huna ujualo kuhusu soka. Ww nakufananisha na wale wakristo au waisilamu wanaoenda ibadani siku ya xmas au Idd na kujifanya wanajua sana ibada.
 
Back
Top Bottom