Wakwepa kodi hawa hapa!

Sijaelewa

TIQO hata mimi nipo nyikani, sijaelewa hata kidogo. Mbona ni kuorodhesha makampuni tu na jinsi yanavyomilikiwa na yanavyomiliki? Sioni wanakwepaje kodi na kwa kiasi gani?

Madhejebu ya dini nayo yajitenge na kutumiwa kukwepa kodi; hayako salama sana kwenye hilo.
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri hii taarifa ndo imemfanya MD wa VodaCom kukimbilia Dodoma kwenda kuongea na spika wa Bunge na kuita waandishi wa habari kusema eti mpaka mwaka ujao wa fedha watakuwa wameshalipa kodi zaidi ya TShs. Bil 700 tangu 2001 na mwaka ujao wa fedha wanatarajia kulipa kodi ya Tshs. bil. 130. VodaCom ni wezi wakubwa. Kila mwaka wakati wa bunge la bajeti huwa wanakwenda Dodoma kuwaandalia wabunge sherehe kama hongo ili wafumbe midomo yao na wao (wabunge) sijuwi kama hawajaishtukia hiyo janja ya ngedere.
 
Bado Oil, Gas na uranium kuja kuibiwa na Mabwana wa CCM kutoka Ulaya. Kazi tunayo.
 
Pumbafu kabisa, makampuni ya simu za mikononi yanaongoza, sijaona Zain tu. Sina hakika kama nao ni wasafi!
 
Fisadi fisadi tu, chenge lowasa na kikwete mkapa mwinyi wote ndiyo waliowaleta hawa na kuwapa hiyo mikataba
 
TIQO hata mimi nipo nyikani, sijaelewa hata kidogo. Mbona ni kuorodhesha makampuni tu na jinsi yanavyomilikiwa na yanavyomiliki? Sioni wanakwepaje kodi na kwa kiasi gani?

Madhejebu ya dini nayo yajitenge na kutumiwa kukwepa kodi; hayako salama sana kwenye hilo.

Ndio maana nimehighlight nyekundu. Kama mpaka hapo haujaelewa pole sana.
 
Disclaimer: The views contained in this report do not necessarily reflect the views of the interfaith standing committee or the religious leaders. A significant degree of due diligence has been exercised in preparing this report but the Interfaith Committee can not be held liable for any factual errors or misrepresentation of data or otherwise which may be contained in the report.

Statements kama hizi huwa zinaniudhi sana
 
Alafu mbona mchango wa hawa "National Muslim Council of Tanzania (BAKWATA)" hauonekani haraka haraka kwenye hii report?
 
nimewekeza zangu kwenye mapenzi ths year kupunguza headaches kama hizi....
 
Back
Top Bottom