Wakuu wa Wilaya kwenye Katiba mpya tuwaondoe!

Firigisi

Member
Feb 13, 2009
91
33
Tunaweza kuondoa wakuu wa wilaya,nchi nzima bila kuathiri shughuli za maendeleo.Watendaji waliopo wanaweza kutimiza wajibu wao bila matatizo yeyote na hawa jamaa kimsingi hamna kazi yeyote wanayofanya ya maana kutu.
Kwanini napendekeza kwenye katiba mpya tuwaondoe.

1.Kupunguza gharama zisizo za lazima kwenye ma VX na majumba ya kifahari ya hawa jamaa,misharara minono na kuelekeza
hilo fungu kwenye maendelea ya sehemu husika kama maji ,nishati ,masoko bora,mikopo kwa wafanya biashara wadogo wadogo nk
Ni mzigo kwa serikali yetu

2.Wanasababisha migogoro kwenye maeneo husika baina ya serikali na wananchi wa maeneo yao

3.Uteuzi wao hauna utaratibu maalumu(criteria) isipokuwa mpaka ''mkuu wa nchi anapopendezwa'' na mtu flani hii inaleta bias
na malalamiko ya upendeleo wa vyeo na kupeana fadhila.

4.Wameshindwa kusimamia miradi ya maendelea na kushindwa kudhibiti rushwa ,ubadhirifu wa mali za umma

5.Wanafanya kazi za chama kimoja kwenye nchi ya vyama vingi

6.Kuna mgongani wa kimajukumu na kuingilia kazi za wakurugenzi

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom