drmkumba
Member
- Dec 27, 2010
- 52
- 1
Imeripotiwa na TBC1 katika kipindi cha DIRA kwamba mkuu wa mkoa wa Ruvuma ameitisha mkutano na wakuu wa shule za msingi na sekondari ili kuwatuma wawashawishi walimu waliogoma warudi kazini.Baadhi ya wakuu wa shule walitoa maoni yao na kuonekana kuwashangaa walimu wenzao waliogoma! Eti wanagoma kwa lipi! Hivi hawa wakuu wa shule wanamaslai gani makubwa yanayowafanya washindwe kuwaunga mkono walimu wenzao? Je kama itatokea serikali kusikiliza kilio cha walimu wanaogoma na kuwapandishia mishahara walimu,kuwalipa posho ya mazingira magumu na maslai mengine wakuu wa shule watakuwa tayari kujiweka kando wasipokee nyongeza hizo za mishahara? Acheni usaliti unganeni na walimu wote kudai maslai yenu ili kada ya yenu iwe na heshma.