Wakurugenzi TANESCO wasimamishwa kazi, mmoja ajiuzulu!

Unajua tungefanya kitu kimoja kuifanya Tanesco mfilisi na kuanzisha kampuni mpya Serikali tumiliki share na private company wamili angalau 25% ya share tu register hiyo kampuni kwenye soko la DSE kukwepa ujanja ujanja....

Hawa wakina IPTL waje kuomba mikataba upya.....
And thats is their mind,huko ndiko tunako elekea kimya kimya,unataka prove?
Hii hapa;

Shirika limeelekezwa lijiiendeshe kwa fedha zake,sawa?
Serikali haitaku kuinject pesa katika shirika,sawa?
Jiulize,litajiendeshaje wakati gharama za uendeshaji ziko juu kutokana na madeni?
Serikali ilipoona Mramba anataka kutumia mbinu mbadala ya kuendesha shirika,ikaingilia kati sababu ingeharibu mkakati wake.
Serikali ilicho taka,shirika likose fedha za kujiendesha,lijifie,mikataba iwe automatically terminated,ndipo lianzishwe shirika jipya lenye jina jipya.
Hapo,richmond,dowans,symbion wakina tegeta escrow,iptl na wengine watakuwa diminished.

TANESCO ITAFUFUKA TENA KWA UJIO MPYA.
 
Tanesco inatakiwa kusafishwa kabisa wala hilo halina ujanja.......

Muhongo nayeye simwamini toka alivyowakutanisha Rugemalila na Singa Singa........

Tanesco ni most corrupt govn institution in Tanzania..........

Magufuli akiendelea kuwachekea iptl na kuwalipa Milioni 400 kwa siku ..........

Kuna siku Tanesco itafilisi nchi.......
Kuna neno jema sana umelinena hapo, ila kwa Muhongo weka pending, kuna yule aliekuwa waziri wa Nishati na Madini wakati Mkwere kashika usukani.
 
Ivi unajua unachokiongea au upo kuonekana nawe umechangia? Kwamba unalipia umeme n aunakaa hadi miezi mi3 hujafungiwa? Je unazijua taratibu anaenunua vifaa ni Mramba au serikali? Fanya even a little investigation then erupt hayo yako.

Kwa hiyo wewe unaona TANESCO inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi?

Kwani suala la nani anunue vifaa limeandikwa kwenye Bible au Qur'an kiasi kwamba haliwezi kubadilishwa kama ndiyo kikwazo?

Na mbona mtu akitumia vishoka vifaa vinapatikana kama issue ni vifaa.

Juzi Bakhresa alimlalamikia Magufuli kuhusu TANESCO kushindwa kumfikishia umeme mbona hawakujitokeza na kusema ni nani anayekwamisha jitihada?

Ndiyo maana nasema TANESCO inatakiwa isukwe upya ikibidi tired minds zote zilizojaa hapo ziwe dumped.
 
Usijifariji mkuu hivi siyo vidagaa ni top management, mnaaibisha sana kujifanya mna sympathy kwa wezi.Nina msifu aliyejiuzuru kwa hiari hopeful ana set precedent Nzuri ya uwajibikaji
Mkuu sio kwamba najifariji chief.....na wala siwaonei huruma hao watu...... Ila tukitaka kweli kukomesha huo ufedhuli na kupata huduma nzuri kutoka Tanesco.....tuhakikishe tunawakamata na kuwawajibisha waliopelekea hilo shirika kufika hapo lilipo........waliotuingiza kwenye mikataba ya IPTL, ufisadi wa ESCROW na mikataba yote ya kinyonyaji......hapo tutatibu hii cancer.......pamoja na kuingia kwa huyo mkurugenzi mpya, natamani tukutane tena hapa baada ya muda uniambie ni kitu kimebadilika.
 
  • Thanks
Reactions: CDG
Matatizo ya Tanesco wa kulaumiwa kwa 100% ni CCM. Tangu enzi za chama kimoja, '94 ndipo mikataba ya kipumbavu na ya kinyonyaji ilipoanza kusainiwa.

Wa kulaumiwa ni CCM na serikali yake.
 
Jamani kwani hawa watu wamekosa nini hasa? Mbona hali ya umeme nchini imekuwa bora sana siku hizi? Tanesco wamejitahidi sana kwa kweli. Kukatika kwa umeme siku hizi imekuwa nadra sana. Sasa sijui hii misukosuko wanapewa ni kwa sababu gani! Au Magufuli amekosa wa kutumbua skaona afukuze tu alimradi? Tynaomba tuelezwe hawa watu wsnafukuzwa wamekosea nini?
Matatizo ya TANESCO yapo deeper zaidi ya huo umeme tunaopata "kwa uhakika", tatizo wala sio management, shida ipo kwa serikali ya CCM tangu enzi za chama kimoja.
 
Muhongo kapata mtu ambaye atafanya anachotaka bila upinzani.
Ndio hua anataka muhongo, yeye hutaka kua juu ya wakurugenzi wa mashirika yaliyo chini yake, Mkurugenzi yoyote ambae anapingana na muhongo hawawezi kurlewana na atafanya kila awezalo kumfitinisha ili aondolewe.

Muhongo hutaka kuongoza mashirika ya umma yaliyo chini yake kama mkurugenzi, mwinuka akikubaliana na muhongo amekwisha.
 
hili shirika sio mchezo kweli nawaambia! usifikiri kwamba Mramba amesikitika kuondoka kwake, naamini anamshukuru MUNGU kuondoka slama hata kwa hilo lililomtoa.
unapo teuliwa kushika nafasi katika shirika hili uwe tayari kufanya kazi ambayo kuisha kwake hakutakuwa kuzuri.
yupo mtu ninayemwamini anaitwa idrisa ambaye alipo hamia kutoka benki kuu kwenda nbc alifanya mabadiliko makubwa sana na hivyo alivyokuwa gavana alijitahidi pia changamoto lakini changamoto alizokutana nazo tanesiko ilikuwa balaa. hivyo ni kazi vinginevyo viongozi waliopo na waliostaafu waache kutazama maslahi yao binafsi katika uendeshaji wa shirika hili.
kila mtu ana lake ukimnyima inawezekana wanaambiwa utaona.
ni rahisi sana kutafuta ubaya wa mtu kuliko uzuri wake na kwa bahati mbaya zaidi jamii nayo inahukumu kwa kile wanachoona kipo kwa maslahi yao wakati huo..
mkurugezi pamoja na mapungufu yake lakini amefanya mengi ikiwa ni pamoja na kuahakikisha kuwa mapato ya bili kwa kiasi kikubwa sana yanakusanywa kwa kuhakikisha wateja wengi wanatumia luku.
swala la kuvuja kwa matumizi hili naweza kumtetea kwa kuwa yeyey ni fundi hivyo kwa upande huu anaweza asiuone vizuri sana.
lakini kwa kifupi ni mmoja aliyeweza kujaribu na kufanya kazi nzuri kwa kipindi chake.
 
Naona TISS walikuwa wamepiga kambi kipindi kirefu hapo Tanesco


Ni kweli Mkuu, Hawa TISS walipiga kambi muda mrefu tu hapo TANESCO wakajichanganya na hao wataalamu wa TANESCO, sasa miongoni mwa hao waliopandishwa kuna TISS humo, kazi inaendelea kama kawaida
 
Wanaoingia ndo wameoza zaidi Tanesco itaendelea kwenda hatua 2 mbele 4 nyuma halafu watapongezwa bila kuangalia hatua 2 walizopoteza
Hongera sana wewe ni great thinker.. Tanesco was moving forward ila chuki binafsi na siasa zimeamua kukataa wataalam.
Hili shirika lingekuwa independent lingekuwa mbali sana. I hate politics
 
Kama kweli Magu ni mwanaume wa chuma kama kauli mbio yake ya HAPO KAZI TU angeanza na:
1.Simamisha malipo ya mabilioni ya shilingi tunazolipa IPTL
2.Katisha mkataba wa IPTL
3.Amrisha mwenye IPTL aondoe mitambo yake chakavu nchini.
4.Serikali iuzie wananchi baadhi ya hisa za TANESCO ili kuongeza uwajibikaji
Vinginevyo utaendelea kutumbua majipu madogo tu.
 
TANESCO KWAWAKA, WAKURUGENZI WATATU WATUMBULIWA, MMOJA AANDIKA BARUA KUACHIA NGAZI




Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM



VIGOGO watatu ambao ni wakurugenzi katika Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), makao makuu Dar es Salaam, wameshushwa vyeo huku mmoja akiamua kuacha kazi mwenyewe.

Hatua hiyo imekuja siku nne tangu Rais Dk. John Magufuli atengue uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Mramba alitenguliwa uteuzi wake siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kutangaza kuridhia ombi la Tanesco la kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 8.5 kutoka 18 waliyoomba.

Wakurugenzi hao wamesimamishwa jana kupisha uchunguzi, huku chanzo cha kusimamishwa kwao kikiwa hakijaelezwa.

Taarifa kutoka ndani ya Tanesco ambayo ilithibitishwa na Kaimu Mkurugenzi mpya wa shirika hilo, Dk. Tito Mwinuka kwa simu jana, ilieleza kusimamishwa kwa vigogo hao ambao walikuwa wasaidizi wa karibu wa Mramba katika utendaji.

“Ni kweli wamesimamishwa, lakini kwa kuwa sikuwa ofisini ngoja niisome vizuri taarifa iliyopo mezani kisha niwatumie taarifa iliyokuwa sahihi kuhusiana na hilo.

“Hapa nilipo nipo ofisini na ofisa habari wangu (hakumtaja jina) tunaandaa taarifa ya pamoja, kwa maana kila mmoja anapiga simu kutaka taarifa, hivyo siwezi kuzitoa nusu nusu,’’ alisema Dk. Mwinuka.

Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni taarifa hiyo ilikuwa bado haijatumwa na alipopigiwa tena simu Dk. Mwinuka hakupokea.

Taarifa zinaeleza kwamba wakurugenzi watatu wameshushwa vyeo na kuhamishiwa katika Chuo cha Mafunzo cha Tanesco (TSS) kwa madai kuwa shirika linaboresha ufanisi wake.

Walioshushwa vyeo ni pamoja na Declan Mhaiki ambaye alikuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji aliyekuwa anashughulikia usambazaji wa umeme.

Hata uamuzi huo unachukuliwa inaelezwa kuwa Mhaiki alikuwa kwenye msiba wa kaka yake mkoani Ruvuma, marehemu Kapteni Keenan Mhaiki.

Kapteni Mhaiki aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), alifariki dunia mapema wiki hii.

Wengine walioshushwa vyeo na kuhamishwa ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji na Huduma kwa Mteja, Mhandisi Sophia Mgonja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme, Nazir Kachwamba.

Wakati hao wakipigwa na panga hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu, Watson Mwakyusa, aliamua kuandika barua kuacha kazi mwenyewe.

Januari Mosi mwaka huu, Rais Magufuli alimteua Dk. Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, baada ya kumng’oa aliyekuwa mkurugenzi wa shirika hilo, Mhandisi Mramba.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Mwinuka alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akiwa mjini Bukoba kwenye ibada ya Mwaka Mpya, Rais Magufuli alisema amekerwa na kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya watumishi wa umma kujitokeza hadharani na kutangaza au kuzungumzia mambo ya kitaifa kama uamuzi wa Serikali bila kushirikisha viongozi wao wa ngazi za juu.

Kutokana na hali hiyo, alisema watendaji hao ni miongoni mwa majipu yanayostahili kutumbuliwa.

Hatua ya kutumbuliwa kwa Mramba ilikuja siku moja baada ya Ewura kutangaza kuridhia ombi la Tanesco la kupandisha bei ya umeme.

SOURCE: Mtanzania
 
Acha uongo! Kushuhudia uongo ni dhambi kubwa sana! Acha kushuhudia uongo! Huyo Bwana alikuwa kwa mkataba na wamemwambia hawata renew mkataba wake!! Period hakuna cha zaidi
AFADHALI HUYO WA RASILIMALI WATU AMEACHIA NGAZI NASIKIA ALIKUWA ANATOA AJIRA BILA INTERVIEW, ALIKUWA ANAWAPITISHIA KWENYE TEMPORARY EMPLOYMENT KISHA ANAWAAJIRI HASA NDUGU ZAKE NA NDUGU WA MARAFIKI ZAKE.
 
Na bado tumeshaona nini?
kilichoniacha kinywa wazi ni ile kupandishwa kwa bei ya umeme na kuja nyuma kusitisha

Maswali yangu je huo mchakato ulikuwa wa kimya kimya? jibu hapana swali kulikuwa na sababu gani kutoisitisha huko anasubiri itanganzwe aje asitishe jibu sijui

hapo hapo Mramba mkataba ukasitishwa TOBA!!!!! tutayaoa mengi kwa kweli

Mungu tupe afya

"wonders never end"
Ni baada ya barua ya mnyika kusema bei ya umeme isipande
 
Tanesco inatakiwa kusafishwa kabisa wala hilo halina ujanja.......

Muhongo nayeye simwamini toka alivyowakutanisha Rugemalila na Singa Singa........

Tanesco ni most corrupt govn institution in Tanzania..........

Magufuli akiendelea kuwachekea iptl na kuwalipa Milioni 400 kwa siku ..........

Kuna siku Tanesco itafilisi nchi.......
kwa hiyo sasa kaacha kucheka cheka na milioni 400 haitalipwa tatizo ni tanesco au sera mbovu za ccm hadithi hizo kawaiambie mizoga
 
Back
Top Bottom